CCM ifanyike mabadiliko suala la kofia mbili

Mkuu, hawa jamaa wanahangaika sana. Wamejaribu JF wameshindwa na sasa wamehamia kwenye Magazeti ambako wanaamini hakuna atakayewapinga so long wamelinunua hilo gazeti. Hata hivyo hawatafanikiwa

demokrasia ya ccm hairuhusiwi mtu kupingwa!?
 
Nimeisoma makala kwa kina na nimeiona hoja ya msingi, na huu ndio utaratibu unaotumika nchi nyingi duniani zilizoendelea.

Tunapenda Rais wetu atutumikie Watanzania majungu ya ccm awaachie wengine, tunapoongelea mabadiriko ni pamoja na haya, chama cha mapinduzi kinapaswa kufanya mapinduzi kwa vitendo.

Magufuli akishapewa huo uenyekiti na yeye atarithishwa mipasho tu yatakuwa yaleyale.
Kama unavyosema, huu utaratibu wa kofia mbili unafaa kwa nchi zilizoendelea. Kumbuka Tanzania ni moja ya nchi ya dunia ya tatu.

Tanzania haijafikia kwenye kiwango cha siasa za nchi zilizoendelea na kulazimisha itakuwa kama kumlazimisha mtoto kuanza kukimbia wakati hata kukaa hajaweza.

Mazingira ya Siasa za Tanzania hayaruhusu kofia ya Rais wa Nchi na Mwenyekiti wa Chama Taifa kushikwa na watu wawili tofauti. Hii inasababishwa na Katiba ya Tanzania.

Katiba ya Tanzania imejenga mazingira ambayo kama kofia mbili zitatenganishwa, basi kuna hatari ya kuwepo mvurugano mkubwa ndani ya chama ambao pia utaathiri moja kwa moja utendaji wa serikali. Kuathirika kwa serikali ni kuathirika kwa wananchi wote hata wale ambao hawana kadi au mapenzi ya vyama.

Mbaya zaidi, hii CCM ya sasa inahitaji kusafishwa kabla hata ya kuanza kufikiria kutenganisha kofia mbili.
 
Kama unavyosema, huu utaratibu wa kofia mbili unafaa kwa nchi zilizoendelea. Kumbuka Tanzania ni moja ya nchi ya dunia ya tatu.

Tanzania haijafikia kwenye kiwango cha siasa za nchi zilizoendelea na kulazimisha itakuwa kama kumlazimisha mtoto kuanza kukimbia wakati hata kukaa hajaweza.

Mazingira ya Siasa za Tanzania hayaruhusu kofia ya Rais wa Nchi na Mwenyekiti wa Chama Taifa kushikwa na watu wawili tofauti. Hii inasababishwa na Katiba ya Tanzania.

Katiba ya Tanzania imejenga mazingira ambayo kama kofia mbili zitatenganishwa, basi kuna hatari ya kuwepo mvurugano ndani ya chama ambao pia utaathiri moja kwa moja utendaji wa serikali.

Mbaya zaidi, hii CCM ya sasa inahitaji kusafishwa kabla hata ya kuanza kufikiria kutenganisha kofia mbili.

Nafikiri uoga mkuu upo hapo kwenye kusafishwa maana wengi wamenufaika sana na kuwemo kwenye chama hiki.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom