CCM Ifanyiwe Marekebisho?!

jmushi1

Platinum Member
Nov 2, 2007
24,985
22,512
Ndugu zangu wana JF sina haja ya kuorodhesha yale yote ambayo CCM imeyakwamisha kwenye taifa letu hili changa!

Ila nina machache muhimu ambayo kamwe hatuwezi kuyafumbia macho

Kabla ya kuyataja nataka niwape changamoto wana CCM kuwa huu ni wakati wa kukaa chini na kutafakari namna ya kukifanyia mabadiliko chama chao ili badala ya kubakia na fikra za kimapinduzi tuwe sasa na fikra za kumove forward hence maendeleo!

Bila longo longo nyingi...Yafuatayo ni machache yanayokwamishwa na CCM:

1)Muafaka wa Zanzibar

2)Maamuzi yenye maslahi ya kitaifa bungeni.

3)Kuwalinda na kuwatetea mafisadi.

4)Kumbana Mh Rais kwenye maamuzi yenye kuhitaji uzalendo na utaifa.

5)Kuwapokea watuhumiwa wa ufisadi kwa moyo mkunjufu

Listi ni kubwa ila naanzia hapa!

JE CCM WAFANYE MABADILIKO?
 
Pemba wataka kujitenga

2008-05-11 11:58:19
Na Mwandishi wetu, Pemba


Wafuasi wa Chama cha Wananchi (CUF) Kisiwani Pemba, wameendeleza tishio la kutaka kujitenga na Unguja, ikiwa ni shinikizo la kusainiwa kwa makubaliano ya muafaka kati ya chama hicho na Chama cha Mapinduzi (CCM).
Wakiandamana katika barabara za Chake Chake, kupitia barabara ya Macho Manne kuelekea viwanja vya Gombani ya Kale, ambako viongozi wa juu wa CUF walihutubia, wafuasi hao walikuwa wakiimba kuwa hawataki muafaka, hawataki Serikali ya Mseto Zanzibar na kwamba wanataka Pemba iwe huru kuendesha mambo yake.

Aidha, wametangaza mgomo wa kusafirisha mazao ya chakula kwenda Unguja. Pemba inaaminika kuwa eneo kuu la uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara, visiwani humo.

Kauli hizo zimo katika risala ya wafuasi hao, iliyosomwa na Bi. Rizik Omar, baada ya maandamano yaliyofanyika jana mjini hapa.

Maandamano hayo ambayo ni mfululizo wa maandamano yaliyopangwa kufanywa na CUF kwa nyakati tofauti nchi nzima, yalianzia Macho Manne hadi Gombani, na kupokewa na Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba.

Bi. Omar, alisema mkazi yeyote wa Pemba atayekiuka tamko hilo, atachukuliwa hatua ya kutengwa, kwa vile atakuwa hana uchungu na kile walichokiita kuwa madhila wanayofanyiwa (wakazi wa Pemba) na serikali yao.

Kisiwa cha Unguja kinategemea zaidi ya thuluthi moja ya mazao ya chakula na matunda kama ndizi, muhogo, viazi, embe na mabungo kutoka Pemba.

``Sio ruhusa kusafirisha hata pilipili kwenda Unguja,``alisema Bi. Omar huku akishangiliwa na maelfu ya watu waliojitokeza kushiriki maandamano hayo.

Aidha, wakazi wa kisiwa hicho, wametakiwa wasipande meli za Mv Maendeleo na Mv Mapinduzi, zinazomilikiwa na serikali, ili kuathiri mapato ya vyombo hivyo.

Makamu Mwenyekiti wa CUF, Bw. Machano Khamis, alisema kwa kuwa uamuzi wa mgomo ni msimamo wa wanachama, CUF itawaunga mkono kwa kuwa ni moja ya njia za kuhakikisha haki inapatikana.

Alisema pamoja na kuwa uamuzi huo utamuathiri na yeye kwa vile anaishi Unguja, lakini yupo tayari kufa kutokana na njaa, alimradi haki ya wananchi wa Zanzibar ipatikane.

Naye Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, alisisitiza kuwa CUF imeshafunga mjadala wa mazungumzo ya muafaka, na haipo tayari kurejea kwenye mazungumzo na Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Yusuf Makamba.

Alisema hivi sasa CUF inamsihi Rais Jakaya Kikwete, kumkutanisha (Maalim Seif) na Rais Amani Abeid Karume.

``Ni kikao hicho ndicho kitakachokuwa na uwezo wa kutatua tatizo la Zanzibar na si kuendelea na mzaha wa kuwa na kikao na Makamba,`` alisema.

Maalim Seif, alisema katika utatuzi wa migogoro duniani zipo njia tatu za kidikteta, kura ya maoni na mazungumzo.

``Panapotumika moja kati ya hizo njia tatu, basi nyingine zinakufa moja kwa moja na hazifai tena. Lakini kinachofanywa na CCM hapa ni usanii ambao hauonekani pengine duniani,``alisema.

Kwa upande wake, Profesa Lipumba, pamoja na kusisitiza kusainiwa kwa muafaka, alilaani kitendo kilichofanywa na viongozi wa CCM mkoani Shinyanga, kumpa mapokezi aliyekuwa Waziri wa Miundombinu, Bw. Andrew Chenge.

``Kitendo cha kumpokea Chenge kwa furaha ya nyama choma na pombe, ni kuikejeli misingi ya utawala bora na kuidharau ahadi ya Rais Jakaya Kikwete kutaka kupambana na mafisadi,`` alisema.

Mapema, wanachama wa CUF waliandamana wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe kama : Comoro na Kenya ni kwa wenzako�Zanzibar ni kwako; CCM msifanye usanii katika mazungumzo, wekeni mbele maslahi ya Taifa, Zanzibar ni ya Wazanzibari na Zanzibar ni sehemu ya Watanzania.
  • SOURCE: Nipashe
 
Mambo yaendelea kuwa mambo! Highlights pekee zinatosha kukupa ujumbe kamili wa makala hii!

CUF bado yalia na safari za JK

na Kulwa Karedia



SIKU moja baada ya Ikulu kutoa taarifa ya mafanikio ya safari za nje zilizofanywa na Rais Jakaya Kikwete, Chama cha Wananchi (CUF) kimeitaka serikali kutangaza pia gharama zinazotumiwa na Rais katika safari za nje.
Akizungumza na ‘Tanzania Daima’ jana, kiongozi Upinzani Bungeni, Hamad Rashid Mohamed, alisema gharama zinazotumiwa na Rais Kikwete kwa safari za nje ni kubwa, hivyo zinapaswa kuwekwa dharani kila mtu azijue.
“Nimesikia kwamba Ikulu inasema ziara za Rais Kikwete nje ya nchi zimekuwa na mafanikio makubwa. Haya ni yapi? Tunapaswa kuelezwa ukweli kwanza wa gharama anazotumia,” alisema kiongozi huyo.
Alisema Ikulu imekuwa ikifanya siri kubwa ya gharama zinazotumiwa na Rais wakati ni kodi ya wavuja jasho, hivyo kabla ya kufurahia mafanikio, wananchi wanapaswa kuelezwa gharama zilizoleta mafanikio hayo.
Alisema kwa vile Rais amechaguliwa na wananchi kwa ajili ya kuwatumikia, anapaswa pia kuwa wazi na kupunguza safari za nje, ili kushughulikia masuala ya ndani zaidi.
“Rais tumemchagua kwa ajili ya kushughulikia zaidi masuala ya ndani…sasa inakuwaje kila leo unasikia yuko safari tena nchi za mbali. Hii inatupa picha gani tunao mtegemea?” alihoji Hamad.
Alisema kitendo cha kuwa na safari nyingi kimesababisha Rais Kikwete kushindwa kushughulikia kwa kina suala la mpasuko wa kisiasa Zanzibar, ambalo sasa linaekea kuchukuwa sura mpya baada ya mazungumzo ya kusaka mwafaka kuingia dosari.
“Tuliamini kwamba Kikwete kama alivyowahi kuahidi kama anageshughulikia suala hili kwa kina, sasa imebaki mvutano tu, huku hatima ya mazungumzo baina ya CCM na CUF yakibaki kitendawili,” alisema Hamad.
Safari za Rais Kikwete nje ya nchi zimekuwa nyingi lakini faida yake imekuwa kidogo, tofauti na Ikulu inavyodai kupata mafanikio makubwa.
“Hata zile fedha zilizosainiwa na Rais Gorge Bush wa Marekani hazikutokana na ziara ya Rais Kikwete, bali ni mpango wa Serikali ya Marekani katika kampeni yake ya kusaidia nchi masikini…hata hapa pia tunapaswa kuelezwa ukweli,” alisema Hamad.
Alisema hali hiyo imekuwa ikichangia kila mwaka bajeti ya serikali kuongezeka huku ikitegemea zaidi wafadhili. “Nakwambia kwamba hivi sasa serikali imeelekea kuelemewa na mzigo huu mzito, wakati serikali ya Mwalimu Nyerere haikuwa tegemezi kiasi hiki, licha ya kukabiliwa na matatizo mengi ya uchumi enzi hizo na alikuwa akitegemea asilimia 6 tu kutoka kwa wafadhili,” alisema Hamad. Juzi Ikulu kupitia kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano, Salvatory Rweyemamu, ilitoa taarifa kuwa ziara za Rais Kikwete nchi za nje zimekuwa na mafanikio makubwa, ikiwa ni pamoja na msaada wa dola milioni 698 kupitia Mpango wa Milenia (MCC) kutoka Serikali ya Marekani.
 
Pia wale ambao wana amini kuwa ni vigumu kwa CCM kufanya mbadiliko na hivyo wasirudi madarakani mnakaribishwa na maoni yenu pia kwa vielelezo.
Shukran.
 
Marekebisho pekee ambayo CCM inahitaji kwa sasa ni kupunguziwa au kuondolewa kabisa mzigo mzito wa kuongoza serekali yetu ambao niwazi umewashinda.
 
Mkuu unajua kinachotushinda kutumia katiba ya nchi kuhakikisha watu kama Mkapa na wale waliokula pesa za umma wanafikishwa katika vyombo vinavyohusika ndicho hicho hicho kinawafanya CCM wasiweze kutekeleza majukumu yao.

Nilichokiona tunatakiwa kuidentify Adui yetu ni nani. Watanzania tukiangalia vizuri tuna adui mmoja tu nao ni MAFISADI. CCM kama chama hakina uwezo wa kubadili jambo lolote kwa sababu kuna mafisadi wameteka chama.

Kinachohitajika ni kupambana na fisadi mmoja mmoja.

Mafisadi wanafurahia tunapowaunganisha kwenye chama maana tunapambana na wana CCM badala ya wahuni moja kwa moja.

Nafikiri sasa tutafte strategy za kuangalia MAFISADI moja kwa moja bila kupitia CCM.
 
Mimi kwa maoni yangu CCM inabidi ife au isambaratike maana ni chama ambacho kimejaa wahuni na mafisadi hasa katika nafasi za juu za uongozi ndani ya chama hicho ambao siku zote wako radhi na watasimama kidete kutetea maslahi ya CCM kuliko yale ya Tanzania.

Na kuna mambo yenye kuthibitisha ushahidi wa hili yakiwemo mikataba isiyo na maslahi kwa Tanzania, kushindwa kuwafilisi na hatimaye kuwafungulia mashtaka mafisadi wote wakiwemo fisadi Mkapa, Lowassa, Sumaye, Mramba, Mkono, Karamagi, Msabaha, Chenge na wengineo chungu nzima.

Kwa kumalizia CCM haiwezi kurekebishwa bali ife au isambaratike na kutoa chama/vyama kingine/vingine.
 
wakati huu si majaribio na nchi yetu hATUWEZI KUMPA MTU TUSIEMUAMINI KUTUONGOZA HATUKO TAYARI KUWA KAMA YALIOTOKEA KENYA.

NI CCM PEKEE KWA SASA NDIO INAYOWEZA KURUVUSHA
 
wakati huu si majaribio na nchi yetu hATUWEZI KUMPA MTU TUSIEMUAMINI KUTUONGOZA HATUKO TAYARI KUWA KAMA YALIOTOKEA KENYA.

NI CCM PEKEE KWA SASA NDIO INAYOWEZA KURUVUSHA

Unaposema maneno kama hayo hapo juu tungependa pia utumabie CCM inafaa in which terms!

Rejea sababu zote zinazopelekea kukwama kwa maendeleo, Vita ya ufisadi pamoja na mwafaka wa Zanzibar!

Naomba uje na hoja tafadhali..JF HII MKUU!
 
wakati huu si majaribio na nchi yetu hATUWEZI KUMPA MTU TUSIEMUAMINI KUTUONGOZA HATUKO TAYARI KUWA KAMA YALIOTOKEA KENYA.

NI CCM PEKEE KWA SASA NDIO INAYOWEZA KURUVUSHA


huh!? What? :confused:
Hiki chama cha wahuni na mafisadi kinachosadia katika kuiangamiza Tanzania kitatuvusha katika lipi hasa? Mabilioni ya shilingi yanakwapuliwa kila kukicha sasa hivi tunazungumzia shilingi trilioni moja na hizi ni katika kipindi kifupi tu, halafu unadai kamba CCM ndiyo chama pekee kitakachoweza kutuvusha? Are you in your right mind? :confused:


Haya ni ya maneno ya Jaji Waroba ambaye aliwahi kuwa Waziri Mkuu Wa Tanzania


Vigogo wazito waanikwe, sheria isivunjwe


Asema viongozi wetu ni dhaifu

Amtaka Mkapa akajitetee mahakamani

KATIKA kauli ambazo zitawashitua watawala, Waziri Mkuu wa zamani, Jaji Joseph Warioba, amesema nchi ina viongozi dhaifu, umma unanyonywa, rushwa imeongezeka, wezi wa fedha za EPA waanikwe na Rais Msitaafu, Benjamin Mkapa akajibu tuhuma zake mahakamani.

Katika mahojiano maalumu na Raia Mwema, Warioba amesema kuna dalili ya kuwapo watu wakubwa nyuma ya kashfa ya fedha zilizopotea katika sakata la EPA na kwamba yaliyotokea ni wizi wa hali ya juu na baadhi wameghushi na kwamba hatua za kisheria ni lazima zichukue mkondo wake.

"Sina hakika kama wote wamezinduka hivi. Jana walikuwa wanasema hakuna rushwa, hakuna ufisadi. Leo ndiyo wako msitari wa mbele wanatafuta mafisadi na ukiangalia zaidi ni viongozi. Na hasa wabunge ndio wanaongoza vita hii. Ni vizuri Bunge liongoze lakini je, tunawaamini wote? Kwamba nia yao hasa ni kumaliza ufisadi au kuna sababu nyingine?

"Ikifika mahali tuwaulize hawa ambao sasa wanaonekana wana uchungu sana na ufisadi. Mwaka 2005 tuliona yaliyotokea. Hivi ni wangapi ambao wako safi? Mwananchi akimwuliza mbunge wake, na hii inawezekana kwa zaidi ya nusu ya wabunge, kwamba mbona wewe ulikuja na fedha nyingi sana kwenye uchaguzi na wewe si tajiri, ulizipata wapi?" anahoji Jaji Warioba.

Hilo ni suala muhimu, hapo ndipo uongozi unapohitajika. Huwezi kukwepa. Uongozi kazi yake ni kuamua mambo mazito, na wakati wote unaweza kuwa na wasiwasi, lakini unaamua kwa maslahi ya taifa. Hata kama katika kuamua huko unahisi kuwa kuna baadhi watakulaumu. Usiogope lawama, dira yako iwe kuwa hii ni kwa manufaa taifa ama hapana."


Je kuna mantiki yoyote ya Chama cha Mafisadi kuendelea "kutuongoza"? "Wanatuongoza" katika lipi hasa? Kuna umuhimu gani wa kuendelea kuongozwa na chama na viongozi dhaifu inapokuja kwenye maslahi ya nchi?
 
Halafu jambo lingine la kushangaza ni wale wanaojiita wana CCM ambao tulitegemea wangeikemea CCM ili ifanye mabadilko badala yake wanaikumbatia na kuanzisha matawi ya vyama ughaibuni ili na wao wawe vijifisadi vidogo vidogo badala ya kuukemea ufisadi!
 
Halafu jambo lingine la kushangaza ni wale wanaojiita wana CCM ambao tulitegemea wangeikemea CCM ili ifanye mabadilko badala yake wanaikumbatia na kuanzisha matawi ya vyama ughaibuni ili na wao wawe vijifisadi vidogo vidogo badala ya kuukemea ufisadi!

lako hilo, utaranda randa nalo, ss tunajiandaa kutoa somo 2010
 
lako hilo, utaranda randa nalo, ss tunajiandaa kutoa somo 2010

Somo lipi mtakalolitoa 2010!? :confused:
Somo la jinsi Chama cha Mafisadi na wahuni kilivyofanya ufisadi wa kuiangamiza Tanzania kwa kukwapua mabilioni ya shilingi na kusaini mikataba isiyo na maslahi kwa Tanzania?
 
huu ni uwoga wa kisiasa, MWALIMU nyerere aliwahi kusema c cm siyo mamake angeweza kuhama wakati wowote, angekuwepo wakati ndoo huu, pia huo msemo bila ccm imara nchi yetu itayumba ni msemo wa nyerere, ccm aliyoanzisha nyerere siyo hii, ilikuwa na watu kama akina makweta, elinawinga, kawawa, profesa mmari,sokoine,etc, hii ccm ya akina lowasa, chenge, rostamu,siyo ile ya mwalimu, inaweza isiwepo na nchi haitayumba
 
wakati huu si majaribio na nchi yetu hATUWEZI KUMPA MTU TUSIEMUAMINI KUTUONGOZA HATUKO TAYARI KUWA KAMA YALIOTOKEA KENYA.

NI CCM PEKEE KWA SASA NDIO INAYOWEZA KURUVUSHA

Mkuu hapa umechemusha kwa taharifa Kenya wako ahead of us. Itatuchukua muda mrefu wakati wao watakuwa wanakimbia sisi bado tutakuwa tunatambaa.

Hayo maneno unayoyasema sasa aliyasema mwalimu 1995, tena yeye alitumia maneno makali sana ambayo kwa kweli labda kwa kuwa alikuwa anaheshimika. Alisema hawezi kuacha Nchi yake ikaongozwa na Mbwa.

Ilikuwa ni statement kubwa sana ambayo kwa kweli ilinitoa chozi. Lakini angelikuwepo sasa maana aliyekuwa anampigia debe alikuwa Mkuu Benjamini William Mkapa, Swali langu kwake je aliyewaamini na kuwaita wapinzania mbwa wamefanya nini?

Mkuu swali kwako afadhali wapinzani hawajaingia ukaona utawala wao. Waliopo tayari wana kila sifa mbaya duniani tufanyeje. unless unashare mkate na wao!

Mimi wito wangu ni kwamba hii kazi itafanywa na watanzania wenyewe, hakuna mtu atatoka uingereza akatuletea maendeleo. Ni jukumu la watanzania kuwakataa watawala wasiokuwa na vision.
 
wako watanzania tele wanaoweza kuingoza nchi hii vema, tatizo ni kuwa nchi iko likizo au imezingirwa na mbwa mwitu yaani mafisadi, tukimaliza mapambano na mafisadi, watajitokeza watanznia wema wenye uchungu na nchi yao, wote waliko madarakani hat ajk mwenyewe amewekwa na mafisadi, yameanza kujiengua mmoja mmoja yataisha na nchi itarudi kwa wenyewe, nina imani na anachofanya msekwa, kwamba anasaka vijana wenye vipaji toka vioni kwa ajili ya uongozozi wa baadaye wa taifa letu, tumpe muda
 
Taarifa nilizonazo ni kwamba kuna grassroot movement ya kuindoa CCM madarakani!

Je wana cha kufanya kuwa win back wananchi?

Na kama je kuna hiyo possibility..Then mafisadi watakamatwa etc etc?

Je ni kwa namna gani chama hiki kinaweza kufanya mabadiliko ili kuweza kuendana na wakti pamoja na kuridhia matakwa ya wananchi?

Je kaburi la CCM linachimbwa?
 
Back
Top Bottom