VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
CCM ni chama chetu. Tumekuwemo humu miaka na miaka. Tunakipenda na kukitumikia. Uchaguzini, hukipigania. CCM inaunda Serikali. Serikali ni zao la CCM yetu. Ni zao la tunachokiamini kama chama tawala.
Kinachofanywa na kusemwa na Serikali, kina baraka za CCM. Na kinyume chake pia. Siasa za uongouongo na utapeli zimepitwa na wakati. Siasa za kusema tui ni maziwa;kitumbua ni andazi zimepita. Hazina nafasi tena.
Kauli hufuata baada ya tafakuri. Hakukuwa na haja ya kutangaza kuwapora mihuri Wenyeviti wa Serikali za Mitaa halafu kuahirisha. Hakukuwa na hoja wala haja ya kusema chakula hakitagawiwa kwa wahitaji halafu tani milioni 1.5 ziko njiani kugawiwa.
Siasa la kulaghai, kurubuni, kutapeli, kudanganya,kigeugeu na kughiribu zimepitwa na wakati. Karne hii ni siasa za ukweli. Ukweli utuongoze. Tuseme baada ya kutafiti. Tuseme tukiwa tayari ni well informed. Siasa za kekundu tuwaachie wapinzani.
Mwafaaaa!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam