CCM hivi kweli hamuioni kero sugu ya ubovu wa viwanja?

Kamgomoli

JF-Expert Member
May 3, 2018
1,865
3,815
Watanzania tunapenda football sana asikwambie mtu. Lakini kikwazo namba 1 cha soka letu ni ubovu wa pitch.

Asilimia 90 kama si zaidi ya viwanja vyote vinavyotumika ligi kuu na daraja la kwanza vinamilikiwa na CCM. Lakini viwanja vingi ukiondoa kiwanja cha Samora Iringa havina hadhi kabisa ya kuchezea mpira hata kwa mashindano ya mbuzi.

Sijui kwanini CCM wanaving'ang'ania hivi viwanja kama hawawezi kuvitunza. Yaani viongozi wa mkoa mzima mnashindwa kutunza eneo la ekari moja tu kwa kupanda nyasi na kumwagilia? Ndio mtaweza kweli kumsaidia Mh. Rais kutatua kero kubwa kubwa za wananchi?

Mkuu wa mkoa yupo, Mkuu wa Wilaya yupo, makatibu tawala nk mnafanya nini? Mmerundikana maofisini tu eti na hili mpaka Rais aje tumuinulie mabango?

Katika mechi mbalimbali za ligi kuu viongozi mbalimbali wa chama na serikali huwa wanakuwepo na wanashuhudia wachezaji wetu wanavyohangaika na kuteswa na ubovu huo wa viwanja lakini wanajifanya hawaoni tatizo.

Nashangaa sana baadhi ya wakuu wa mikoa wapo bize na mambo ya ndoa na mahusiano ya watu utadhani ndio kipaumbele tulichowatuma.

Jamani hivi sisi watanzania kipaumbele chetu nini kama taifa? Ligi yetu ni kubwa sana. Inatazamwa na nchi takribani zote za ukanda wa East, South and Central Africa.

Hivi kama taifa tunatumiaje kujitangaza maana mtu akiona ubora na uzuri wa viwanja vyetu anaanza kujenga picha ya uzuri wa nchi hata kama hatuna ubora huo ila tayari tutamjengea picha nzuri.

Kwa ufupi viongozi wengi hawana upeo. Wapo wapo tu bora liende. Kama Mwl. Nyerere aliweza kujenga hivi viwanja kwa gharama kubwa nyie mmeshindwaje kupanda nyasi na kuzimwagilia tu?

Vipi kuhusu kuingia ubia na wadau wafanye uwekezaji nalo limewashinda? Mnawaza siasa siasa siasa tu. Mimi naamini kama chama kikiamua seriously kinaweza kutuondolea aibu hii.

Wapo watu kwenye chama na nje ya chama kama wakishirikishwa vizuri wanaweza kujitolea au kufanya uwekezaji wa pamoja na chama.

Pokeeni ushauri, CCM ndio serikali yenyewe hofu ya nini? Badilikeni!

Ni mimi mkereketwa wa soka la bongo.

Kamgomoli Rock mountain.
 
Mkuu unashangaa ubovu wa pitch vipi kuhusu vyoo? Yaani balaa tupu. Nadhani viongozi wengi wanaohusika na usimamizi wa hivi viwanja hawafahamu kama mpira umekuwa ni biashara na unaweza toa ajira nyingi na kuchangia pato la taifa.

Kwa mtizamo wangu Tanzania ndio nchi ambaye wananchi wake wanapenda sana soka kwa nchi za ukanda wa Afrika mashatiki na kati, na pia wachezaji wengi wa nchi hizi hupenda kuja kucheza Tanzania kwa ajili ya ushindani wa soka uliopo, hivyo basi kama tutakuwa na viwanja vizuri na venye ubora unaotakiwa tunaweza vutia wawekezaji wengi sana kutoka ndani na nje ya nchi na kuitangaza nchi yetu na utalii pia.
 
Ccm watapata wapi hela ya kumiliki viwanja vya mpira Tanzania nzima! Viwanja hivyo walivikwapua kwa nguvu baada tu ya kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi.

Tunatakiwa Watanzania kwa umoja wetu kuvikomboa viwanja vyote na hivyo kuwa chini ya uangalizi na usimamizi wa Halmashauri zetu, Manispaa, Miji na Majiji yote nchini.
 
Back
Top Bottom