Elections 2010 CCM - Hatimaye kuku wamerudi nyumbani kutaga! - Mavuno ya Ufisadi

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
Na. M. M. Mwanakijiji

Tumepiga kelele kwa miaka minne na kelele zetu zimebatizwa kuwa ni "chuki binafsi". Tumewapigia mbiu waamke lakini panda zetu zimekuwa ni "kelele za mlango" ambazo hazimzuii mwenye nyumba kulala. Tumesema mfumo wa utawala wa kifisadi nchini ni matokeo ya utawala wa CCM, wakatuambia kuwa 'ufisadi ni wa mtu mmoja mmoja na siyo chama". Wengine wakathubutu kutuambia kabisa kuwa "mafisadi ndani ya CCM ni wanne na wamefikishwa mahakamani". Tumesema ufisadi ni matunda na mazao ya utawala wa CCM na watu wengine wanasema tumefanya hivyo kwa sababu tuna "wivu".

Sasa twayaona matunda ya ufisadi uliokithiri na mfumo wenye kulea ufisadi. Leo tunashuhudia jinsi vyombo vya kusimamia sheria (law enforcement agencies) vikicheza kama "ukuti ukuti" na vitendo vya rushwa huku wakituonesha mazingaombwe ya kuwa wako makini.

Matukio mbalimbali nchi nzima ambapo mchakato wa kutafuta nafasi ya kugombea ndani ya CCM umegubikwa na vitendo vya rushwa na ufisadi. Hii yote si kitu kingine bali ni AIBU YA CCM. Leo hii tunaweza kujua kabisa kile alichouliza Mwalimu kina mantiki kubwa sana. Kwamba hawa wanaotumia fedha nyingi kutaka kuingia madarakani tena kwa njia za giza giza watarudisha vipi fedha zao hizo wakiingia madarakani?

Ukweli ni kuwa siri ambayo inajulikana kwa muda mrefu sasa inawakodolea CCM machoni kama jogoo linalosubiri kuchinjwa, yale ambayo yalikuwa yanafanyika kwa kificho sasa yanakuja hadharani. Matokeo yake PCCB, TISS, POlisi na Mwanasheria Mkuu wote wanajikuta hawana ujanja wa cha kufanya.

Hawawezi kuwatia pingu wote bila kuharibu mchakato wa uchaguzi wa CCM; hawaweti kuwasimamisha wote kugombea kwa sababu kwa kufanya hivyo "nani msafi" atakayeshika madaraka. Kumbe siri ya uchafu wa CCM ni kubwa zaidi.

Hii ni aibu ya CCM na aibu ya wale wote ambao wamejipanga kuishangilia. Haiwezekani kuwa na mtindo mbovu wa kuingia madarakani ambao ungezaa mtindo mzuri wa utawala wakiwa madarakani. Kama hawa watu wanajihusisha na vitendo vya kifisadi kabla ya kuingia madarakani itakuwaje watakaposhika madaraka? Kama leo wanajaribu kuuharibiana na kuumizana kabla hawajakutana na wapinzani Augusti 20 itakuwaje baada ya hapo?

Tunachoshudia basi ni maandalizi ya vitenvo vibaya kabisa vya uchaguzi mkuu tutakavyoviona. Kama ambavyo imedokezwa na mtu mwingine kuwa hadi tarehe moja hakuna mwana CCM ambaye anadaiwa kuwa amejihusisha na vitendo vya rushwa atakayefishwa mahakamani. HAKUNA. Wote ambao wanadaiwa "kukamatwa" watashiriki kana kwamba hawana tuhuma.

Ninaamini, kwenda kuwaengua wagombea hao kwenye vikao kwa kutumia ushahidi wa "TAKUKURU" itakuwa ni kitendo cha kiwoga zaidi. CCM isikimbie utawala wa sheria. Kama TAKUKURU ina kesi dhidi ya watu hao basi wasiruhusiwe kushiriki kura za maoni kabisa na waondolewe kabla ya majina yao wagombea kutangazwa na Kamati Kuu Augusti 14.

Tunachoshuhudia ni kile kile ambacho tunakijua kuwa "kile unachopanda ndicho unachovuna". Kwa muda mrefu CCM imepanda mbegu za ufisadi ndani ya wanachama wake na uongozi wake, na sasa wanavuna matunda yake na nina uhakika watavuna zaidi mavuno haya ya ufisadi kuelekea uchaguzi mkuu. Hatimaye kuku walioenda mitaani kucheza na majogoo ya ufisadi, sasa wamerudi CCM kutamia.

CCM itaelea vifaranga.
 
Mkuu

Umewasahau wale walioteka nyara issue ya ufisadi na sasa hawana cha kufanya bali kulia lia tu. Hawa hatutwasahau
 
Hii ni aibu ya mwaka kwa CCM sijui waificha wapi hata mtoto mdogo sasa anajua kilichobaki wanajivunia ni ubabe na kiburi.

Baada ya TAKUKURU kuja kutangaza kuwa hakuna ushaidi uliopatikana kwa mtu yeyote kujihusisha na rushwa ndani kura za maoni za CCM, itawageukia wapinzani na kuanza kuwasumbua, lakini ninachojua wananchi tayari wameshaona na kujua nani baba wa rushwa tanzania.
 
Nakumbuka mkuu wa kaya alipojinadi mjengoni kwamba serikali yake na chama chake hakitamkamata mtu isipokua wamejiridhia kwamba mtuhumiwa kahusika. Sasa kina Mramba wamekamatwa, maana yake ni kwamba washajiridhisha. Hizo form za kugombea ubunge huko Rombo ujasiri kapata wapi? Kama sii huu ndo ule usanii wa ccm? Aaah bwana unajua huyu anatuhumiwa tu, haijathibitika kwamba ni fisadi. Ama kweli mama kuku anaamini hata mayai yake viza yatatotolewa. Huh! This is dubious.
 
Back
Top Bottom