CCM hata kama ni kifo bora kiwe kifo cha heshima

Mtaka Haki

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
492
149
Kuna watu wanaogopa kuwa kuvuliwa magamba kunaweza kuleta kifo cha CCM. Lakini kuliko kuweka azimio la kuwataka wenye tuhuma za ufisadi waondoke na wasipoondoka chama kitawaondoa, basi kama kuwaondoa kunaleta kifo basi hicho kitakuwa kifo cha heshima. Kama CCM isipochukua hatua yeyote basi kifo kitatokea kisichokuwa cha heshima.
Itakufa kifo cha fedheha.
Namuomba tena mwenyekiti alinde heshima yake na ya chama na achukue hatua nzito kwa kufuata maamuzi ya chama chake, na hata maazimio/mapendekezo ya BUNGE LA JAMHURI. Heshima ya chama itarudi na hata heshima ya bunge.
Ni muhimu kujua watu wamechoka na wanaendelea kubeba chuki juu ya serikali na chama cha mapinduzi.
 
Tatizo linalokusumbua wewe unamwogopa Lowasa. Mwenyekiti wako anatambua akifanya jambo lolote ambalo litapelekea CCM kupungukiwa na nguvu na kuondolewa madarakani kwamba ndiyo mmezika chama chenu! Achana na stori za vijiweni za akina Sitta na Mwakyembe ndugu yangu,CCM ikipiga chini haitonyanyuka tena,hii pumzi kidogo unaona inapumua ni kwasababu bado iko na dola!
 
Watu wamechoka kumuuguza huyu Mgonjwa, Ni bora Afe watu wapate nafasi ya kufanya mambo mengine.
 
Kama mgonjwa anakufa basi afe na heshima. Kwa mfano De Clark wa Africa kusini aliua chama chake lakini anapaswa kuheshimiwa kwa sababu alianzisha mpango uliomweka Mandela huru.
 
Kifo kizuri asiwafukuze mafisadi! Ccm kufa ni wazi kabisa. Wakibaki walivyo watakuwepo kwa muda mpaka 2015 maana wana dola. Wakiwafukuza mafisadi 2015 hawafiki maana mafisadi ndio wamiliki wa dola. Watumishi wote wa dola shida yao ni pesa na wenye pesa ni mafisadi. Kwa vile mafisadi wana pesa kuliko ccm basi bora kumtii mwenye pesa.
 
Kifo kizuri asiwafukuze mafisadi! Ccm kufa ni wazi kabisa. Wakibaki walivyo watakuwepo kwa muda mpaka 2015 maana wana dola. Wakiwafukuza mafisadi 2015 hawafiki maana mafisadi ndio wamiliki wa dola. Watumishi wote wa dola shida yao ni pesa na wenye pesa ni mafisadi. Kwa vile mafisadi wana pesa kuliko ccm basi bora kumtii mwenye pesa.
Ile dhana ya kwamba chama cha siasa kinataka kufanya kila kiwezekanacho kibaki madarakani ndiyo pekee inayowasimamisha baadhi ya vyama. Lakini morally baadhi ya vyama vinapaswa vikubali kuwa kifo sio option na ni vizuri kuitii dhamira yao kuliko pesa
 
Back
Top Bottom