CCM Hii ndo Hii au tutegemee Mabadiliko?

marine 1

Member
Jul 29, 2015
41
125
Habari za muda huu ndugu wanajamvi.
Natumai kila mmoja anaendekea na pilika za kuweza kuuelekeza mkono kinywani.

Kwa wale wa makamu yangu, tutakubaliana kwamba tangu kuanza kwa siasa za vyama vingi, CCM imejipambanua katika weledi, ukomavu, uzoefu na historian katika majukumu yake. Wabobezi na wazoefu wa chama kama wazee na wastaafu wamekuwa wakijitokeza katika nyakati ngumu za kisiasa na kutoa tafsiri na uzoefu wao, ambao mara zote umekuwa ukitoa dira na utatuzi wa nyakati husika. Hayo tumeyashuhudia kwa wazee kama Pius Msekwa, Jaji Warioba , Mzee Butiku n.k.

Wakati huo, tumekuwa na vijana wasomi na werevu ambao wamekuwa wachangamfu na wenye kuleta hamasa na siasa za majadiliano baina yao na vijana wenzao wa upinzani na hivyo kuleta Chachu bungeni na katika hoja za kuchangamsha nchi na maendeleo. Kwa nyakati za mwishoni tumeshuhudia siasa za kina Nape, January, Pole pole n.k.

Hata hivyo hayo yote kwa sasa yametoweka. CCM Hatuoni wazee wa kuwasemea na kukemea. Hatuna vijana wanaoweza kukaa na vijana wenzao wa upinzani kuweka mada mezani na kushindana kwa hoja. Hatuna watu wa kuwalinganisha na kina Zitto, Myika, Eche n.k. Wote wamebaki kumsifu na kupamba mwenyekiti wao.

Njia ilionekana kuanza kupotea kwenye awamu iliyopita kutoka na misimamo ya awamu hiyo. Tulitarajia chama kuwa na intelligence ya kuweza kujipanga vizuri baada ya awamu Ile Kwisha. Badala yake chama kimepoteza Haiba na mvuto.

Tuna mwenyekiti ambaye ni mpole kwa Haiba yake, na mgeni pia kwenye chama. Karibu mkuu, mpole na mgeni. Mwenezi Mpole zaidi. Kwa Haiba hii ya uongozi wa juu, umekifanya chama kuwa kigeni na Kilichopoa sana.

Hivyo kwa kuwa chama kimepoa, hatuna watu wa kushindana na vuguvugu la wapinzani, ambao wengi ni vijana machachari. Hivyo kuacha jukumu la kuwajibu wapinzani kwa polisi na vyombo vya Dola. Wapinzani wamefanywa kuwa maadui wa nchi kwa Uzembe wa CCM. Wapinzani wamesusiwa hoja zote, wamesusiwa mijadala na badala ya kujibiwa kwa hoja wananyanyaswa na kuteswa kama maadui. Wamekuwa adui wa Dola.

Bunge kimepoteza Haiba na mvuto. Kauli za kujipendekeza kutafuta uteuzi zimetawala. Hakuna tena uchambuzi yakinifu wa hoja zinazoletwa. Mijadala imehamia kwenye mitandao ambapo pia Vijana wa CCM wamekimbia na kuwaachia wapinzani.

Tunajiuliza CCM itabaki hivi au tutarajie Mabadiliko.?
Tutaendelea hivi kwa kutegemea Dola kama alivyoshaurinbashiru, au tutatoka kujibu hoja kama alivyotuambia mzee wa msoga. Tutaendelea na kauli za kusifu Mapambio kubembeleza teiluzi au tutaanza kujadili vitu kwa weledi na kujenga nchi?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom