Elections 2010 CCM hawakuwa namna zaidi ya kutumia dola na kuvunja katiba na sheria za nchi ili kubaki madarakani

DIZZO MTAWALA

JF-Expert Member
Aug 22, 2015
240
767
Yes ni ukweli ambao CCM ilishindwa 2015 ilibaki kwasababu ya dola na kuendelea kuongoza na ndo tatizo lilipoanzia.
2015 ulikuwa mwaka ambao kimatinki kabisa ndo ilikuwa mwisho wa CCM kama chama cha siasa na kubaki tu chama dola nakumbuka namna January Makamba alivyokuwa anazunguka na Kova ili kuwawakamata vijana wa CHADEMA waliokuwa wanakusanya matokeo kwa njia ya kidijitali.

Leo ni miaka mitano tangu CCM kama chama cha siasa kianguke na kibaki chama dola kumekuwa na vilio vingi sio kwa wafanyakazi tu wafanyabiashara mama ntilie wanasiasa wanahabari viongozi wa dini kote huko ni vilio ilianza kama utani pale mikutano ya hadhara ilipozuiwa watu walidhani CHADEMA wamebanwa baada ya kutangaza maandamano ya kuzuia njia hii kiimla yaaani UKUTA baada ya muda watu wakaanza kupotezwa yes Ben Rabiu Saanane, Simoni Kanguye, Azory Gwanda kushambuliwa kwa mnadhimu mkuu wa upinzani bungeni mh Tundu Antipast Lissu pia maiti ziliokotwa nakumbuka majibu ya Mwigulu akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani aliongea kwa kukosa utu kabisa

Hoja kubwa hapa Chama cha Mapinduzi hakipo tena kwa umma miaka mitano ya ukandamizaji kwa watu uimbaji wa maendeleo ya vitu kumgeuza Magufuli kama alfa na omega, ununuaji wa wabunge na madiwani, kutunga sheria kandamizi za kupoka uhuru wa habari, sheria ya mitandao, kujipa mamlaka ya kusikilizwa wao tu ktk media bado haijawasaidia kukubalika kwa jamii sasa wameona kura alizopata Magufuli ni chini ya asilimia 60 wameona anguko
Wameanza kuwasha taa uchaguzi 2020 vitendo vya Spika kulazimisha mbunge aliyejiuzulu kwa hiari yake mwenyewe na akapokelewa na Katibu Mkuu wa CCM hiii ni wazi kutakuwa kuna uvunjaji mkubwa wa katiba na sheria za uchaguzi mkuu 2020 maanake kutakuwa na battle baina ya umma na chama kilichovaa udola ndani yake

Na hiii ndo uhai wa CCM unapoenda kukatika najua praise team na MATAGA mnawaza nguvu ya kauli ya nabii wenu itakwenda kushinda nguvu ya umma huko ni kupiga sarakasi huku umevaa taulo
2020 CCM nakwenda kupumzishwa ikafanye kazi ya kurudisha uhalali wa kisiasa.


Wenu dizzo mtawala raia wa tanganyika na Zanzibar


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Nyie chadema endeleeni kuota ndoto za alianacha

October 2020 ndio mwisho wa kula ruzuku
Tunampogeza raisi maguufuli kwa kuadimimika kwa sukari, pia kwa kufanikisha ziwa Victoria kujaa kupita kiassi. Hongera sana JPM
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom