CCM hawaoni Makundi haya ndani yao yanakiumiza chama chao? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM hawaoni Makundi haya ndani yao yanakiumiza chama chao?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by M'Jr, Jul 22, 2011.

 1. M'Jr

  M'Jr JF-Expert Member

  #1
  Jul 22, 2011
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 3,539
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Hivi ni mimi ndio naona vibaya au ni kweli kwamba CCM hawaoni kwamba MAKUNDI yao yanakwenda kukiua chama? Ni kweli kwamba they are all blind? Au ndo ile gundi ya kichina iliyowaunganisha imeanza kuyeyuka?
   
 2. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #2
  Jul 22, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  wala si makundi ndugu yangu wakati wao umekwisha ukiona makundi namna hiyo ujue ndo tunaelekea mwisho. ingekuwa kama ni kenya tusingekuwa na CCM tena leo tayari wangekuwa wamesambaratika kwa vile kenyan politicians are stronger than tz
   
 3. M'Jr

  M'Jr JF-Expert Member

  #3
  Jul 22, 2011
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 3,539
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Ni kwamba Kenya politicians wako strong au ni namna watu walivyo huru kuweza kuexpress hisia zao ambapo hapa kwetu haipo hiyo?
   
 4. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #4
  Jul 22, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,144
  Trophy Points: 280
  Makundi ndani ya chama yanaonesha kuwa kuna kuhitilafiana, ingawa wote wanakikubali chama lakini si wote wanakubali vipi kielekee. Utaona kuwa kuhitilafiana kunaleta changamoto ya ushindani na ni nzuri kisiasa, kwani kila atakae ongoza inabidi awe na uono mpana wa kuweza kuongoza makundi yote yanayo hitilafiana. Na hiyo ndio demokrasi. Ikiwa watu hamkubaliani lakini mnashindwa kuonesha tofauti zenu kiuwazi na mnabaki kuwa kama misukule, ujue hapo kuna udikteta. Kitu ambacho Watanzania wengi wamekikuta na wamekirithi ni kuwa anachosema fulani mradi ni kiongozi basi kifatwe na anaeleta hoja ningine basi ni msaliti. Huo ni mtizamo wa kidikteta na haufai hata kidogo na ndio JMK anaumaliza. JMK anahakikisha demokrasia ya kweli inatimizwa ndani ya chama chake kama inavyotimizwa katika uongozi wake kama Rais.
   
 5. M'Jr

  M'Jr JF-Expert Member

  #5
  Jul 22, 2011
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 3,539
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Nakubaliana na wewe kwenye upande wa kuwa hii inaonyesha ukuaji wa demokrasia, lakini napata tatizo sehemu moja makundi ndani ya CCM hayako rasmi na kama utaangalia vizuri si makundi ya kimtazamo bali ya kisasi. Kingine ni kwamba sio makundi ambayo yako rasmi ila ni mpaka utazame kwa mtizamo wa mbali kuweza kuyagundua kama yapo maana ukiangalia kwa juu wote watasema CCM lakini ukisikiliza kwa makini utagundua sauti tatu tofauti ambazo nyingine hazisemi CCM.

  Kingine ni hiyo mitazamo tunayoizungumzia, je ni ya kujenga au kubomoa chama na nchi kwa ujumla? Maana CCM ndio chama tawala na lazima tukubali kwamba kuyumba kwa CCM ni kuyumba kwa taifa zima
   
 6. shegaboy

  shegaboy JF-Expert Member

  #6
  Jul 22, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 214
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MUSIMO JR. Wewe umesema hukiangalia kwa undani sana utagundua tu kuna kitu cha ziada na kuna sauti zaidi ya moja hapo ila wenzetu wanasema tu kujipa moyo ha huyo @ faizafoxy kwa kuwa yeye ni CCM anataka kutuaminisha kuwa ni migongano ya mawazo wakati sio. kwa mfano Mbunge kagasheki amewapiga marufuku kina sita na nape kufika katika jimbo lake kwani ni wanafiki. pia leo tumesoma kuwa Mwenyekiti wa ccm dar anamwambia sita kuwa analake jambo na si bure hii ina shangaza unaweza kusema ni migingano ya mawazo tu kwanini wasiongelee katika vikao ndio tukajua kuwa ni migongano ya mawazo tu
   
 7. M'Jr

  M'Jr JF-Expert Member

  #7
  Jul 22, 2011
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 3,539
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Mi naangalia kwa mtizamo wangu mimi wanavyolitazama CCM wenyewe ndipo tatizo linapokuwa kubwa zaidi maana sasa tatizo linaingia kwenye taifa kwasababu ndio chama tawala. Sasa wanatakiwa watatue tatizo ili wasitupeleke kwenye matatizo tukiwa kama nchi
   
 8. Crucifix

  Crucifix JF-Expert Member

  #8
  Jul 22, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 1,618
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Ya nini kuisakama CCM pekee ilhali makundi yapo katika vyama vyote? CDM kuna genge la Kabwe lisiloshabihiana na Mbowe, CUF kuna kilinge cha Hamad (wa Wawi) kisichompenda Lipumba na hata TLP juzi tu tumeona timbwili la Tao aliyejipanga dhidi ya Mrema. makundi hata katika vyama vikubwa kama Democrat na Republican vya marekani yapo, na tatizo si kuwa na makundi bali kama makundi hayo ya hapa kwetu yanawasilisha kwetu kile yanachokiamini na kiwe ni kweli ndicho wanachoamini. Kundi la Sitta kwa mfano, linataka kutuaminisha kuwa wao ni kondoo kati ya mbwa mwitu na kama tukiwapa dola basi wataua mbwa mwitu wote. Tatizo hapa ni kuliamini kundi hilo kwa sababu hata mchanganyiko wake una kondoo na mbwa mwitu waliokubaliana kuishi pamoja. Siku vikitibuka, kondoo wataliwa tu.
   
 9. M'Jr

  M'Jr JF-Expert Member

  #9
  Jul 22, 2011
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 3,539
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Nimeenda moja kwa moja kwa CCM kwasababu ndicho chama tawala na kile kinachotokea CCM sio tu kwamba kinakuwa na impact kwa chama chenyewe bali ni kwa taifa zima na ndio maana nimeanza kuiongelea CCM. Najua kuna makundi karibu kila chama lakini je athari kwa taifa ni kwa kiwango gani?
   
 10. k

  kiloni JF-Expert Member

  #10
  Jul 22, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 575
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Labda kama si ya kupigania maslahi ya UFISADI. Fulani kala zaidi kuliko sisi. Huu ni wakati wa watu wa pwani kula! wengine wamevimbiwa!- by jumuia ya vijana wa CCM.
  Huko ndiko " kuhitlafiana"
   
 11. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #11
  Jul 22, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,144
  Trophy Points: 280
  Kama chama kitabomoka kwa ajili ya makundi na mitazamo ndani ya chama hiyo inadhihirisha kuwa demokrasia inakuwa na hakuna anaeburuzwa. Wala hilo sio tatizo bali ni jambo jema katika kuitumikia nchi, kwani hapo ndio hutokea wa kweli ambao wako kwenye vyama vya siasa kwa ajili ya maslahi ya nchi na hutokea mabao wako kwenye vyama kwa ajili ya maslahi yao na hutokea pia ambao wako wako tu na wanafata mkumbu bila kujuwa ni nini kimaweka hapo, na pia wapo kwa ajili ya kuganga njaa.

  Kwa hayo yote, kwa muono wangu, sioni kama ni tatizo kuhitilafina katika chama ni ukomavu wa demkrasia na inadhirisha kwamba hakuna kuburuzana.

  Mfani mzuri ni Shibuda na Slaa ambao wote walitemwa kwenye kugombea ubunge CCM lakini walipotoka na kujiunga na magwanda wakachaguliwa na wananchi wao na tunaona hata wao kwa wao hawakubaliani kimisimamo, Hiyo ndio ukomavu wa demokrasia. Si nchi nyingi duniani zenye fursa ya ku "practise" siasa kama kwetu hapa. Na miaka michache tu ntuma demokrasia haikuwa kama ilivyo sasa, iwe ndani au nje ya CCM, Tunepiga hatua kubwa kidemokrasia, tushukuru kwa hilo na tushukuru kuwa na Rais ambae analijali hilo.
   
 12. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #12
  Jul 22, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,144
  Trophy Points: 280
  Inawezekana kabisa ikawa ndio hivyo na ndio maana kuna kuhitilafiana. Kumbuka demokrasia kwetu ni changa sana na viongozi karibu wote (si wa CCM pekee), wametoka kwenye lindi la umasikini na bado wanauchu wa kujinufaisha, lakini kila siku zinvyokwenda ndivyo tunavyozidi kuona madudu yaliyojificha yanajitokeza na hiyo ni kwa sababu tu ya uongozi uliopo. Ingekuwa ni uongozi wa kidikteta na unaokumbatia maovu basi yote tunayaona sasa, ndani na nje ya CCM, tusingeyaona.
   
 13. Crucifix

  Crucifix JF-Expert Member

  #13
  Jul 22, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 1,618
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Si kweli kwamba ni rais ndiye aliyesababisha ukomavu huu. Ni wakati tulionao ndio unaolazimisha hali iwe kama unavyoiona sasa. Rais hana ujanja na ndio maana kuna baadhi ya maamuzi anakubali kuburuzwa kwa sababu akifanya vinginevyo inakula kwake.
   
 14. M'Jr

  M'Jr JF-Expert Member

  #14
  Jul 22, 2011
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 3,539
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Labda nikukumbushe kidogo kuhusu suala la demokrasia kabla sijaongelea kwanini nina hofu na hii demokrasia unayoisema imekua ya sasa. Wakati wa chama kimoja kwa mtizamo wangu ndipo kulikuwa na uhuru wa kweli wa kusema yale ambayo mtu alikuwa anaona kweli yana maslahi kwa watu (Kumbuka zama za G55 ya kina Njelu Kasaka) lakini hii demokrasia ya sasa ya kupitisha kila linalosemwa na mtu hasa bungeni kwasababu tu ni wa "chama chetu" lakini ukitoka nje unasema tofauti mi inanitatiza sana demokrasia ya aina hii!
   
 15. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #15
  Jul 22, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,144
  Trophy Points: 280
  Njelu Ksaka alifanywa nini baada ya kuongea?
   
 16. M'Jr

  M'Jr JF-Expert Member

  #16
  Jul 22, 2011
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 3,539
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Alipewa madaraka na mwenzie Philip Marmo akapewa unaibu waziri wakawa wamefichwa kwa staili hiyo lakini at least walikuwa na uwezo wa kutoa maoni yao sio kama ilivyo sasa
   
Loading...