CCM huwabadili watakatifu kuwa waovu?

Kitila Mkumbo

JF-Expert Member
Feb 25, 2006
3,354
1,943
Nimekuwa nikiisoma barua ya Butiku, now and then, natafakari mshangao wake kumuona Mkapa alivyobadili baada ya kuukwaa urais. Mshangao wake unaibua maswali mengi ikiwa pamoja na: i) kwamba ina maana huyu bwana pamoja na kuwa karibu na Mkapa ni kweli kwamba hakumjua Mkapa kwa kiasi hicho? au ii) tuseme ni kweli kwamba Mkapa alibadilika baada ya kuingia madarakani kama Rais? iii) na kama hivi ndivyo, kwamba alibadilika, ni kitu gani kilimbadili Mkapa kiasi hicho? iv) Je, kuna wengi tuliokuwa tunawona kuwa ni wazuri lakini ghafla wakabadili baada ya kupata madaraka ya CCM? v) Kingunge na Warioba wanaweza kuwa ni mifano mingine jinisi CCM ilivyowabadili kutoka kuttetea utakatifu hadi kupenda uovu?

Baadhi ya maswali haya yanajibiwa katika makala niliyoandika hivi karibuni na kuchapwa katika gazeti la Tanzania Daima mwanzoni mwa Mwezi huu. Kwa maoni yangu ni kwamba ni vigumu kupambana na madhira katika nchi ile kupitia CCM. Hiki si chombo salala tena cha kusafisha uchafu bali ni agency wa uchafu. Kwa hiyo hatua ya kwanza ya mtu yeyote anayetaka kupambana na matatizo ya nchi yetu ile kwa kupitia siasa ni kuchagua njia ingine mbali na CCM. Butiku naye kwa kuendelea kupiga kelele huku akiendelea kubaki hukohuko anaweza akakuta naye anajichafua. Endelea kusoma na toa maoni yako pia.
________________________________________________________
Jinsi CCM ilivyowabadili watakatifu kuwa waovu

Kitila Mkumbo


NI hivi punde tu nimehitimisha kusoma kitabu kipya kiitwacho “The Lucifer effect: How good people turn evil” kilichoandikiwa na mmoja wa magwiji wa saikolojia ya jamii, Profesa Phillip Zimbardo.
Kwa tafsiri isiyo rasmi tunaweza kutafsiri kitabu hiki kama ‘Athari za Lucifer: Jinsi watu watakatifu wanavyobadilika kuwa waovu’.

Katika kitabu hiki, Profesa Zimbardo kwa kutumia matokeo ya tafiti alizofanya kwa zaidi ya miaka 15, anaeleza jinsi ambavyo mazingira maovu yanavyoweza kumbadilisha mtu aliyekuwa mtakatifu na kuwa mwovu kwa kiwango cha kutisha. Profesa Zimbardo anabainisha mambo matatu kuhusu utakatifu na ushetani.

Kwanza, anabainisha kuwa dunia wakati wote ina watu wa aina mbili - yaani watu walio watakatifu na waovu. Pili, ukuta kati ya utakatifu na uovu unapenyeka. Tatu, inawezekana kwa malaika kuwa shetani, na mashetani kuwa malaika!
Kwa mujibu wa Profesa Zimbardo, dawa ya kupambana na uovu katika jamii, si kupambana na waovu, bali kupambana na mazingira yanayosababisha watu wafanye uovu. Ndiyo kusema kuwa hata kama mtu atakuwa mtakatifu namna gani kuna uwezekano mkubwa wa mtu huyo kuchafuka kama atawekwa katika mazingira machafu.

Profesa Zimbardo anahitimisha kitabu chake kwa kutoa tahadhari kuwa ili kuyashinda mazingira ya uovu katika jamii, kunahitajika wajitokeza watu jasiri (heroes). Hata hivyo Profesa Zimbardo anakiri kuwa katika jamii mara nyingi watu jasiri ni wachache mno na nguvu zao huonekana tu pale ambapo jamii huwaunga mkono katika jitihada zao za kupambana na mfumo unaojenga na kulinda watenda maovu. Bila jamii kuwaunga mkono watu jasiri, juhudi za watu hawa huonekana kama za kujikweza na zisizokuwa na manufaa yoyote katika jamii.

Kwa bahati mbaya au nzuri nimemaliza kusoma kitabu hiki katika kipindi ambacho nchi yetu ipo katika mkanganyiko mkubwa kuhusu usafi na uadilifu wa viongozi wetu tuliowakabidhi mamlaka na madaraka ya kuongoza nchi. Nimehusisha maudhui ya kitabu hiki na tuhuma nzito za ufisadi zilizotolewa na viongozi wa upinzani dhidi ya viongozi kadhaa wa serikali. Nimehusisha pia maudhui ya kitabu hiki na juhudi za baadhi ya watu wanaoheshimika katika jamii yetu za kujaribu kuwasafisha waliotuhumiwa na kuwabeza wale wanaoibua tuhuma za ufisadi.

Nitawatolea mifano watu wawili ambao ni Kingunge Ngombale-Mwiru na Jaji Joseph Sinde Warioba, ambao wote kwa muda mrefu wamejijengea heshima kubwa katika jamii yetu.

Mzee Kingunge alikuwa mtu wa kwanza kujitokeza katika kujaribu kuwasafisha viongozi waliotuhumiwa kuhusika na ubadhirifu wa mabilioni ya pesa kwa kutumia nafasi za uongozi tulizowakabidhi.

Majibu ya Kingunge yalikuwa rahisi kabisa; kwamba tuhuma za wapinzani hazikuwa na ukweli wowote, bali “jitihada ya kutaka serikali iondoke kwenye mstari wa kushughukia maendeleo ya wananchi, ihangaike na tuhuma za hewani.” (Mwananchi, Septemba 19, 2007, uk. 2). Mzee Kingunge alikwenda mbali zaidi kwa kusema: “Nongwa iliyopo ni kuona maendeleo yanakua kwa kasi. Angalia shule tunazijenga kwa kasi na sasa tunageukia kwenye zahanati, sisi kwetu haya ni maendeleo na dunia inaona na kutusifu, lakini kwa wenzetu hawa ni nongwa” (HabariLeo, Septemba 19, 2007, uk.2).

Hili la kwamba maendeleo yanakua kwa kasi na kwamba wapinzani wanaona nongwa linahitaji makala nyingine. Lakini inatosha tu kusema kuwa inawezekana Kingunge na viongozi wenzake wanaishi dunia nyingine.

Kama kweli serikali ya leo inaleta maendeleo makubwa kama anavyodai Kingunge, wananchi wasingewazomea mawaziri katika mikutano ya hadhara na Waziri Mkuu asingeitikiwa na wananchi kwa kusema “ovyo” aliposema pale alipotarajia aitikiwe “oyee” katika ziara zake huko mikoani.

Bahati mbaya kwake Kingunge alitoa kauli zake hizi kabla hata hajasoma kwa kina tuhuma zilizotolewa na wapinzani kama alivyokiri mwenyewe pale aliposema “tunangoja tupate nyaraka zao tutajibu tuhuma zote”. (Mwananchi, Septemba 19, 2007, uk. 2).

Kwa hiyo kimsingi Kingunge aliamua kuzungumzia jambo asilolijua na kusahau usemi maarufu wa Rais mstaafu Mzee Mkapa, ambaye Kingunge alikuwa mshauri wake mkuu, ya kwamba huna haki ya kulizungumzia jambo ambalo hujalifanyia utafiti. Kibaya zaidi, jambo alilokuwa analizungumzia ni kutetea tuhuma zinazohusu uchafu.

Kitu ambacho Kingunge hakukijua ni kuwa kwa kutetea uchafu naye alikuwa anajichafua na kubadili milele nafasi yake katika jamii kutoka kuwa mtu anayeheshimika kwenda kuwa kitu kingine kabisa ambacho bila shaka sasa anakijua!

Pengine aliyeiweka nafasi yake ya kijamii katika utata mkubwa zaidi ni Jaji Joseph Sinde Warioba. Mzee Warioba naye amejikuta akijaribu kuwasafisha waliotuhumiwa kwa kauli za kujichanganya.

Warioba alikaririwa na magazeti ya tarehe Septemba 28, 2007 akitoa kauli zilizolenga bila mafanikio kuwasafisha viongozi wa serikali wanaotuhumiwa kushiriki katika ubadhirifu.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari, Warioba alizungumzia mambo mawili makubwa. Kwanza aliwataka viongozi wa kisiasa (nafikiri aliwalenga zaidi wale wa upinzani) kujadili matatizo ya wananchi na kwamba viongozi wa sasa wamekuwa mstari wa mbele kuzungumzia masuala ambayo hayamsaidii mwananchi kujikwamua na umaskini.

Kwa maneno mengine, anachotwambia Warioba ni kuwa ufisadi na rushwa si matatizo ya wananchi yanayokwamisha juhudi zao za kujikwamua na umaskini.

Hii ni kauli ya ajabu na inatosha tu kusema kuwa ni ya ajabu bila kutoa maelezo yoyote kwa sababu naamini hata yeye Warioba aliporudi nyumbani na kuisoma kauli yake kesho yake atakuwa alijilaumu na hakuamini macho yake kwamba aliitoa yeye!

Ajabu nyingine katika kauli ya Warioba ni pale alipojaribu kuonyesha kuwa tuhuma za ufisadi zilizoibuliwa na wapinzani hazina maana kwa kuwa tu si mpya.

Hii pia ni hoja dhaifu kwa sababu tatizo haliwezi kuacha kuwa tatizo kwa sababu tu eti si jipya. Tatizo linakwisha kwa kutatuliwa na sio kwa kuwa kuukuu. Kauli ya pili ya Warioba iliyopewa uzito katika magazeti ni ile iliyohusu kumhusisha Rais wa nchi na tuhuma za ubadhirifu. Warioba aliwataka viongozi wa upinzani waache kumkejeli Rais anayebeba nembo ya taifa letu. Nami nakubaliana na Warioba kuwa si jambo linalopendeza kuona Rais anakejeliwa.

Hata hivyo, nitumie nafasi hii kumuweka sawa Warioba kuwa suala hapa si kuacha kumkejeli Rais na viongozi wengine wa serikali, bali ni hao viongozi wakiongozwa na Rais anayebeba nembo ya taifa letu kuacha kujiweka katika hali ya kukejeliwa. Labda mzee Warioba atusaidie. Hivi kwa mfano, ni nini hasa maana ya Rais kutangaza hadharani kuwa anawajua wala rushwa na kwamba ana majina ya watu wanaofanya biashara ya mihadarati na kisha kukaa kimya bila kuchukua hatua zozote?

Mzee Warioba atusaidie pia; ni nini hasa tafsiri ya Rais kuwaacha madarakani watu ambao wana tuhuma nzito kwa kiwango cha Gavana wa Benki Kuu na Waziri wa Nishati na Madini? Mimi ninaamini kuwa kukaa kimya bila kuwachukulia hatua watu ambao wewe mwenyewe umesema unawajua kuwa ni wala rushwa ni kuiweka nafasi yako katika hali ya kukejeliwa.

Dawa ya kukwepa kejeli si kuwakemea wale wanaokukejeli, bali ni kuhakikisha kuwa huiweki nafasi yako katika mazingira ya kukejeliwa kwa kuchukua hatua zinazostahili pale watendaji wako wanapofanya mambo yatakayosababisha wewe ukejeliwe.

Mzee Kingunge na Warioba inabidi wajiulize kama kweli haya wanayoyasema wapinzani hayana maana, inakuwaje wao wahamaki na wananchi wahamasike kuwaunga mkono wapinzani kwa kiwango tulichokishuhudia? Pengine swali kubwa ambalo inabidi tulijibu ni kuwa iweje watu waliokuwa wanaheshimika katika jamii kwa kiwango cha Kingunge na Warioba wafikie hatua ya kutokuona kuwa tuhuma za ufisadi si jambo la maslahi kwa wananchi?

Na je, ni kitu gani kimewapata watu hawa hata watoe kauli ambazo zinasababisha mkanganyiko katika jamii badala ya suluhu na amani kama tulivyowazoea?

Je, hawa watu wamebadilika au mazingira yamewabadilisha kutoka umalaika kwenda u-Lucifer?

Kwa kutumia mantiki iliyomo katika maudhui ya kitabu cha Profesa Zimbardo, ni wazi kuwa hawa wenzetu ni waathirika wa mazingira waliomo ambayo ni CCM. Chama hiki (CCM) kimechafuka kwa kiwango ambacho kila apitaye humo lazima achafuke.

Haishangazi kuona kuwa watu ambao kabla ya kuingia CCM walikuwa wanaonekana kuwa watu wema wanaoweza kuisaidia jamii katika kujikwamua na matatizo yake ukiwamo umaskini, lakini walipoamua kufanya hivyo kupitia CCM wakajikuta ama wanachafuka kama wenzao waliowakuta humo au wanashindwa kufurukuta.

Nani angejua kuwa ingefika wakati Kingunge na Warioba wangetoa kauli ambazo hata mtoto wa shule ya msingi anazishambulia na kuzizomea?

Kinachowaponza ndugu zetu hawa ni mazingira waliyomo; maadamu wamechagua kubaki katika mazingira machafu hawatakwepa kuchafuka! Vilevile tumewashuhudia watu waliokuwa wanaheshimika kwa usafi kutokana na kuchukia rushwa na ufisadi, lakini walipopata uongozi kupitia CCM wakabadilika ghafla na kuanza kutamani utajiri wa haraka na kuupata utajiri huo kupitia ufisadi na rushwa hiyohiyo waliyokuwa wanaichukia.

Ndio kusema basi tatizo hapa si hao watu wanaofanya ufisadi; tatizo ni hayo mazingira yanayowafanya wapende ufisadi yaani CCM. Kwa hiyo juhudi za kweli za kupambana na ufisadi huo si tu kupambana na hao mafisadi, bali lazima ihusishe pia kupambana na mazingira yanayosababisha hao watu wapende vitendo vya ufisadi. Katika mapambano haya tuna habari mbaya na njema.

Habari mbaya ni kwamba mapambano dhidi ya mazingira yanayofanya watu wafanye ufisadi ni magumu na ya hatari. Lazima wapatikane watu wachache jasiri ili waongoze mapambana haya. Habari jema ni kwamba tayari wameshajitokeza watu wenye ujasiri wa kupambana na ufisadi katika jamii yetu. Hata hivyo, juhudi za hawa majasiri haziwezi kufua dafu kama hawataungwa mkono na jamii nzima hasa pale watu wanaokubalika kwa kiwango cha kina Warioba watajitokeza kuwabeza watu hao na kutetea mazingira ya ufisadi.

Kwa hiyo, natoa wito kwa wananchi kuwaunga mkono sana kina Dk. Slaa na wenzake kwa juhudi wanazofanya katika kuibua na kuwaumbua mafisadi. Uungwaji mkono wa majasiri hawa usifanyike tu katika mazungumzo ya vijiweni, majumbani na maofisini. Kuna haja ya kuunga mkono juhudi zao kwa njia ya vitendo kama vile maandamano. Hata hivyo niseme tena kuwa juhudi za kupambana na fisadi moja moja ni mkakati wa muda mfupi ambao hautarajiwi kumaliza kabisa hili tatizo ambalo sasa ni kama kansa katika nchi yetu.

Mkakati wa muda mrefu wa kutokomeza hii kansa ya ufisadi lazima uwe ni kuyamaliza mazingira yanayosababisha watu kuwa mafisadi; mazingira haya ni CCM.

Ndiyo kusema tunapoendelea na mapambano haya kwa sasa tutambue kabisa kuwa dawa ya kweli ya ufisadi na uchafu mwingine katika nchi yetu ipo katika uchaguzi wa 2010.

kitilam@yahoo.com
0754 301908
 
Kitila, you are a critical thinker.. Thank you.

Nakubaliana na philosophy ya "Lucifier effect". It is funny but very educative.
 
kweli kabisa Kitila,

Hata mimi nakubaliana nawewe katika hili. Nitajaribu kufuatilia namimi nipate copy ya hicho kitabu.

Asante
 
kama mtu ana akili timamu then mnasema anabadirishwa hapo kosa linakuwa la nani ? mbona hapa pia kuna watu wanataka kubadirisha watu vile wanavyofikiria ? nao tuwaite waovu ?
 
Kitila,

Nakubaliana nawe kwa namna fulani ila sidhani kama ni CCM peke yake ndio watu wanabadilika. Hata vyama vya upinzani kuna watu wamebadilika na kuwa mafisadi. This is everywhere.
 
Kitila,
siyo watakatifu peke yao wanaogeuka waovu wakijiunga na CCM. kuna wasomi wanaogeuka na kufanya mambo ya hovyo kabisa wakipewa uongozi na CCM.

Nitafurahi kama utalitafiti suala la wasomi kufanya mauzauza wanapojiunga na utawala wa CCM.


Hii theory ikiwa ni ya kweli maanake ni kwamba hata hao wasomi tatizo ni hilohilo mara walipojitumbukiza ndani ya CCM wakaenda na maji, wakapenda uovu, wakautukuza na kuusifu! Mwisho wa siku walionekana watu wa ajabu mbele ya jamii! Mifano ipo tele na kedekede!
 
Kitila,

Nakubaliana nawe kwa namna fulani ila sidhani kama ni CCM peke yake ndio watu wanabadilika. Hata vyama vya upinzani kuna watu wamebadilika na kuwa mafisadi. This is everywhere.


Well, this could be true, lakini so far hatuna ushahidi wa wale waliofanya ufisadi walipoenda upinzani. By the way, ninapoongelea upinzani simaanishi vyama vyote vya upinzani vilivyopata usajili wa kudumu. Kuna vyama vya upinzani ambavyo mandate yake inaishia kisheria lakini havina legitimacy! Naongelea sanasana vyama vinne vya CUF, CHADEMA, TLP na NCCR. Sasa wale wa CCM wametajwa kwa majina na vituko walivyovifanya kuanzia A hadi Z. Kama kuna tuhuma pia kwa wapinzani ziwekwe hadharani kwa ushahidi unaoshikika kama ule uliotumika kwa wale wa CCM. Vinginevyo kila mtu anaweza kumtuhumu mtu kwamba ni mwizi, fisadi na vile, lakini bila ushahidi wa maana zinabaki kuwa kelele katika jitihada za kuonyesha kuwa hata wapinzani ni walewale wakati pengine sio!
 
Sawa Kitila, Makala imetulia sana; Nafaham msimamo wako mzuri wa maendeleo toka ulipokuwa Leader wetu University of Dar es Salaam.

Please keep it up,
 
Hii theory ikiwa ni ya kweli maanake ni kwamba hata hao wasomi tatizo ni hilohilo mara walipojitumbukiza ndani ya CCM wakaenda na maji, wakapenda uovu, wakautukuza na kuusifu! Mwisho wa siku walionekana watu wa ajabu mbele ya jamii! Mifano ipo tele na kedekede!

Kweli kabisa,

Ndio maana wasomi wengi mlimani wanataka kwenda kwenye siasa.
Huko vyuoni sijui nani atafundisha sasa.

Asante Kitila!
Good job
 
Kitila,

Nakubaliana nawe kwa namna fulani ila sidhani kama ni CCM peke yake ndio watu wanabadilika. Hata vyama vya upinzani kuna watu wamebadilika na kuwa mafisadi. This is everywhere.

na hapa nadhani tutakuwa tunaloop around kama watu wanadhani mafisadi unafanywa na viongozi wanaotoka ccm, huku wakiwaacha wengine bila ya kuwatilia shaka, ishakuwa akili ya watu kusema kwamba ukitoka ccm basi wewe ni muovu, mjinga, ok that might be true, lakini je ni ccm tu peke yake ?

sawa nyie endeleeni kuangalia viongozi wanaotoka ccm peke LAKINI kama kweli mnataka kuleta maendeleo ndani ya nchi bila ya kujali chama, then nashauri hao watu wabay waangaliwe sehemu zote, ccm/upinzani, kwenye dini, maofisini, sehemu za kazi n.k regardless of their political differences !
 
sawa nyie endeleeni kuangalia viongozi wanaotoka ccm peke LAKINI kama kweli mnataka kuleta maendeleo ndani ya nchi bila ya kujali chama, then nashauri hao watu wabay waangaliwe sehemu zote, ccm/upinzani, kwenye dini, maofisini, sehemu za kazi n.k regardless of their political differences !

Nadhani wewe ndio unataka kulazimisha hapa cha kufanya. Watu wanaweza kufanya au kusema kile kinachofuata uwezo wao wa kufikiri.

Wao wakiamua kuwapondea ssm wana haki ya kufanya hivyo kama wewe ulivyo na haki ya kutetea mafisadi wa ssm. unalia kuwa kuna watu wanakulazimisha cha kufanya hapa kumbe wewe ndio unataka watu wafanye unachotaka
 
tusipige kelele, lete sehemu inayoonyesha nimemlazimisha mtu ninachotaka wafanye ninachotaka zaidi ya mie kutaka wao waelewe what i stand for involving ccm !
 
tusipige kelele, lete sehemu inayoonyesha nimemlazimisha mtu ninachotaka wafanye ninachotaka zaidi ya mie kutaka wao waelewe what i stand for involving ccm !

Je, wewe unaweza kuleta sehemu inayoonyesha kuwa watu wamekulazimisha hapa ufuate wanachotaka wewe kama ambavyo umekuwa unalalamika hapa na kupondea JF kila siku?
 
The Logic is so simple. Human beings are selfish.
It all goes down to wanting more, I don't believe and I have never doubted that we have people in the system that are good in all senses of the word. But, the human nature part of selfishness is what drives people in doing what they do. Ni ule usemi wa kila mtu anakula ofisini kwake. You just think for a minute, wewe hapo ulipo, pamoja na kuwa huna nafasi ya uongozi or vice versa, umesha-cheat vitu vingapi to your own advantage?? Mfano walio US, how many people have cheated on tax returns, hii yote ni ili upate pesa zaidi, pesa unayojua kabisa hukui-earn. Si mnafanya hivi kwa sababu ndio uwezo wa kuvunja miiko umefikia? Hapa kuna question ya wizi na ethics! Sasa niambie, leo wewe na wengine labda tuko humu humu ndani ya JF pointing fingers to leaders, ukipata nafasi sehemu yenye ulaji, uta-abuse your office to what extent? CCM ni mfano tu, lakini kama wengine walivyosema hapo juu, this is just not about being a politician. Nyerere and the like wako wachache sana hapa duniani, let alone in JamboForums. Wengine kesho tutawachagua muwe reps wetu in the system, but utakatifu, will all go down the drain. Its human nature!!!

Having said that, I don't mean to support the practice, or making excuses for being human; naahhh, I'm just trying to be realist!
 
Je, wewe unaweza kuleta sehemu inayoonyesha kuwa watu wamekulazimisha hapa ufuate wanachotaka wewe kama ambavyo umekuwa unalalamika hapa na kupondea JF kila siku?

mbona unageuza muelekeo wako ? soma posts ambazo umeona nimeshikilia kidete ndio utajua nini ninachozungumza, where is your credibility now ?

UMEJIUA MWENYEWE !
 
The Logic is so simple. Human beings are selfish.
It all goes down to wanting more, I don’t believe and I have never doubted that we have people in the system that are good in all senses of the word. But, the human nature part of selfishness is what drives people in doing what they do. Ni ule usemi wa kila mtu anakula ofisini kwake. You just think for a minute, wewe hapo ulipo, pamoja na kuwa huna nafasi ya uongozi or vice versa, umesha-cheat vitu vingapi to your own advantage?? Mfano walio US, how many people have cheated on tax returns, hii yote ni ili upate pesa zaidi, pesa unayojua kabisa hukui-earn. Si mnafanya hivi kwa sababu ndio uwezo wa kuvunja miiko umefikia? Hapa kuna question ya wizi na ethics! Sasa niambie, leo wewe na wengine labda tuko humu humu ndani ya JF pointing fingers to leaders, ukipata nafasi sehemu yenye ulaji, uta-abuse your office to what extent? CCM ni mfano tu, lakini kama wengine walivyosema hapo juu, this is just not about being a politician. Nyerere and the like wako wachache sana hapa duniani, let alone in JamboForums. Wengine kesho tutawachagua muwe reps wetu in the system, but utakatifu, will all go down the drain. Its human nature!!!

Having said that, I don't mean to support the practice, or making excuses for being human; naahhh, I’m just trying to be realist!

kidogo napumua ! nadhani umeelezea vizuri sana and keep it up !

Mfano nakiuliza, ikitokea kwamba JF tumchague rep atuwakilishe sehemu na apewe share awaletee wanaJF hapo ndipo utajua kama watu maneno yao/maandishi yao yanaendana na vitendo vyao !
Its not about walking the walk, but also talking the talk !
Humu kuna mifano mingi ya yule boss ya ENRON ( uliza alikuwa anatembea na nini ) halafu yeye kumbe ndio mkoseaji namba moja....so, kuongea kwa mtu maneno makini haimaanishi maneno yake yanaendana na vitendo vyake, wengi tunaweza kuongea na inafahamika hiyo !
 
mbona unageuza muelekeo wako ? soma posts ambazo umeona nimeshikilia kidete ndio utajua nini ninachozungumza, where is your credibility now ?

UMEJIUA MWENYEWE !

Teh teh the teh,

swali limekushinda kujibu hilo?
Unangangana na kulialia kuwa watu wanakulazimisha ufuate maneno yao wakati wewe unafanya the same things!

Kinachoboa zaidi ni unapoanza kupondea JF ambayo wewe uko hapa every now and then. Watu kwa kukosa misimamo? no wonder mnauza nchi wa wazungu everyday na mikataba yenu mibovu. Hamna misimamo kabisaaaaa
 
CCM ndo walioshika dola na ndio waliopewa dhamana kubwa zaidi ya mustakbali wa nchi yetu, Kwa hiyo ni rahisi zaidi kwa wao kufanya ufisadi wa kutafuna pesa za wananchi kuliko jinsi wapinzani wawezavyo kufanya, kwa sababu wao ndo wako jikoni.

Kwa hiyo hoja ya kudai tusiwakabe mashati mafisadi wa CCM eti kwa sababu na kwenye upinzani Mafisadi wapo, hilo mimi ninalikataa.

Besides ziko wapi shutuma zenye ushahidi za kuonyesha kwamba Wapinzani ni mafisadi?. kwa upande wa serikali ya CCM shutuma zenye ushahidi ziko tele, kuna richmondi, kuna iptl, kuna bot, kwa ishu kama richmondi ukiachilia mbali ripoti ya dokta slaa (ambayo serikali haijaipinga kwa kutoa data) zipo taarifa za uchunguzi zilizoonyesha pale kuna tatizo.. sasa swali linakuja je ni shutuma zipi zenye chembe ya uchunguzi zinazoonyesha wapinzani ni mafisadi?
 
sifikirii kuwa hili ni suala la ccm kugeuza watu waovu, labda tunawaona ccm kwa vile wao pekeyao ndio waliowahi kushika madaraka makubwa.

nahisi ungelisema madaraka yasiyokuwa upeo wa kuyatumia, amdaraka ambayo unaweza kufanya chochote, wakati wowote, bila ya kuogopa ktachofuatia , madaraka yanayompa mtu nguvu za kuiona mungu mtu, ndio yanayobadilisha watu kutoka kuwa wasomi, watawa, wachungaji, kugeuka kuwa mafisadi.

naamini kuwa iwapo nguvu za sheria zitaweza kufanya kazi kwa kila kiongozi atakaefanya ufisadi akiwa madarakani, basi ikiwa ccm au chama chengine cha upinzani, viongozi watajichunga na watabakia na hulka zao njema
 
Back
Top Bottom