Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,192
- 25,493
Kwanza, Kamati Kuu ilikutana Dodoma chini ya Uenyekiti wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete. Kikao kilifanyika chini ya Mwenyekiti huyo huyo na ajenda zote hujadiliwa. Mwisho mwishoni maazimio au maamuzi kufikiwa. Halafu Katibu wa Itikadi na Uenezi akautangazia umma juu ya maamuzi hayo.
Pili, Kamati Kuu hiyo hiyo (inayoongozwa na Rais) ikapendekeza kwa Rais kuwapumzisha baadhi ya Mawaziri katika Serikali yake. Mawaziri hao wamepachikwa jina la 'Mawaziri Mizigo'. Kama yeyote anaangalia kwa mkini hapa, atagundua kuwa kuna mkangantiko. Yaani, hata Mwenyekiti amejipendekezea mwenyewe!?
Kwa kuongezea, ajenda za Kikao cha Kamati Kuu zilishajulikana kabla ya Kikao chenyewe. Mojawapo ilikuwa ni ya Mawaziri husika (nahisi hivyo tu). Si ingetosha Rais kuwasikiliza Washauri wake wa Ikulu-hasa wa mambo ya siasa na kuchukua hatua?
Haya mambo ya kujipigia pasi mimi binafsi huniacha hoi sana. Rais ndiye mwenye mamlaka juu ya Mawaziri. Akitaka kuteua na kutoa anaweza kufanya hivyo sekunde yoyote. Haitaji Kikao cha Kamati Kuu ya CCM kufanya hivyo. Rais pekee ni taasisi.
Au ndiyo kutuainisha kuwa Kamati Kuu inafanya kazi za kuidhibiti Serikali ipasavyo? Siasa bwana....