CCM hatarini: Wafuasi wa Lowassa, Chenge wapanga kuipasua | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM hatarini: Wafuasi wa Lowassa, Chenge wapanga kuipasua

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sulphadoxine, Aug 5, 2011.

 1. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #1
  Aug 5, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  • Waandaa kuleta vurugu kikao kijacho cha NEC
  • Wala njama kuzuia wafadhili wao wasing'olewe

  BAADHI ya wenyeviti wa mikoa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamepanga kuleta vurugu kubwa kwenye kikao cha mwezi ujao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho (NEC) ili kuzuia Waziri Mkuu wa zamani aliyejiuzulu kwa kashfa ya Richmond, Edward Lowassa, pamoja na waziri wa zamani, Andrew Chenge, wasing'olewe kwenye chama.

  Wenyeviti hao wa CCM na wajumbe wengine wa NEC wamepangwa kusimama kwenye kikao hicho cha Septemba na kupingana na uamuzi wa chama hicho wa kuwataka wanasiasa wenye tuhuma za ufisadi kujiuzulu wao wenyewe kwenye nafasi za uongozi kabla ya kusubiri kufukuzwa.

  Kundi hilo la wajumbe wa NEC, wakiwemo wengine kutoka Tanzania bara na Zanzibar, limepangwa ili kujaribu kuleta mapinduzi haramu ndani ya chama katika jitihada za kuzuia wanasiasa hao wasifukuzwe.

  Genge hili la wajumbe wa NEC limeapa kuwa haliko tayari hata kidogo kuona "wafadhili" wao wanatimuliwa kwenye chama.

   
 2. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #2
  Aug 5, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,529
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Washauri wafanye ziara Afrika Kusini wakapate uzoefu jinsi kundi la Zuma lilivyoangusha kundi la Thabo Mbeki. BWT Katiba ya chama inawalinda wakifanya hivyo?
   
 3. nachid

  nachid JF-Expert Member

  #3
  Aug 5, 2011
  Joined: Apr 14, 2011
  Messages: 898
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  <br />
  <br />
  source.......
   
 4. F

  FJM JF-Expert Member

  #4
  Aug 5, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Sioni ni kwa vipi CCM inaweza kuzuia huu mpasuko unaowatizama? Labda kwa nguvu za majini, tena majini yenye nguvu za kipekee na hata hivyo yawezekana yasifue dafu. Mambo ni mazito kweli kweli, Zuma inaweza kabisa kuwa cha mtoto, and I bet my bottom dollar mfumo wa chama kushika hatamu utafutika kabisa by 2012 (latest).
   
 5. Paul Kijoka

  Paul Kijoka JF-Expert Member

  #5
  Aug 5, 2011
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 1,400
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Waende SA walete hela yetu 3TRILLION ya SHIMBO
   
 6. M

  Mjenda Chilo JF-Expert Member

  #6
  Aug 5, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 1,425
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  come soon, come!
   
 7. KIWAVI

  KIWAVI JF-Expert Member

  #7
  Aug 5, 2011
  Joined: Jan 12, 2010
  Messages: 1,747
  Likes Received: 376
  Trophy Points: 180
  hawana cha kupasua wala nini... ni uleule unafiki wa kisiasa

  leo utasikia haya, kesho utasikia yale

  to me, sio tofauti ya magamba, CCM, NEC wala CC

  Nataka dawa, maji, umeme, nishati, elimu, kilimo nk
   
 8. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #8
  Aug 5, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,222
  Likes Received: 3,782
  Trophy Points: 280
  Mpasuko haukuanza leo! Muasisi wa mpasuko huo na muathirika mkuu ni Jakaya Kikwete!
  Hana uwezo wa kuuzuia,kilichobaki ni huruma ya wajumbe hao tu!
   
 9. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #9
  Aug 5, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  source:gazeti la kulikoni.
   
 10. Laurence

  Laurence JF-Expert Member

  #10
  Aug 5, 2011
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 3,106
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Watajijua wenyewe namagamba yao waendelee kupasuka zaidi maana wote ni majizi mpaka wamefikia hatua ya kushirikiana na wanajeshi(Shimbo) kuiba mipesa yetu,viongozi wa nchi hii walioko madarakani wanakera sana
   
 11. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #11
  Aug 5, 2011
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  CCM Woyeeeeeeee!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 12. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #12
  Aug 5, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,529
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Tanzania tuna mikoa 25; ukuzungumza wenyeviti wa mikoa unazungumzia watu 25 kati ya wanachama wapatao 4000. Hakuna mpasuko wowote ni hofu tuu ya kuwakosa watu waliozoeleka kwenye kundi
   
 13. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #13
  Aug 5, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mkuu, CCM hivi sasa mpasuko hauwatazami bali imeshapasuka na kugawanyika vipande vingi sana. Kama ukiamua kuhesabu factions zote zuilizotokana na mpasuko huo, unaweza kumaliza vidole vya mikono na miguu na bado ukawa haujamaliza makundi yaliyotokana na CCM. Kuna baadhi ya watu hivi sasa tunapata matatizo sana kujua ni kipi hasa kinamaanishwa mtu anapotaja CCM
   
 14. semango

  semango JF-Expert Member

  #14
  Aug 5, 2011
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 532
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  adui muombee njaa!
   
 15. F

  FJM JF-Expert Member

  #15
  Aug 5, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  @Vincent, I wish ningekuwa optimistic kama wewe hapo kwenye red. Subiri uchaguzi wa mwenyekiti 2012 ndio utaona uwekezaji wa 15 (15yrs) unalipa vipi.
   
 16. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #16
  Aug 5, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,595
  Likes Received: 4,709
  Trophy Points: 280
  Mimi changu ni kicheko tuuuuuuuuuuuuuuu.Magamba kwishneyiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
   
 17. m

  mudavadi Member

  #17
  Aug 5, 2011
  Joined: Apr 19, 2011
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa wenyeviti wa aina ya Mgeja, Guninita, Jah People na wengine kadhaa hiyo hainishangazi. Lakini wajue kwamba kuna wenyeviti wenye akili timamu, uwezo wa kujenga hoja na ushawishi kama vile Makongoro Nyerere ambao hawatakuwa tayari kuona mafisadi wakiendelea kukivuruga chama na kukitia matopeni. Kwa ujumla karibu la sahau la mafisadi lilishaandikwa na sasa hivi jitihada zao ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu.
   
 18. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #18
  Aug 5, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Kwani wenye viti wa mikoa wana madaraka kuwashinda wajumbe wa cc?wakifanya ujinga hao 25 si wanafukuzwa tu kwa nini wapinge maamuzi ya cc ya magamba?je hivi sasa magamba hawana mpasuko?
   
 19. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #19
  Aug 5, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Usicheze na kiongozi wewe, mwenyekiti ni mmoja JK lakini akisema mguu pande wanachama wote mil.4 mnatii mguu sawa mbele tembea mnakwenda unacheza nini.
   
 20. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #20
  Aug 5, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Don't try to please yourselves mechi ndio inataka kuanza haijaisha kama unavyosema.
   
Loading...