CCM hamnaga Siasa mbadala zaidi ya kuumizwa na Chadema

MAGEUZI KWELI

JF-Expert Member
Jul 16, 2011
1,947
253
Sioni Sababu ya watu kuongea bungeni, Sijui Chadema kafanya nini au lile, Hoja mbazo kweli zinaonekana kama ni mtaji kwenu CCM lakini kweli ni hasara na kujishusha kwa Hali ya Juu.
Mara ngapi Chadema kinatamkika kwenye baadhi ya vichwa vya watanzania?
Kama ingekuwa ni Maradhi kweli Muhimbili ingekuwa ndogo kutibu wanaougua Maradhi yaitwayo Chadema.
Yaacheni ya Chadema yabakie chadema na ya CCM mubebe wenyewe kama wenye dola.
Nimechoka ..Daily Mbowe, Daily Zitto, Daily Slaa, Why....?

I am proud to be Chadema as i do believe the same, People don't like me at all.

Mods, Please Keep this...
 
Watazipata wapi, Itikadi wala falsafa, wataongelea nini?

Angalia hapa:

FALSAFA YA CHADEMA

  1. Falsafa ni fikra na mtazamo wa Chama ambayo ni kuamini katika "Nguvu na Mamlaka ya Umma" (The People's Power) katika kumiliki, kuendesha, kubuni, na kuendeleza maamuzi, mawazo, rasilimali, uchumi na siasa ya nchi yao.
  2. Aidha falsafa ya "Nguvu na Mamlaka ya Umma" ndiyo msingi na chimbuko la kuundwa dola ya nchi, na kuwa, Umma ndiyo wenye madaraka ya mwanzo na ya mwisho katika kuamua hatima ya nchi na taifa pasipo kuingiliwa, kudanganywa au kughilibiwa na viongozi, watawala au wageni.
  3. Ujenzi na udumishaji wa Demokrasia na Maendeleo nchini vitatokana na Nguvu na Mamlaka ya Umma wa Watanzania. Nguvu na Mamlaka ya Umma itabainishwa, kuainishwa na kulindwa katika Katiba ya nchi na Umma ndiyo utakuwa chimbuko la Katiba hiyo.
  4. Historia inaonyesha kuwa "UMMA" wa Watanzania haujawahi kuwa na sauti, mamlaka na madaraka juu ya maamuzi ya hatima ya maisha ya watu. Uhuru, nguvu, mamlaka na madaraka wakati wote, tokea enzi za ukoloni mpaka leo, vimekuwa vikihodhiwa na kumilikiwa na watu wachache ambao wana mamlaka ya kuongoza SERIKALI na kuwakandamiza wananchi.
  5. CHADEMA tunaamini kuwa mifumo na miundo ya utawala wa nchi yetu havijawapo kwa ajili ya kuutumikia umma, bali umma ndiyo huzitumikia serikali hizo ambazo ni mali ya watu wachache wanaopoka "Nguvu ya Umma". Sambamba na hilo, umma wa Watanzania umekuwa hauna mamlaka ya mwisho ya kuhoji maamuzi ya serikali yanayowaathiri watu, na hivyo kujikuta hauna mamlaka juu ya rasilimali, sheria, utawala, na uendeshaji wa nchi. Aidha, Katiba ya Nchi imekuwa miliki ya Serikali kwa kutumia Bunge ambalo linatawaliwa na mawazo kongwe ya ukiritimba wa enzi za mfumo wa Chama kimoja cha siasa nchini.
  6. CHADEMA tunaamini na kutambua kuwa "kuchaguliwa" kuunda utawala wa kuongoza nchi hakumaanishi wachaguliwa kujitwalia mamalaka ya UMMA na kisha kuyatumia mamlaka hayo kuwakandamiza "waliowachagua" kwa sababu tu ya kutetea maslahi binafsi badala ya maslahi ya umma.
  7. Hivyo basi, falsafa ya "Nguvu na Mamlaka ya Umma" ndiyo njia ya msingi ya kubadilisha fikra na uongozi unaokandamiza umma, ili kuibua fikra mpya na kuweka uongozi unaoweza kumilikiwa, kuhojiwa, na kuwajibishwa na umma kwa kutumia vyombo vilivyopatikana kwa utashi wa wengi kupitia chaguzi huru na za haki.
  8. Falsafa ya "Nguvu na Mamlaka ya Umma" inalenga kuwaamsha, kuwahamasisha, kuwaelimisha, kuwashawishi na kuwaandaa Watanzania wachukue hatua ya kuimiliki, kuitawala, kuilinda na kuifaidi nchi yao tofauti na kipindi cha miaka mingi chini ya mfumo wa chama kimoja cha siasa na miaka kumi na nne ya mwanzo ya mfumo wa vyama vingi.
Hebu tafuta kama CCM wana kitu kinachofanana na hiki. Tangu Nyerere afe wameshindwa kabisa kuandika chochote. Na ndicho kolimba alichowaambia. Hakuna hata mtu mmoja anaelewa Kolimba aliwaambia nini.
 
mbona cdm kila siku mulugo.mara muhongo.mara mwiguru. mara rizone kwani hamna sera zenu.
 
CDM inaongoza nchi, thats why hakuna mbunge wa CCM ama Waziri atamaliza kuchangia hoja yake bila kuizungumzia CDM. Sasa hivi wameishiwa mpaka wanaingilia mambo ambayo hayana tija kwa taifa!!

Inafikia hatua mbunge wa CCM anatumia dakika zake zote kulia wivu bungeni - hii ni aibu sana kwa chama tawala.
 
Ukitaka kupendwa na wanaCCM na hata kupata uongozi CCM basi we ikandie CDM mara kwa mara. We angalia viongozi wengi wa CC ya CCM ndio utaelewa.
 
quote_icon.png
By amakyasya

CHAMA CHAKAVU huzaa HOJA CHAKAVU, MAWAZIRI MIZIGO, WABUNGE MIZIGO ...

Well thought
 
mkiondoa siasa za majitaka za ccm basi watafutieni kazi masalia wote , maana njaa kali ndiyo iliyowasukuma kutukana cdm .
 
SIKU ZOTE NAAMINI FALSA ZA CDM. Mungu wabariki wananchi wa TZ kuendelea kuchagua kilicho mahususi kwao ili kuondokana na utumwa juu ya mtu mweusi ccm na vibaraka wake chini ya utawala wa shetani.
 
Back
Top Bottom