Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,280
- 25,858
- Ni nyinyi ambao mmekuwa mkiunda Serikali kwa miaka yote kabla na baada ya kuanza kuchimbwa madini.
- Ni nyinyi ambao, kupitia wingi wa Wabunge wenu Bungeni, mlipitisha Sheria zote zinazohusu madini na uwekezaji kwa ujumla. Mfano ni mwaka 1997 na 1998 ambapo Sheria ya Uwekezaji na ile ya Madini zilipitishwa kwa Hati ya Dharura.
- Ni nyinyi ambao mlipigia debe sera za utandawazi na ubinafsishaji/uwekezaji.
- Ni nyinyi ambao mlikuwa kwenye nafasi za kiserikali wakati wa majadiliano na hata utiwaji saini wa mikataba ihusuyo madini.
- Ni wana-CCM ndio walikuwa washauri na wapigadebe wa masuala yote ya madini.
- Ni wana-CCM ndio waliozima hoja ya kupeleka mikataba yote ya madini Bungeni ili Bunge liione,kuijadili na kuithibitisha.
Wana-CCM hamna sifa, uwezo wala nafasi ya kumuunga mkono Mhe. Rais na kupoka suala lake na kulifanya kama moja ya mafanikio ya CCM. Nyinyi mnapaswa kujificha ndani na kuangua kilio kwa jinsi mlivyoyafikisha mambo haya hapa yalipo. Wana-CCM mnapaswa kufanya toba na kujitenga na Mhe. Rais katika hili. Watanzania tunaomuunga mkono Rais tunatosha.