Elections 2010 CCM ifungue kesi ya Kikatiba dhidi ya CHADEMA kuwalazimisha kutambua matokeo!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
Nilikuwa nafikiria namna nyingine ya kutatua mgogoro uliopo sasa hivi kati ya CCM na CHADEMA kuhusu suala la matokeo ya Urais. Nimefikiria kuna kesi mbili ambazo nikiwasikiliza CCM na wale wenye kulaani kitendo cha "kutoka nje" kilichofanywa na CHADEMA wanaweza kuja nazo.

1. Kesi ya Kikatiba ya kuwalazimisha CHADEMA kumtambua Rais Kikwete kwa vile waliamua kutoka wakati Rais ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu na Mkuu wa serikali ya JMT alipokuwa anazungumza. Kwa vile kitendo kile kimeelezewa na Kapt. Chiligati kuwa kilikuwa kinavunja Katiba basi mantiki inataka wale wanaotetea Katiba wachukue hatua za kuitetea Katiba hiyo kwa kufungua kesi ya Kikatiba dhidi ya CHADEMA.

2. Kesi ya pili nayo ni ya Kikatiba vile vile nayo iwe ni ya kulazimisha CHADEMA WATAMBUE matokeo ya Uchaguzi wa Rais kwani kutokutambua matokeo ya kura za Urais yanatuleta kwenye tatizo la kwanza hapo juu. Kwa vile CCM na wengine wanaamini kuwa kura zilizopigwa na kutangazwa zilikuwa ni halali na hakuna mashaka yoyote basi jawabu pekee ni kuwalazimisha CHADEMA KUKUBALI matokeo hayo. Katiba inazuia kuhoji kutangazwa kwa Rais lakini HAKUZUII kutetea kutangazwa huko mahakamani! Hivyo, CCM na wanasheria wake wafikirie namna ya kuthibitisha au kuutetea ushindi mahakamani. Hapa napendekeza wao CCM waitishe kura zote za Urais kutoka majimbo yote ili kuonesha kiasi cha kura alizoshinda. Watakapofanya hivyo watafunga kelele zote za Chadema na kuwaridhisha Watanzania kuwa hakuna kura zilizochakachuliwa. Hapa itakuwa ni goli kama la Maradona au lile goli la elfu moja la Pele.

Kwa ufupi naamini CCM wanaweza kutoa mfano wa utawala wa sheria kwa kwenda mahakamani kufungua kesi hizo za Kikatiba.
 
sijakusoma kaziyamahama nikufafanuwa sheriya sikumrazimisha mtuhumiwa.nakusumatokeoyaraisi hakunachombochochote kikatiba kuhojimatokeo yaraisi sijuwi ccm wakiendamahakamanikuirazimisha chadem wakubarimatokeo itakuwavunjakatiba? au nikuiungakatiba? tatizokatibainamfumowa wachamakimoja dawakatibaibadirishwenatumeyauchaguzi hatutakivurugu turishazoeaamani
 
Wataanzia wapi mwanakijiji! Hawaogopi kwamba mengi yataibuliwa wakati wa kesi yanayoweza kumfanya raisi afe kwa shinikizo la damu? Yangu macho labda watakuwa na ujasiri wa makamba na kufuata ushauri wako!
 
CCM wanajua dhahili matokeo ya kura siyo tu ya ubunge na udiwania bali na ya uraisi hususani yametengenezwa toka wanakokujua hivyo
hawatakubali kamwe kwenda mahakamani kujimaliza.Ninachokiona ni ccm kujaribu kupima upepo umekaaje halafu wajifanye kana kwamba hawajwahi kutamka walichotamka. Nduu yangu ccm siyo tu ni wasanii bali ni kituko.Tuvute subura tu nakwambia TIME WILL TELL!
 
Naomba tuungane kutaka CCM ifungue kesi ya kuwalazimisha CHADEMA kutambua matokeo.. na kumtambua Kikwete.. lets join hands wale wote tunaotaka utawala wa sheria na ambao tunaamini kitendo cha Chadema kutoka Bungeni hakikuwa sahihi..
 
hakuna "mgogoro uliopo sasa hivi kati ya CCM na CHADEMA"

get your subject right
 
Sidhani kama ccm wanaweza coz watakuwa wanahofia ushahidi walionao chadema utakuwa ni wa aina gani, dunia isije jua waliyoyafanya katika kukirudisha chama chao madarakani...
 
Katiba inazuia kuhoji kutangazwa kwa Rais lakini HAKUZUII kutetea kutangazwa huko mahakamani!

Tatizo Mzee Mwanakijiji.................Mahakama hazina mamlaka ya kisheria kuingilia majukumu ya NEC yakiwemo kumtangaza Raisi aliyeshinda.........hivyo kwa mantiki hiyo mahakama haiwezi kupokea migogoro itokanayo na maamuzi ya NEC yawe ni kutambua au hata kutotambua maamuzi ya NEC kuhusiana na uraisi............................kwa hiyo hayo yote uliyoyandika hapo juu hayatekelezeki kwa maana ya kisheria...................................

lakini ipo sababu nyingine kwa nini CCM haina sababu ya kuumiza kichwa na kelele za Chadema...........................ni kuwa Chadema wamkubali au wamkatae JK bila ya kwenda mahakamani ni sawsawa kabisa na kutwanga maji kwenye kinu.............................CCM wao watakaa kimya na kuvuta pumzi tu hawana jingine la kufanya................................

Chadema kama wana ushahidi wa kuwa NEC ilikiuka taratibu za kisheria katika kumtangaza JK na ushahidi wanao basi itabidi watinge mahakamani na vinginevyo hizo purukshani nyingine ni ubabaishaji tu...mwaka 1995 mahakama hiyo hiyo ilikwisha sema pamoja na Ibara ya katiba inayokataza kuchunguza matokeo yaliyotangazwa na NEC lakini mahakama yaweza kuichunguza NEC kama ilifuata sheria katika kumtangaza aliyeshinda Uraisi................
 
hii itakuwa si mada ya kuhoji kutangazwa "kwake" itakuwa ni kesi ya kuwalazimisha chadema wamtambue Rais na kutambua matokeo ya uchaguzi. Katiba haikatazi kesi ya kulazimisha watu kumtambua Rais.. Katiba inakataza kuhoji kuchaguliwa kwa yule aliyetangazwa kuwa Rais. Kwa hiyo CCM ina uwezo na haki ya kufungua kesi.. naomba tuwasihi walete kesi hiyo..
 
CCM waoga, hawatathubutu! Lakini ni kwa jinsi gani tungaliweza kuwashawishi wakafungua kesi. Maana kwa uhakika, Chiligati na wenzie wengi wanaamini CHADEMA wamevunja sheria tena sheria mama, sasa mahakama ingesaidia na ingewaamuru CHADEMA wamkubali aliyetangazwa kuwa Raisi!
 
Unaruhusiwa kuleta mada yako iliyoenda shule kwa level yeyote ile!
hatumuongelei mchangia maoni kwamba alete mada zake tofauti, tunaongelea mada hii, ambayo inaambiwa haijaenda shule hata ya kata!
 
hii itakuwa si mada ya kuhoji kutangazwa "kwake" itakuwa ni kesi ya kuwalazimisha chadema wamtambue Rais na kutambua matokeo ya uchaguzi. Katiba haikatazi kesi ya kulazimisha watu kumtambua Rais.. Katiba inakataza kuhoji kuchaguliwa kwa yule aliyetangazwa kuwa Rais. Kwa hiyo CCM ina uwezo na haki ya kufungua kesi.. naomba tuwasihi walete kesi hiyo..

Mwanakijiji nimekupata sana,

Hapa unataka kuwakaanga CCM kwa mafuta yao wenyewe!

Kwanza, CCM wakienda mahakamani na kesi ikafikia hatua ya kuwataka mawakala wote wa CCM walete zile fomu orijino za matokeo ya uchaguzi ili ziwe-compared na zile za mawakala wa CHADEMA kamwe hawatafanya hivyo.

Pili, sasa hivi CCM wana-operate kama-disjointed outfit, ndio maana unaona Chiligati anasema hivi, mara Makala anasema vile, halafu dakika hiyohiyo yule katibu wa Dar anasema vingine!. Inawezekana kabisa walio na priveldge ya kuelewa ukweli wote wa yaliyotokea kwenye uchaguzi ni vigogo wachache sana ndani ya CCM na NEC. Na vigogo hao kamwe hawatataka wanachama wao watambue jinsi gani walivyoumbuka kwenye kura!

Tatu, ningependa tu kuona maandamano ya CCM maaana huo ndio utakuwa mwanzo wa yale yaliotokea Kenya....
 
Mwanakijiji,ni vigumu kwa ccm kukusanya matokeo yote na kuyahoji mahakani,ukifanya hivyo tayari umehoji matokeo ya urasi na inapelekea kuvunja katiba
pia kuhusu chadema kutoka nje ni utaratibu wa kawaida kwani hakuna sheria inayo mlazimisha mtu kumsikiliza raisi akitoa hotuba ili mradi maamuzi yako yasivunje uhuru wa mwingine kumsikiliza raisi,hivyo pale kwa chadema hakuna issue,tambuwa kuwa hata wabunge wa ccm wangetoka nje ni ruksa ni taratIbu za bunge kuwa na kamati za vyama wakati kunajambo linaendelea bungeni ni utaratibu walio jiwekea tangu kitambo,
hivyo hakuna kesi yeyote itakayo tengenezwa juu ya matukio hayo mawili

mapinduziiiiii daimaaaaaaaaa
 
hatumuongelei mchangia maoni kwamba alete mada zake tofauti, tunaongelea mada hii, ambayo inaambiwa haijaenda shule hata ya kata!

Sasa hapo amechangia nini?
Ikiwa ameona haijaenda shule basi na alete yake kama hawezi kaa kimya kuliko kusema haijaenda shule.
 
Back
Top Bottom