CCM Hamuwezi kupona bila kuipenda chadema na upinzani kwa ujumla!!

NAMBA MOJA AJAYE NCHINI

JF-Expert Member
Oct 29, 2019
8,516
17,425
Wanabodi za jioni!poleni kwa changamoto za Corona,sukari na kukosa matumaini ya nchi yetu!!!

CCM mngetengeneza demokrasia yetu!!kuliko kutumia polisi na rasilimali nyingi kuua upinzani nchini!Hao mnaowaita mabeberu walileta demokrasi ili kutugawa tusiwe wamoja kama wao,wanaogopa umoja wetu utaumiza maslahi yao lakini kwa kutoutambua mtego huu mmeingia kichwa kichwa hadi mmeligawa taifa.Leo upinzani wanatafuta msaada nje ya nchi kupambana na serikali hatua hii ni kufeli kwa utanzania wetu,kufeli kwa usalama wa taifa,kufeli kwa uzalendo wetu yaani mmefeli kabisa kila kitu!kwa maana nyingine siri za taifa letu zimevuja kwa maadui kwa kushindwa kuuhodhi upinzani nchini!!!

Kwanini msijifunze kwa hao waliotuletea demokrasia?Pale marekani Republican na democratic wanabadilishana vijiti kila awamu,Pale uingereza Conservative na Labour party nao hivo hivo!!!Nyie mmeshindwa nini kucheza mchezo huu?kwanini msitengeneze demokrasia yetu na vyama vikuu viwili vitakavyo badilishana madaraka na ku recruit wazalendo wa pande zote za vyama hivi????Leo jpm asingetumia fedha za maendeleo kwenye manunuzi ya kishenzi ya wapinzani wala ndugu zetu polisi wasingefanywa watesaji wa ndugu zao kisa kikundi cha wahalifu waliomo CCM wajilinde na wizi wao!!!!

Kama mtaendelea kuuchukia upinzani badala kuupenda na kuutumia ku balansi hisia za watz mtaishi kwa shida sana kwa ulinzi wa mtutu kama majambazi !!!Nyakati zimebadilika acheni kuwalazimisha wananchi itikadi yenu wape nafasi ya kupumua kwa kutengeneza upinzani wa kweli ambao utakuwa mbadala wa hisia zao!!!!!Mtakuja iingiza nchi kwenye machafuko kisa kutetea uchama kama anavofanya sizonje!!!

Ni wakati wa mabadiliko ya muelekeo wa siasa zetu!tumechoka damu zinazomwagika kila uchwao kulinda chama tawala!!!RIP DR.OMARI ALLY JUMA,MWANGOSI,ALPHONCE MAWAZO,HORACE KOLIMBA,IMRAN KOMBE NA N.K..
Hivi NDUGU zangu the state huwa mna masikio? Mkitaka kufanya hicho nilichoshauri na ukiongeza na upatikanaji wa katiba mpya Basi mtumie mtu wa kawaida kabisa tena mtumishi wa chini kabisa mfanyakazi wa kawaida ndio atwae kiti cha uraisi ili afate maekezo yenu katiba mpya ipatikane na demokrasia ya kweli!!lakini mkitumia makada wazoefu wa chama tena wenye mtandao watawasumbua Sana!!Nadhani mnitumie mimi uwezo ninao wa kuwapatia katiba mpya na demokrasia ya kweli na uwezo ninao!!tena kijana mdogo kabisa nayaweza Hayo tena Sana!kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 katiba mpya ishapatikana!!
 
Kiukweli vyama vyote hapa bongo miyeyusho ila ccm imezidi miyeyusho, yaani wanaongoza nchi lakini kihuni sana.Spika wao aliacha kuilinda katiba aliyoapa kuilinda kitambo sana. Ccm walichobakiza Ni ubabe Na kutumia vyombo vya dola kibabe.
 
Chadema Lazima ife ili kizaliwe chama cha upinzani kinachojitambua km Nccr mageuzi

Sio wahuni wa ufipa wanaotumika na Mabeberu
 
Chadema Lazima ife ili kizaliwe chama cha upinzani kinachojitambua km Nccr mageuzi

Sio wahuni wa ufipa wanaotumika na Mabeberu
Tatizo kubwa ccm njia wanayoitumia kuiua chadema ndo wanaipaisha zaidi, mitaani wananchi wanasema wale wabunge kumi wote walioasi maamuzi ya chadema walipaswa kufukuzwa wote. Tatizo kubwa LA ccm haijajua umma kwa nn wanaiamini chadema
 
Duh! hii hoja ya kulazimishana wote kuwa ccm ndio uwa naipinga mpaka kesho watu hatuwezi kuwa na mawazo ya namna moja!

Nchi lazima ikubali kuwa kuna Ccm, Kuna Wapinzani ni mahitaji ya wakati hata iweje nchi hii haitakuwa moja bila kuwepo mfumo unaosikiza pande zote na bado tutaingia kwenye mgogoro mkubwa uko mbeleni

Ccm imechokwa na isipojipanga viongozi wake watafungwa kwa kuleta machafuko tuendelee kuwepo.
 
Bado sana kwa hivi vikundi vya wahuni au saccos kukabidhiwa taifa kuongoza.
Wao waendelee kubweka ili kuwastua walio ndani wasilale jumla.

Hatuwezi kujifananisha na Marekani au Waingereza, wana miongo mingi yakujenga hio tunayoiona ni demokrasia ya kuiga.

Kwahiyo NYUMBU tuvumiliane tu hakuna namna nyie kushika madaraka piga garagaza haipo.
Ni mpaka CCM ipasuke vipande na sio leo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chadema Lazima ife ili kizaliwe chama cha upinzani kinachojitambua km Nccr mageuzi

Sio wahuni wa ufipa wanaotumika na Mabeberu

Mmekipotezea CUF mvuto baada ya kumtumia Lipumba kama kondomu, saa hii mnamrukia Mbatia mkidhani atapata mvuto. Wananchi sasa hivi wanachagua wamtakaye, sio anayetakiwa na genge la ccm.
 
Kama CCM ni mzimu Basi tutaiuliza mizimu iseme kafara GANI inataka ili iachie nchi hata kwa miaka mitano tu ili tuingize chama kingine kwa muda huo Halafu CCM itarudi tena kwa miaka mingine mitano tena kuwa kupokezana vijiti!!!
 
Back
Top Bottom