CCM hili linawahusu, jamaa anawaulieni chama 100%

Mahweso

JF-Expert Member
Jan 10, 2014
1,098
1,501
Hakuna Chama duniani kinaendeshwa bila kutegemea watu,
Hakuna chama Duniani kinaendeshwa bila kuchangiwa,
Hakuna chama Duniani kinajiendesha bila Wafadhiri, Hivi kweli CCM leo iwe ya masikini gafra hivi?
Yaani kutoka kununulia watu T-shet na kanga hadi kuziuza? kusafirisa watu mikutanoni na kuwagawia Pesa leo kifuatwe bure? hivi alitoa kauli ya kwa kuna CCM mcha usiku Chadema ni nani?

Kazi kwenu CCM , lakini kama mmekubali CCM ife nakaa kimya,

Huwezi kuwafanya watendaji wote wa Serikali ni wezi, Huwezi kuwa ni mtu wa amri tu bila kukaa vikao na wenzio wakupe wanakutana na ugumu gani au vikwazo gani kwenye kazi zao na nini uwasaidie ili wafanye kazi vizuri.

Sehemu kuna njaa, unasema hakuna chakula cha msaada hivi kweli? Unaipenda kweli CCM?
Una uhakika Polepole anaifahamu CCM kweli mpaka aieneze?
Kazi kwenu CcM
 
Kiburi uleta maanguko
 
Watu wengine mna mioyo ya chuma, kwani umewekeza hisa huko mpaka kuhofia ufaji wa chama na hisa zako?
 
Humphrey Pole Pole hakijui Chama Cha Mapinduzi. Chama hiki kilishindwa kutimiza ahadi zake kwa wananchi hata kabla Mwalimu Nyerere hajang'atuka madarakani 1985. Akina Pole Pole na wenzake Lumumba wanapotosha historia kwa kuaminisha umma kwamba CCM ilipotea njia baada ya mwalimu kuondoka, kwamba iliachana na misingi yake baada ya Mwalimu kuondoka. Hii sio kweli. Tutaeleza ukweli ambao ni pamoja na kwamba:

1. Misingi ya CCM ambayo Pole Pole et al wanaambia umma kwamba ni lazima irejewe, msingi hiyo hiyo ndio chanzo cha umaskini wa taifa letu.

2. Misingi hiyo ndio ilipelekea CCM kupoteza dira. Ujamaa ilikuwa ni itikadi ya kuunga unga tu (tutaona kwa kifupi baadae). Material basis ya itikadi hii ilitokana na uwepo wa maskini ambapo karibia 90% ya nchi ilikuwa ni rural on the eve of independence. These conditions provided excellent and perfect material and social basis for various petty bourgeois ideology, Ujamaa in particular ambapo ilikuwa ni rahisi kuwaunganisha 90% ya watanganyika weusi kuwa kitu kimoja. Kwa kifupi, Ujamaa as an ideology was an idealization of the life situation of the peasants as well as rationalization of the poor peasants, who constituted almost 90% of the population at eve of independence. Baadae tutakuja kuona kwa undani jinsi gani TANU (bila hata uwepo wa upinzani) ilivunja matumaini ya wananchi ndani ya miaka kumi tu ya azimio la arusha.

3. Misingi hiyo ambayo Pole Pole ameapa kuisimamia, ikirejewa nyakati hizi itatuangamiza kama taifa kiuchumi, kijamii na kisiasa.

Misingi husika (katika muktadha wa ujamaa) haipo supported by any explicit social theory, ndio maana ilifeli. Itikadi ya Ujamaa ilikuwa ni mkusanyiko tu wa glorious description of the past (very flawed description historical wise). Itikadi ya ujamaa was definitely a very powerful statement of an idealist policy (Mwalimu wa essentially an idealist more than anything), lakini itikadi hii haikuwa na political programme. Ujamaa ulikuwa na maono makubwa ya mbeleni (grandiose vision of the future), lakini it lacked ground theory of society. Ndio maana katika yote, legacy pekee ya Mwalimu itakayobakia pengine milele ni kwamba - he had sincere objectives/alikuwa na madhumuni ya dhati'. Na inaishia hapo kwa sababu mijadala mengine itakuwa clouded na mapungufu ya utawala wake.

Kwahiyo hata wakati wa Mwalimu Nyerere, TANU/CCM haikuishi hata siku moja katika ujamaa na kujitegemea. Mafanikio (kama sio matumaini ya mafanikio) ya TANU yalikuwa ni ya muda mfupi sana - 1967-1977. Baada ya hapo, TANU iliyoimbwa kwamba 'yajenga nchi' ikaanza kuyumbisha na hatimaye kubomoa nchi. Na haya yote yaliyokea wakati wa mfumo wa chama kimoja, hasa kuanzia miaka ya kati ya sabini kuelekea miaka ya themanini. Hadi leo, wasiwasi juu ya 'amani na utulivu' wa nchi unatokana na matatizo ya CCM yenyewe (ndani ya CCM), sio nje ya CCM. Nje ya CCM kuna mbadala wa mfumo huu unaoendelea kuangamiza taifa kiuchumi, kijamii na kisiasa (hasa demokrasia). Ni bahati mbaya sana mapambano dhidi ya mfumo huu mbovu yanageuzwa na akina Pole Pole na wenzake pale Lumumba kuonekana kwamba ni mikakati ya upinzani/ukawa dhidi ya tunu za amani na utulivu. Ni ajabu sana kwa mtu eloquent kama polepole kuwa consumed na ulaghai kama huu.

Wengine tulishaondoka CCM muda mrefu hasa baada ya kuelewa ukweli wote hapo juu. Tumeamua kujitenga na uongo. Kuendelea kubakia CCM ni kuendelea kulea ujinga, jambo ambalo ni mmoja wa maadui watatu wa maendeleo ambao CCM hiyo hiyo ikiwa TANU iliwatambua mara tu baada ya uhuru. The fact kwamba maadui hao wanaendelea kutuzonga miaka karibia sitini baada ya uhuru ni kielezo tosha kwamba linapokuja suala la maendeleo ya wananchi, CCM imeishiwa pumzi. Treating CCM synonymously as the STATE na kuaminisha wananchi wasio na uelewa kwamba the two are inseparable ndio nguzo kuu inayoipa CCM mileage, ndio inayojenga uhalali wa kufanya maovu yake yote na kutumia mabavu kuhalalisha kuziba midomo wapinzani, kuangamiza demokrasia, kunyima vyombo vya habari uhuru nk. Jitiada zote hizo ni kuzuia wananchi wasielewe ukweli ambao nimeugusia kidogo hapo juu.

Binafsi nafurahi sana kwamba hatimaye kijana wa generation yetu/kizazi chetu ambae ni mwelewa zaidi ya aliyemtangulia, amepata nafasi ya kukitumikia chama (CCM) katika nafasi hiyo ya itikadi na uenezi. Tutakabiliana na PolePole kwa hoja, na atatuelewa tu, na pengine atakuja chukua maamuzi magumu kuliko haya ya juzi ya kutamka wazi kwamba mfumo sahihi ni mfumo wa serikali tatu. Na hii sio mara ya kwanza kwa polepole kuunga mkono hoja zangu, kwani alishafanya hivyo wakati wa mjadala wa serikali tatu wakati ule bunge la katiba likiketi - rejea:

.

Matamshi kama haya kwa kawaida huwa ni karibia na usaliti ndani ya chama kama sio uhaini. The fact kwamba anaendelea kubakia katika nafasi yake ya uongozi CCM huku akiwa hana imani na sera kuu ya CCM (mfumo wa serikali mbili) ni kielelezo tosha kwamba something is brewing. Ni muhimu Pole Pole akatambua kwamba mfumo wa serikali mbili ni moja ya nguzo kuu tatu zilizokipa CCM uhalali wa kisiasa nchini. Nguzo nyingine mbili zilikuwa ni Mfumo wa Chama Dola na Itikadi ya Ujamaa. Kufikia hapa, kwa wanaoelewa wataona wazi kwamba nguzo zote hizi tatu zimemomonyoka, na ndio maana Chama hiki kina struggle kujitafutia uhalali nje ya sanduku la kura.

Itaendelea kupitia uzi maalum ambao upo katika hatua za mwisho za maandalizi.

cc Humphrey Polepole, MsemajiUkweli, Kobello, Nguruvi3, Ritz, Mag3, JokaKuu, Jasusi, Lizaboni, MTAZAMO
 
Wakati wa TANU kulikuwa na ahadi moja maarufu sana. "NITASEMA KWELI DAIMA FITINA KWANGU MWIKO" lakini CCM wameibadili hiyo ahadi na kuwa " SITASEMA KWELI DAIMA NA FITINA KWAKO NI JADI"
Na ndio maana wakina Kinana,Polepole, Sendeka na vijana wao mazombie kama Lizaboni. Wakudadavuwa &company wamejikita kutimiza hiyo ahadi mpya ya ccm
 
Hakuna Chama duniani kinaendeshwa bila kutegemea watu,
Hakuna chama Duniani kinaendeshwa bila kuchangiwa,
Hakuna chama Duniani kinajiendesha bila Wafadhiri, Hivi kweli CCM leo iwe ya masikini gafra hivi?
Yaani kutoka kununulia watu T-shet na kanga hadi kuziuza? kusafirisa watu mikutanoni na kuwagawia Pesa leo kifuatwe bure? hivi alitoa kauli ya kwa kuna CCM mcha usiku Chadema ni nani?

Kazi kwenu CCM , lakini kama mmekubali CCM ife nakaa kimya,

Huwezi kuwafanya watendaji wote wa Serikali ni wezi, Huwezi kuwa ni mtu wa amri tu bila kukaa vikao na wenzio wakupe wanakutana na ugumu gani au vikwazo gani kwenye kazi zao na nini uwasaidie ili wafanye kazi vizuri.

Sehemu kuna njaa, unasema hakuna chakula cha msaada hivi kweli? Unaipenda kweli CCM?
Una uhakika Polepole anaifahamu CCM kweli mpaka aieneze?
Kazi kwenu CcM

Nilifikiri kufa kwa CCM ndo furaha yako/yenu, sasa iweje tena unawashauri ili wasife na muendelee kuwa Upinzani? Kuna kitu hakikpo sawa hapa!
 
Kwa dunia ya leo ni ngumu mtu mmoja kuweza kufanya kama atakavyo, ninachokiona kuna hali ya kutafuta legacy kama ya kina Che Guevara, Fidel Castro, Mao nk. Dunia ya sasa ya demokrasia ni kushirikiana na wenzako na kupima upande wa wale wanaokupinga ili kupata mafanikio. Lakini kudhani una mawazo sahihi kisha kuyaficha kwenye kichaka cha nia njema, inakuwa ngumu kufikia maendeleo ya kweli kwani kuna sehemu mawazo yako sio sahihi na kibaya zaidi kundi la wale watakaokuwa wanakuzunguka watakusifia tu na wale wanaukupinga utakuwa hukubaliani na mitazamo yao.
 
kule Kenya chama cha KANU kwa kuwa ndicho kilichokuwa kimesimamia kupatikana kwa uhuru wa taifa hilo na hatimaye kikawa madarakani kwa miaka mingi kilibweteka na kujiona kina misingi imara na hivyo hakiwezi kuanguka.
leo hii KANU kimesahaulika katika siasa za Kenya.
na chanzo cha kufa kwa KANU ni aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho - Daniel Toroitich arap Moi.
CCM waende wakazuru kaburi la KANU.watajifunza jambo.
 
Hakuna Chama duniani kinaendeshwa bila kutegemea watu,
Hakuna chama Duniani kinaendeshwa bila kuchangiwa,
Hakuna chama Duniani kinajiendesha bila Wafadhiri, Hivi kweli CCM leo iwe ya masikini gafra hivi?
Yaani kutoka kununulia watu T-shet na kanga hadi kuziuza? kusafirisa watu mikutanoni na kuwagawia Pesa leo kifuatwe bure? hivi alitoa kauli ya kwa kuna CCM mcha usiku Chadema ni nani?

Kazi kwenu CCM , lakini kama mmekubali CCM ife nakaa kimya,

Huwezi kuwafanya watendaji wote wa Serikali ni wezi, Huwezi kuwa ni mtu wa amri tu bila kukaa vikao na wenzio wakupe wanakutana na ugumu gani au vikwazo gani kwenye kazi zao na nini uwasaidie ili wafanye kazi vizuri.

Sehemu kuna njaa, unasema hakuna chakula cha msaada hivi kweli? Unaipenda kweli CCM?
Una uhakika Polepole anaifahamu CCM kweli mpaka aieneze?
Kazi kwenu CcM
Kwa akili ya Nyumbu

Kutoa elimu bure ni kuuwa chama

Kuzuia machinga na mama ntilie wasinyanyaswe ni kuuwa chama

Kuzuia umeme usipande bei ni kuuwa chama

Kuzuia nauli ya mabasi ya mwendokasi yasipande bei ni kuuwa chama

Kununua ndege ili kuinua utalii ni kuuwa chama
 
Hahahaaaaa soma ulichoandika...unaweza usiamini kama ni wewe. Elimu bureee..kuna vitabu? Kuna walimu wa Maths? Wa sayansi je? Na vipi kuhusu maslahi yao? Au ndo KAZI bure?....Jiulize na hayo mengine.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom