CCM ijitathmini takwimu za uchaguzi mkuu 2005, 2010 na 2015 hazinipi raha

mkafrend

JF-Expert Member
May 12, 2014
3,047
1,503
WanaJF, Salaam!
Nimepitia kwenye mitandao ya kijamii kwa ajili ya kupima mwenendo wa matokeo ya uchaguzi Mkuu kwa miaka mitatu ambayo ni 2005, 2010 na 2015. Kwa ujumla nimegunduwa kwamba CCM inapaswa kuongeza nguvu na ushawishi ili kijiweke katika nafasi nzuri ktk chaguzi zijazo. Aidha, hapa chini nawawekea takwimu za Tume ya Uchaguzi kwa chaguzi tatu:-

CHAMA Mwaka
2005 2010 2015
Chama Cha Mapinduzi
9,123,952 (80.28) 5,276,827 (61.17%) 8,882,935 (58.46%)
CHADEMA 668,756 (5.88) 2,271,941 (26.34%) 6,072,848 (39.97%)
CUF 1,327,125 (11.68) 695,667 (8.067%) -

Mawazo ya ufafanuzi:-
(i). Inaonesha kwamba CCM zaidi ya wapiga kura 2M kila uchaguzi - jitihada zinatakiwa kufanyika ikiwa kinapenda kubaki madarakani;

(ii). Uwekezaji kwa vijana (kundi lika) la miaka 18 - 30 unahitajika kwa kuwa huenda vijana wengi hawakiungi CCM - Mwaka 2020 kuna takriban vijana 5M wataongezeka kwenye orodha ya wapiga kura hivyo chama chenye ushawishi kwa kundi hilo kitakuwa ktk nafasi ya kushinda;

(iii). Uimara wa wapinzani unategemea zaidi muungano wa vyama zaidi ya kimoja - hivyo CCM iune muungano wa UKAWA kama threat kwa ushindi wao na ijielekeze kwenye mbinu, mkakati na uwezo. Hali hii inaweza kutumiwa pia na upinzani nchini.

Nitarudisha hii mada baada ya Oktoba, 2020
 
Yaan kwa akili yako unadhani Magufuli atapata chini ya asilimia 70%

Haijalishi atazipata vipi lakin ubao wa marais wenye hulka kama za Magufuli chaguzi zao huwa zinasomeka 90+

Cc Pascal Mayalla
 
Baeleze baelewe, tukisema sisi tunaoonekana kama CCM CCM watasema tunachukia upinzani.

Swali la Ukweli Mchungu: Je, 2020 Magufuli ana mpinzani au mshindani, au Ni Magufuli tu?!. - JamiiForums

Trend Reading: Wanaohamia CCM wasibezwe! Wanaona mbali, 2020 Majimbo yote kurejeshwa. Je tunarejea nchi ya Chama kimoja? - JamiiForums
P
 
Hakuna asiyejua', hata CCM wanajua' kuwa mwaka 2015 hawakushinda. Mwaka 2020 wataanguka zaidi lakini atatangazwa kwa kura nyingi zaidi.

Hakuna dikteta huwa anatangazwa kuwa mshindi kwa ushindi chini ya 80%. Wa kwetu, kama ilivyokuwa kwa mwenzie, atatangazwa kwa 90+%
 
WanaJF, Salaam!
Nimepitia kwenye mitandao ya kijamii kwa ajili ya kupima mwenendo wa matokeo ya uchaguzi Mkuu kwa miaka mitatu ambayo ni 2005, 2010 na 2015. Kwa ujumla nimegunduwa kwamba CCM inapaswa kuongeza nguvu na ushawishi ili kijiweke katika nafasi nzuri ktk chaguzi zijazo. Aidha, hapa chini nawawekea takwimu za Tume ya Uchaguzi kwa chaguzi tatu:-

CHAMA Mwaka
2005 2010 2015
Chama Cha Mapinduzi
9,123,952 (80.28) 5,276,827 (61.17%) 8,882,935 (58.46%)
CHADEMA 668,756 (5.88) 2,271,941 (26.34%) 6,072,848 (39.97%)
CUF 1,327,125 (11.68) 695,667 (8.067%) -

Mawazo ya ufafanuzi:-
(i). Inaonesha kwamba CCM zaidi ya wapiga kura 2M kila uchaguzi - jitihada zinatakiwa kufanyika ikiwa kinapenda kubaki madarakani;

(ii). Uwekezaji kwa vijana (kundi lika) la miaka 18 - 30 unahitajika kwa kuwa huenda vijana wengi hawakiungi CCM - Mwaka 2020 kuna takriban vijana 5M wataongezeka kwenye orodha ya wapiga kura hivyo chama chenye ushawishi kwa kundi hilo kitakuwa ktk nafasi ya kushinda;

(iii). Uimara wa wapinzani unategemea zaidi muungano wa vyama zaidi ya kimoja - hivyo CCM iune muungano wa UKAWA kama threat kwa ushindi wao na ijielekeze kwenye mbinu, mkakati na uwezo. Hali hii inaweza kutumiwa pia na upinzani nchini.

Nitarudisha hii mada baada ya Oktoba, 2020

Usiwe na shaka, kwa sasa mwenyekiti wa ccm amehakikisha vyombo vya kimamlaka vinafanya anavyotaka. Hivyo tume ya uchaguzi itawatangaza wagombea wa ccm, na vyombo vya dola vimekabidhiwa jukumu la kuhakikisha mgombea atakayetangazwa ndio anapita. Uamuzi wake ni kuwa yeye atangazwe kwa 90%+, na wabunge wa ccm wawe 85% bungeni ili wamuongezee muda wa kukaa madarakani. Hayo ndio yatakuwa matokeo, nadhani hapo utakuwa umefurahi.
 
Sawa mimi nimeleta hii hoja kwa kuzingatia chaguzi tatu - tusibeze
 
Back
Top Bottom