CCM huwabadili watakatifu kuwa waovu?

Hahahhahaha alafu leo umeenda kujiunga na HAO WAOVU?? mbona sisikii ukiwapigia kelele hao waovu ili watimuliwe?? Ulipiga kelele sana ufisadi mbona sisikii ukitaka waliohusika na kashfa ya makinikia na Tanzanite waburuzwe mahakama ya mafisadi kwa ufisadi waliofanya?? Hivi una huo ujasiri tena mkuu?? Hivi CCM wakisoma bandiko hili wataweza kukuamini tena kweli??

Afrika tuache kutegemea wanasiasa watatuangusha wanaangalia maslahi yao tu sio yetu.... Ssa fikiria professor kama huyu anaikosoa serikali kwa miaka 15 alafu barua moja tu ya UTEUZI imembadili kila kitu leo hii anasimama kuitetea CCM aliyoita ya waovu?? Kazi kwelikweli
 
Well, this could be true, lakini so far hatuna ushahidi wa wale waliofanya ufisadi walipoenda upinzani. By the way, ninapoongelea upinzani simaanishi vyama vyote vya upinzani vilivyopata usajili wa kudumu. Kuna vyama vya upinzani ambavyo mandate yake inaishia kisheria lakini havina legitimacy! Naongelea sanasana vyama vinne vya CUF, CHADEMA, TLP na NCCR. Sasa wale wa CCM wametajwa kwa majina na vituko walivyovifanya kuanzia A hadi Z. Kama kuna tuhuma pia kwa wapinzani ziwekwe hadharani kwa ushahidi unaoshikika kama ule uliotumika kwa wale wa CCM. Vinginevyo kila mtu anaweza kumtuhumu mtu kwamba ni mwizi, fisadi na vile, lakini bila ushahidi wa maana zinabaki kuwa kelele katika jitihada za kuonyesha kuwa hata wapinzani ni walewale wakati pengine sio!
Mwenyekiti wa CCM kule mkoani mara si Raia wa Tanzania lakini CCM wanamlinda kwa gharama kubwa
 
Haya nae yamemkuta-sasa anashauri mikopo itolewe kwa wanafunzi wanaodahiliwa vyuo vya serikali na sio kwa wale wa vyuo binafsi. Huyu ndio Kiti.la mpya.

Kwa hiyo hatua ya kwanza ya mtu yeyote anayetaka kupambana na matatizo ya nchi yetu ile kwa kupitia siasa ni kuchagua njia ingine mbali na CCM.
 
Sababu kuu ya kuipenda JF huwa wana archive posts vizuri kwa reference baadaye. Daaah, safi sana hatimaye mbwa karudia matapishi yake. Huyu huyu Mkumbo alikuwa anatushawishi kipindi tuko wanafunzi UDSM kujiunga na Chadema, leo hii ndo kwishnei.
 
Hivi Mkumbo bado yumo JF kweli? Huyu bwana sijawahi.kumwamini na hata elimu yake huwa naiona ni ukanjanja flani hivi; alikuwa mwaka mmoja yuma yangu A _ level Pugu ni mtaani wangu_ namjua kiasi chake. Ni ka opportunist flani hivi ambako hua kana maneno mengiii...kanaongea mpaka mapovu yanatoka lakini porojo ili kafikie lengo flani
Kimsingi si mtu wa kumwamini.

Angalia sasa, makala ndefu tena yenye hisia lakini kumbe anabweka tu; katupiwa mfupa _ kimyaa anaongozana na wezi kupora lindo.
Anyway, songela mayo endelea kula na wahenga walisema hakuna kuongea ukiwa unakula.
 
Sababu kuu ya kuipenda JF huwa wana archive posts vizuri kwa reference baadaye. Daaah, safi sana hatimaye mbwa karudia matapishi yake. Huyu huyu Mkumbo alikuwa anatushawishi kipindi tuko wanafunzi UDSM kujiunga na Chadema, leo hii ndo kwishnei.
Hakuweka akiba ya maneno, Lazima uwe na akiba ya maneno, Aliongea sana nae ameenda kuchafuka
 
Nimecheka sana, nikasikitika sana. Hii tabia ya kufukua makaburi muache.

Hivi boss wangu Kitila anaweza kupitia uzi huu??

Thanks kwamba JF sio Instagram kwamba unaweza futa sredi zako za Zamani. Ona aibu hii kwa boss wangu.
 
Njaaaa Mbaya sana.......
Unafkiiii...........teh teh
Inawezekana sahvi akiulizwa Kuhusu kuandika uzi huu anaweza kusema alikuwa tungi....
Namkumbuka kitila mkumbo aka mzee wa Nissan extrail zamani

OvA
 
Hii theory ikiwa ni ya kweli maanake ni kwamba hata hao wasomi tatizo ni hilohilo mara walipojitumbukiza ndani ya CCM wakaenda na maji, wakapenda uovu, wakautukuza na kuusifu! Mwisho wa siku walionekana watu wa ajabu mbele ya jamii! Mifano ipo tele na kedekede!
Usitukane wakunga na Uzazi ungalipo
 
Aliwahi Fanya field mkwawa high school. Wkt huo tukiwa wanafunzi, kwa kweli brother huyu siyo wa kumuamini. Si mzalendo ni mtafutaji na wajanja walishamjua!
 
Kitila,
siyo watakatifu peke yao wanaogeuka waovu wakijiunga na CCM. kuna wasomi wanaogeuka na kufanya mambo ya hovyo kabisa wakipewa uongozi na CCM.

Nitafurahi kama utalitafiti suala la wasomi kufanya mauzauza wanapojiunga na utawala wa CCM.
Hii inamhusu mtoa mada
 
Nimecheka sana, nikasikitika sana. Hii tabia ya kufukua makaburi muache.

Hivi boss wangu Kitila anaweza kupitia uzi huu??

Thanks kwamba JF sio Instagram kwamba unaweza futa sredi zako za Zamani. Ona aibu hii kwa boss wangu.
Yajayo yanafurahisha, Sasa anakula kuku kwa mrija, Tablemanners huruhusiwi kuongea ukiwa unakula

Hapa atayakana maandiko na kusema account imekuwa hacked chezea tumbo na njaa wewe
 
Back
Top Bottom