CCM, iheshimuni KATIBA ambayo ndiyo sheria mama.

mcoloo

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
918
1,401
Majuzi mahakama ilitoa maamuzi kwenye kesi ya msingi iliyo funguliwa na Bob Wangwe iliyo kuwa ikipinga wakurugenzi kusimamia uchaguzi.
Mahakama ilitoa maamuzi kwa kuzingatia katiba ambayo ndiyo sheria mama , inayo jieleza wazi kabisa kuwa wakurugenzi hawaruhusiwi kusimamia chaguzi zinazo endana na vyama vingi vya siasa.
Jambo la kushangaza eti hili nalo CCM wanalikatia rufaa kwa kupinga maamuzi ya mahakama kuwa haikuwatendea haki.
CCM lazima itambue kuwa watanzania wa sasa wameelimika na wanafahamu sana haki zao kuliko wao CCM wanavyo dhani.
CCM ni chama tawala, ambacho kimekuwa madarakani kwa muda mrefu kiasi kwamba hakipaswi kuonyesha umbumbu wa kujifanya kuwa hawajui kile kinacho elezwa na katiba, huu ni uzwazwa ulio pindukia.
CCM wanadhani kuwa leo hii bado yupo mtanzania asiyejua kuwa mikutano ya vyama vya siasa ni haki kufanyika tena bila ya kuomba . ili mradi tu watoe taarifa kwa ajili ya kupewa ulinzi.
CCM wandhani kuwa ni mtanzania gani asyejua kuwa katiba iko wazi kuhusu watumishi wa serikali kuto kuhusika na siasa.
Kiujumla ni kwamba CCM miaka mitano mlioipata awamu hii imeonyesha wazi kuwa uwezo wa kuiongoza nchi umewaishia na wala hamfai tena kupewa dhamana hii.
CCM imegeuka kuwa adui mkubwa wa katiba ya nchi hii, katiba ambayo ndiyo jicho la kuliongoza taifa, ila wao wameamua kulitia hilo jicho chongo.
Kama uliapa kusimamia katiba na tunaona wazi kuwa umeshindwa kusimamia kiapo chako kuna haja gani ya kukuongezea muda? Lilo baki ni kupigwa chini ili waje watakao iheshimu katiba ya nchi na watanzania kiujumla.
 
Ni dhahiri CCM hawatako tayari kukubali kukabidhi madaraka ya kuongoza nchi hii kwa chama kingine(upinzani).
Hawa ni mpaka wapigwe na confusion kama Mungu alivyozipiga Misri, Tunisia, Sudan n.k

Situation ya Zanzibar, ndio case study.
 
Back
Top Bottom