CCM hawawataki Wazanzibari lakini wanautaka Muungano!

Petro E. Mselewa

Verified Member
Dec 27, 2012
9,484
2,000
Sijui ndiyo sanaa za kisiasa au vipi.Kuna wakati hata werevu tunaachwa njia panda. CCM kama chama tawala, kupitia wasemaji wa chama au viongozi watokao humo, wamekuwa wakitoa kauli mbalimbali za 'kisanii' sana. CCM hujenga taswira ya kuwachukia Wazanzibari lakini kuupenda Muungano. Ajabu kabisa!

Kuanzia kwenye Bunge la Katiba, Wajumbe watokanao na CCM wamekuwa wakitoa matusi,kashfa,kejeli na kauli za kibaguzi dhidi ya Wazanzibari. Hali ilipozidi uwezo,UKAWA wakatoka nje ya Bunge lla Katiba. Chanzo kilikuwa hicho cha 'kuwachukia' Wazanzibari. Hata kwenye Bunge la Bajeti mambo kama hayo yamejitokeza.Rejea kauli ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na kauli ya leo ya Mbunge Ali Kessy wa Nkasi.

Ni CCM hao hao wanaoutaka mfumo wa Muungano uliopo ubaki.Wanajenga hoja kuwa ni mfumo huu uliopo tu ndio utaoulinda Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Hapa wanadai kuupenda Muungano. Inawezekana mimi sielewi sanaa ya CCM. Lakini nahisi jambo.Kuna kupaka mafuta kwa mgongo wa chupa. Hakuna mambo yaelewekayo katika jambo hili. Labda nieleweshwe na wajuzi wa jambo hili hasa watokao ndani ya CCM.
 
the ultimatum

JF-Expert Member
Dec 16, 2012
401
250
Wabunge wa CCM wanamtihani mmoja mkubwa nao ni kuujadili muungano katika uhalisia wake. Kila wanapojadili muungano katika uhalisia yakinifu wanatonesha machungu ya wazanzibari wenyewe kitu ambacho ni hatari kwa muungano wenyewe na aina ya muungano wanayopendekeza watu wa CCM. Kitu pekee ambacho wanafanya ni kuujadili muungano kiujanja ujanja tu ilimradi watimize matakwa yao, lakini kila wanapojadili muungano katika uhalisia hakika ni uchungu mkubwa sana kwa wazanzibari. Niwatie moyo ndugu zetu wa Zanzibari, nuru inamulika na matunda ya muungano yatakuja chamsingi muungane kikamilifu na watanganyika katika kuitetea rasimu yenye maoni ya watanzania kama ilivyowasilishwa na jaji Warioba.
 
Ni kweli Mkuu. Kuna mambo mengi sana humu ndani
 
Genekai

R I P
Feb 9, 2010
12,535
2,000
Nilishasema, labda nirudie "unahitaji kuwa na matatizo kichwani kuwa mwanaCCM"
 
MwanaDiwani

JF-Expert Member
Mar 22, 2013
5,535
1,195
Nilishasema, labda nirudie "unahitaji kuwa na matatizo kichwani kuwa mwanaCCM"
The trouble with the world is that the stupid are cocksure and the intelligent are full of doubt. - Bertrand Russell

He who knows not and knows not that he knows not is a fool. It's advisable to avoid him.
 
Kilala Makusaro

JF-Expert Member
Oct 31, 2013
688
500
Sijui ndiyo sanaa za kisiasa au vipi.Kuna wakati hata werevu tunaachwa njia panda. CCM kama chama tawala, kupitia wasemaji wa chama au viongozi watokao humo, wamekuwa wakitoa kauli mbalimbali za 'kisanii' sana. CCM hujenga taswira ya kuwachukia Wazanzibari lakini kuupenda Muungano. Ajabu kabisa!

Kuanzia kwenye Bunge la Katiba, Wajumbe watokanao na CCM wamekuwa wakitoa matusi,kashfa,kejeli na kauli za kibaguzi dhidi ya Wazanzibari. Hali ilipozidi uwezo,UKAWA wakatoka nje ya Bunge lla Katiba. Chanzo kilikuwa hicho cha 'kuwachukia' Wazanzibari. Hata kwenye Bunge la Bajeti mambo kama hayo yamejitokeza.Rejea kauli ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na kauli ya leo ya Mbunge Ali Kessy wa Nkasi.

Ni CCM hao hao wanaoutaka mfumo wa Muungano uliopo ubaki.Wanajenga hoja kuwa ni mfumo huu uliopo tu ndio utaoulinda Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Hapa wanadai kuupenda Muungano. Inawezekana mimi sielewi sanaa ya CCM. Lakini nahisi jambo.Kuna kupaka mafuta kwa mgongo wa chupa. Hakuna mambo yaelewekayo katika jambo hili. Labda nieleweshwe na wajuzi wa jambo hili hasa watokao ndani ya CCM.

"Ninawavurugia semi" Askofu Z. Kakobe
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom