CCM ifanyike mabadiliko suala la kofia mbili

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
12,884
2,000
Je, ni mwanaccm yupi ameandika maoni haya kuhusu kuondoa kofia mbili kwenye gazeti la Mwananchi?

Leo hii kuna maoni yametolewa na mwandishi maalum wa gazeti la mwananchi kuhusu mkutano wa CCM wa Julai 23 ambao unatarajiwa kumpa uenyekiti wa chama hicho raisi John Magufuli.

Nimechambua kwa kina kila sentensi na kuonisha maoni haya na maoni ya wanasiasa wengi ambao wanatarajiwa kushiriki shughuli hiyo hapo tarehe 23 Julai.

Anatoa sababu kadhaa ambazo ni pamoja na kwamba kofia mbili zitenganishwe, uwajibikaji utaongezeka, huu ndio wakati muafaka.

Pia anaendelea kusema kwamba CCM ibadili ajenda au iendeleze ajenda kwamba mwenyekiti wa sasa ndie aendelee kushikilia kofia hiyo ya uenyekiti.

Ninao wanachama kadhaa waandamizi ambao wanaweza kuwa ndio mhusika mkuu wa maoni haya.

Sasa wanabodi napenda kuwasilisha maoni haya ili usomapo nawe ujaribu kuchambua na utambua haya ni maoni ya mwana- CCM yupi kati ya wle ambao hawapendi raisi John Pombe Magufuli ashike nafasi ya uenyekiti wa CCM.

Mkuu Lizaboni, twende kazi.

==========

CCM ifanyike mabadiliko suala la kofia mbili.

By mwandishi wetu, Mwananchi

Chama cha Mapinduzi (CCM) Jumamosi hii kitafanya Mkutano Mkuu Maalumu mjini Dodoma ukiwa na lengo kuu la kumkabidhi uenyekiti wa chama hicho Rais John Magufuli kutoka kwa mtangulizi wake Jakaya Kikwete.

Huo ndiyo utaratibu wa kawaida wa CCM kubadilisha nafasi ya uenyekiti kwa kila rais mpya anapoingia madarakani baada ya Uchaguzi Mkuu licha ya kuwa mwenyekiti wa chama hicho anakuwa bado hajatimiza muda wake wa kukaa madarakani.

Utaratibu huo unamfanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mbali na kuwa Ikulu kuwa na kofia ya pili ya kuwa mwenyekiti wa chama hicho kinachotawala tangu Tanzania ipate uhuru.

CCM ilizaliwa Februari 5, 1977 baada ya uamuzi wa kuviunganisha vyama vya siasa vya Tanu kilichokuwa kinatawala Tanzania Bara na Afro Shirazi Party (ASP) kilichokuwa kinaongoza Zanzibar.

Uamuzi huo ulifanywa wakati Tanu ikiongozwa na Mwalimu Julius Nyerere na ASP ikiwa chini ya Aboud Jumbe Mwinyi na kuendelea kuitawala Tanzania wakati wa mfumo wa chama kimoja na hadi Uchaguzi Mkuu wa kwanza wa mfumo wa vyama vingi uliofanyika mwaka 1995.

Kofia mbili zitenganishwe

Linaonekana ni jambo la kawaida kwa CCM kuziunganisha kofia mbili za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya mwenyekiti wa chama hicho, lakini kuna haja ya kufikiria upya juu ya suala hilo.

Pamoja na kwamba hali halisi inaonyesha kuwa mkutano mkuu maalumu wa CCM kwa mazingira yaliyozoeleka hautaangalia suala la kuzitenganisha kofia mbili, lakini muda wa kufikiria hivyo umewadia.

Kuna umuhimu kwa ustawi wa Taifa na ustawi wa CCM na mwelekeo wa kuwa na utawala bora zaidi kofia hizo mbili zikatenganishwa ili Rais akabaki na shughuli zake za kusimamia Ikulu na mtu mwingine akawa na majukumu ya kusimamia CCM.

Pamoja na kwamba jambo hilo halijazoeleka, lakini ukweli ni kuwa linaweza kuwa na manufaa kwa vile katika historia ya Tanzania na jinsi wanasiasa walivyojengwa katika nchi hii hakuna siku ambayo itatokea watu hawa wawili wakatofautiana.

Faida kubwa ya kutenganisha kofia mbili itampa nafasi mwenyekiti wa CCM kuwa msimamizi na mshauri wa karibu wa Rais na kumwelekeza pale atakuwa hakwenda katika njia iliyonyooka.

Hata hivyo, ni wazi kwamba kofia mbili zikivaliwa na mtu mmoja kama ambavyo ilivyokuwa imezoeleka kunafanya awe hawajibiki kwa yeyote yule na kama atataka kuzitumia vibaya nafasi hizo anao uwezo wa kuivuruga nchi.

Itaongeza utendaji wa Rais

Iwapo Rais hatakuwa mwenyekiti wa chama itamfanya asijikite zaidi katika siasa hali ambayo itamwongezea nguvu na kutumia muda wake wote katika shughuli za Serikali na kwa hiyo kuongeza ufanisi.

Rais akiwa na kazi mbili kwa hali yoyote ile atalazimika kupanda farasi wawili na kuna sehemu anaweza asitende haki inavyotakiwa.

Kwa hiyo, kuna haja kwa Rais Magufuli kutokana na ari ya utendaji wake aliyoionyesha tangu alipoapishwa kuwa Rais wa Tanzania Novemba 5, 2015 aachiwe aendelee kutumbua majipu Ikulu huku wakiwa na mipango ya kujenga uchumi wa Tanzania.

Hii ni fikra mpya ambayo inafaa wana CCM watakaokutana katika mkutano huo waipe nafasi ya kuijadili kabla ya kutekeleza wajibu wa kumkabidhi kiti cha uenyekiti wa CCM Rais Magufuli.

Inawezekana ikaonekana ni suala gumu, lakini siku zote mabadiliko siyo kitu chepesi na kina hitaji ujasiri kukifanya, ukiamua matokeo yake yanaweza yakawa mazuri.

Huu ndiyo muda mwafaka

Hakuna muda wowote mwingine mwafaka kwa CCM kuweza kuzitenganisha kofia mbili za urais na uenyekiti wa chama hicho kama muda huu Ikulu yupo Rais Magufuli.

Rais Magufuli amelipambanua kuwa ana dhamira ya kutekeleza mambo makubwa kwa ajili ya kuwaletea maendeleo Watanzania kwa hiyo lingekuwa jambo la busara kupewa muda zaidi wa kutekeleza azma hiyo.

Ili kumpa nafasi hiyo ni kutompa nafasi ya uenyekiti wa CCM ambayo nayo ina shughuli nyingi za kukisimamia chama hicho ambacho katika hali ya sasa kinahitaji usimamizi wa karibu ili kurudisha hadhi yake.

Pamoja na kwamba CCM imerudi madarakani kwa upande wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ule wa Zanzibar, lakini chama hicho kinakabiliwa na ushindani mkubwa kutoka kwa vyama vya upinzani ambao unawalazimisha kufanya mageuzi katika chama chao.

Kwa upande wa Zanzibar hivi sasa kuna mpasuko wa kisiasa baada ya Chama cha Wananchi (CUF) kudai kwamba ilishinda Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar uliofanyika Oktoba 25, 2015, lakini iliporwa madaraka.

Uchaguzi huo ulifutwa na mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha Oktoba 28 siku ambayo alipaswa kutangaza matokeo ya urais na kulazimika kufanyika kwa uchaguzi wa marudio uliofanyika Machi 20 mwaka huu na kususiwa na CUF na kuipa ushindi CCM.

Katika mazingira hayo CCM ingepata mtu tofauti wa kuisimamia ili ikasahihisha mambo yake badala ya Rais ambaye ana mambo mengi ya kusimamia Serikali na kutekeleza azma yake ya kujenga Tanzania ya viwanda.

Mkutano wa CCM ubadili ajenda

Ili kutoa uamuzi wa kuzitenganisha kofia mbili za urais na uenyekiti wa CCM, mkutano mkuu maalumu unalazimika kubadili ajenda ya kumkabidhi uenyekiti wa chama hicho Rais Magufuli.

Wajumbe wa mkutano huo wanapaswa kujadili muelekeo mpya wa kuzitenganisha kofia hizo na kumruhusu mwenyekiti wa sasa, Kikwete aendelee kushika wadhifa huo hadi muda wake wa miaka mitano utakapomalizika.

Baada ya hapo wajumbe wa mkutano ndiyo wanaweza kuamua kama Kikwete aendelee kuwa mwenyekiti wa chama hicho au achaguliwe mwenyekiti mpya ambaye kwa namna yoyote ile hatakuwa Rais Magufuli.

Kwa sababu ya mazoea jambo hili linaweza kuonekana kuwa gumu, lakini kama litafanywa lina nafasi ya kuleta changamoto mpya zenye mwelekeo wa kuleta mafanikio katika Tanzania.

Ni dhahiri kwamba wanachama wa CCM watakaokutana mkutanoni wanatakiwa kujikita katika kufikiria kuzitenganisha kofia mbili na kuanzisha utaratibu mpya kwa kuiongoza Tanzania.

Mwandishi ni mchambuzi wa masuala ya siasa na jamii, anapatikana kwa barua pepe: maoni@mwananchi.co.tz
 
NAKWEDE

JF-Expert Member
Aug 1, 2007
27,961
2,000
mh! kazi ipo hiyo tarehe 23 Julai ifike na kupita ili yaishe haya duuuuu
 
YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
29,555
2,000
Gazeti la mwananchi naona toleo la leo naona walinunuliwa na wale wasiotaka Magufuli awe mwenyekiti wa CCM!!
Limejaa makala nyingi tu mpaka za akina Malisa za kushambulia Kofia mbili.Mtandao wa Mafisadi unahaha na kampeni koko butu

Tarehe 23 ni Magufuli sio swala la kuwa mafisadi walio UKAWA na CCM wanataka au hawataki.Ni vizuri HAO MAFISADI waanze kujiandaa kisaikolojia.
 
Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,903

Mkuu, hawa jamaa wanahangaika sana. Wamejaribu JF wameshindwa na sasa wamehamia kwenye Magazeti ambako wanaamini hakuna atakayewapinga so long wamelinunua hilo gazeti. Hata hivyo hawatafanikiwa
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
121,512
2,000
Acha kukurupuka na kuandika pumba. Kama huna la maana la kuandika kaa kimya na kuwaachia wengine wajadili kwa kina.

Ni wale wale tunaopambana nao humu kila siku. Wanafahamika na wamedhibitiwa
 
Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
12,884
2,000
Hiki kitu kinaudhi sana Mkuu Richard.

Unapoweka mada yenye kichwa chake cha habari kunakuwa na maana yake.

Sasa sipingi kubadilisha makosa madogomadogo lakini kubadilisha heading ya mada kama hii kumebadili maana nzima na lengo langu la kuiwasilisha hapa.
 
  • Thanks
Reactions: BAK

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,025
2,000
They are fighting to last drop of blood!

Hawa wanaotaka Rais Magufuli asiwe Mwenyekiti wa CCM Taifa ni kama wamepagawa.

Mbaya zaidi, hawafahamu kama Kikwete ni mtu asiyependa marumbano.

Wanatakiwa waanze tu kuzoea badala ya kupoteza muda kwa suala ambalo haliwezi kutokea.
 
Kamanda D

Senior Member
Jul 11, 2015
134
225
Hahahaha naona wazee wa kuingilia madirishani wakati mlango upo kama alivyosema Mrisho Mpoto kwenye wimbo wake wa sizonje wana kazi kubwa kwelikweli ya kujaribu kumdhibiti JPM. Sasa naanza kukubaliana na kile alichosema Askofu Gwajima natusubiri tuone mwisho wa hizi sarakasi.
 
simba45 mkali

JF-Expert Member
Oct 15, 2012
1,981
2,000
Gazeti la mwananchi naona toleo la leo naona walinunuliwa na wale wasiotaka Magufuli awe mwenyekiti wa CCM!!
Limejaa makala nyingi tu mpaka za akina Malisa za kushambulia Kofia mbili.Mtandao wa Mafisadi unahaha na kampeni koko butu

Tarehe 23 ni Magufuli sio swala la kuwa mafisadi walio UKAWA na CCM wanataka au hawataki.Ni vizuri HAO MAFISADI waanze kujiandaa kisaikolojia.
Mambo ya ukawa yanahusiana vip na mambo ya ccm. Yamewashinda sasa mmeanza fyokofyoko zenu kwa ukawa.
 
simba45 mkali

JF-Expert Member
Oct 15, 2012
1,981
2,000
Mkuu, hawa jamaa wanahangaika sana. Wamejaribu JF wameshindwa na sasa wamehamia kwenye Magazeti ambako wanaamini hakuna atakayewapinga so long wamelinunua hilo gazeti. Hata hivyo hawatafanikiwa
Mkuu naona upo mzigoni full time. Hapana masihara mpaka kieleweke.
 
technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
10,900
2,000
Gazeti la mwananchi naona toleo la leo naona walinunuliwa na wale wasiotaka Magufuli awe mwenyekiti wa CCM!!
Limejaa makala nyingi tu mpaka za akina Malisa za kushambulia Kofia mbili.Mtandao wa Mafisadi unahaha na kampeni koko butu

Tarehe 23 ni Magufuli sio swala la kuwa mafisadi walio UKAWA na CCM wanataka au hawataki.Ni vizuri HAO MAFISADI waanze kujiandaa kisaikolojia.
Mkuu asante
 
technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
10,900
2,000
They are fighting to last drop of blood!

Hawa wanaotaka Rais Magufuli asiwe Mwenyekiti wa CCM Taifa ni kama wamepagawa.

Mbaya zaidi, hawafahamu kama Kikwete ni mtu asiyependa marumbano.

Wanatakiwa waanze tu kuzoea badala ya kupoteza muda kwa suala ambalo haliwezi kutokea.
Exactly
 
simba45 mkali

JF-Expert Member
Oct 15, 2012
1,981
2,000
Nadhani ni vyema sana na ndio muda muafaka sana kama ccm watatenganisha hizi kofia mbili ili kuongeza uwajibikaji kwa nia njema. Kama wakishindwa kufika muafaka ni bora wamkabidhi magufuli uwenyekiti nae afanye yake.
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
121,512
2,000
Mkuu hiyo ni moja ya sababu zinazowakera wengi humu. Hata sijui ni criteria zipi wanazotumia kuamua kubadili heading.

Unapoweka mada yenye kichwa chake cha habari kunakuwa na maana yake.

Sasa sipingi kubadilisha makosa madogomadogo lakini kubadilisha heading ya mada kama hii kumebadili maana nzima na lengo langu la kuiwasilisha hapa.
 
Matola

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
41,497
2,000
They are fighting to last drop of blood!

Hawa wanaotaka Rais Magufuli asiwe Mwenyekiti wa CCM Taifa ni kama wamepagawa.

Mbaya zaidi, hawafahamu kama Kikwete ni mtu asiyependa marumbano.

Wanatakiwa waanze tu kuzoea badala ya kupoteza muda kwa suala ambalo haliwezi kutokea.
Nimeisoma makala kwa kina na nimeiona hoja ya msingi, na huu ndio utaratibu unaotumika nchi nyingi duniani zilizoendelea.

Tunapenda Rais wetu atutumikie Watanzania majungu ya ccm awaachie wengine, tunapoongelea mabadiriko ni pamoja na haya, chama cha mapinduzi kinapaswa kufanya mapinduzi kwa vitendo.

Magufuli akishapewa huo uenyekiti na yeye atarithishwa mipasho tu yatakuwa yaleyale.
 
Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
12,884
2,000
Nimeisoma makala kwa kina na nimeiona hoja ya msingi, na huu ndio utaratibu unaotumika nchi nyingi duniani zilizoendelea.

Tunapenda Rais wetu atutumikie Watanzania majungu ya ccm awaachie wengine, tunapoongelea mabadiriko ni pamoja na haya, chama cha mapinduzi kinapaswa kufanya mapinduzi kwa vitendo.

Magufuli akishapewa huo uenyekiti na yeye atarithishwa mipasho tu yatakuwa yaleyale.

Je ni kwanini hoja hiyo ya mabadiliko imeibuka wakati huu na sio nyakati zingine zilizopita?

Mbona kama kuna uoga hivi ambao hauna msingi?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom