CCM hakuna sababu ya kufanya kampeni 2020 tunahitaji kupita bila kupingwa

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Jul 31, 2017
1,606
1,956
Wana JF wote!

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Ndg Kheri Denice James amesema kuwa CCM haina sababu ya kufanya kampeni katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 badala yake kuna kila sababu ya kupita bila kupingwa kutokana na uimara wa CCM na serikali yake.

Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa ameyasema hayo Leo 12 Januari 2018 wakati akizungumza na Timu mbalimbali za kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani wa Kata ya Kimandolu Mkoani Arusha kutoka jumuiya za CCM sambamba na mabalozi wote wakati wa kikao cha ndani kilichofanyika Mtaa wa Kijenge Kaskazini Kata ya Kimandolu.

Kheri alisema kuwa serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli imedhamiria kutatua kero zote zisizo rafiki kwa wananchi kwa utekelezaji wa Mkataba wa wananchi na CCM kupitia ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015-2020.

Kheri aliwataka wananchi kujitokeza kwa mwingi kupiga kura hapo kesho 13 Januari 2018 kwani ni haki yao ya msingi kikatiba lakini pia aliwakumbusha kuwa katika uchaguzi huo wananchi wanapaswa kumchagua Diwani wa CCM kwa ajili ya maendeleo endelevu kwa ajili ya mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla wake.

Katika uchaguzi huo mdogo utakaofanyika kesho katika Kata ya Kimandolu Ndg Gaudence Limo ndiye mgombea wa CCM ambaye aliwahi kuwa Meya wa Jiji la Arusha.

Katika hatua nyingine Mwenyekiti Kheri alivifananisha vyama vya upinzania nchini Tanzania na waharamia ambao kazi yao kubwa ni wizi na ujambazi, ujangili, udokozi, utapeli na uongo hivyo kupitia ulaghai wao haviwezi kufanikiwa kushika dola kwa zaidi ya miaka 50 ijayo.

Aliwasihi vijana kukumbuka majukumu yao kama nguvu kazi ya Taifa kuwa ni pamoja na kusema ukweli, kuwajibika na kuwa watendaji na viongozi madhubuti sio viongozi biskuti.

Aidha, Kheri amewafikishia wakazi wa Arusha salamu za Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kuwa anahitaji ushindi wa kishindo wa zaidi ya kura 12,000 na hiyo itakuwa zawadi pekee kwake.

“Ndugu zangu sisi wana CCM tunaweza kujadiliana harusi itafungwa vipi na wapi, tunaweza tukajadiliana aina ya magari ya kununua lakini hatuwezi kuwa na mjadala wa namna yoyote ile kwenye utafutaji wa dola ni lazima CCM ishinde” Alikaririwa Kheri James
Chanzo: Mwenyekiti wa UVCCM Taifa
Ndugu Kheri James
 
Tatizo lanchii hii nikujipendekeza kwa vijana wengi na kuwaachia wazee wajenge Uchumi wataifa hili yaani ndo tatizo linaloikabili hii nchi kwa sasa,mawazo finyu yanamna hii mtafanya nchi ya viwanda iwe historia
 
Madaraka ya kulevya
 
Hapo mnapoandikagauzi mrefu alafu mwishoni mnaweka namba za simu,hapo ndio huwa siwaelewagi kuwa je hayo mnayoongeaga mnaongeaga kwa dhati au huwa ni process za kusaka tonge
 
Subutu yenu labda muamuwe kumwaga Damu za watanzania ila kaa mtambuwe wananchi tulio wengi hatuitaki ccm over 70% we just fed up kabisa kabisa Yaani msijidanganye hata chembe kwa kununua hao mamluki kwa pesa za walipa kodi .... Tuone Kama mtaweza kutu nunua over 40millions ya wa tz
 
mimi nilishawambia uvccm siyo jumuiya ya vijana kama inavyopaswa kuwa bali ni genge la wasaka vyeo na teuzi ndani ya serikali.Kwa mantiki hiyo usitegemee kwa mtu yeyote aliyeko kwenye hili asumbue akili zake kufikiria na kuongea ukweli.
Labda WAKATUBU
 
Kweli kabisa,hata uchaguzi huu hapakuwa na sababu ya kufanya kampeni maana mnashindana na kivuli chenu.
 
Ni uwendawazimu uchaguzi huu kupoteza fedha kwa kufanya kampeni wakafi huna unayeshindana naye. Kwa nini NEC isingewatangaza waliopitishwa na CCM kuwa wamepita bila kupingwa?
 
hayo matusi ndyo viwanda enyewe?kweli hi awamu niya hovyo kuliko awamu zote.ni awamu iliyojaa uwizi na ufisadi uliokubuhu,hatuoni sbb tupo gizani.embu bunge liwe huru na live kuwe na uhuru wa vyombo vya habari ndyo utajua ufisadi na uwizi ktk awamu hi
 
Wana JF wote!

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Ndg Kheri Denice James amesema kuwa CCM haina sababu ya kufanya kampeni katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 badala yake kuna kila sababu ya kupita bila kupingwa kutokana na uimara wa CCM na serikali yake.

Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa ameyasema hayo Leo 12 Januari 2018 wakati akizungumza na Timu mbalimbali za kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani wa Kata ya Kimandolu Mkoani Arusha kutoka jumuiya za CCM sambamba na mabalozi wote wakati wa kikao cha ndani kilichofanyika Mtaa wa Kijenge Kaskazini Kata ya Kimandolu.

Kheri alisema kuwa serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli imedhamiria kutatua kero zote zisizo rafiki kwa wananchi kwa utekelezaji wa Mkataba wa wananchi na CCM kupitia ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015-2020.

Kheri aliwataka wananchi kujitokeza kwa mwingi kupiga kura hapo kesho 13 Januari 2018 kwani ni haki yao ya msingi kikatiba lakini pia aliwakumbusha kuwa katika uchaguzi huo wananchi wanapaswa kumchagua Diwani wa CCM kwa ajili ya maendeleo endelevu kwa ajili ya mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla wake.

Katika uchaguzi huo mdogo utakaofanyika kesho katika Kata ya Kimandolu Ndg Gaudence Limo ndiye mgombea wa CCM ambaye aliwahi kuwa Meya wa Jiji la Arusha.

Katika hatua nyingine Mwenyekiti Kheri alivifananisha vyama vya upinzania nchini Tanzania na waharamia ambao kazi yao kubwa ni wizi na ujambazi, ujangili, udokozi, utapeli na uongo hivyo kupitia ulaghai wao haviwezi kufanikiwa kushika dola kwa zaidi ya miaka 50 ijayo.

Aliwasihi vijana kukumbuka majukumu yao kama nguvu kazi ya Taifa kuwa ni pamoja na kusema ukweli, kuwajibika na kuwa watendaji na viongozi madhubuti sio viongozi biskuti.

Aidha, Kheri amewafikishia wakazi wa Arusha salamu za Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kuwa anahitaji ushindi wa kishindo wa zaidi ya kura 12,000 na hiyo itakuwa zawadi pekee kwake.

“Ndugu zangu sisi wana CCM tunaweza kujadiliana harusi itafungwa vipi na wapi, tunaweza tukajadiliana aina ya magari ya kununua lakini hatuwezi kuwa na mjadala wa namna yoyote ile kwenye utafutaji wa dola ni lazima CCM ishinde” Alikaririwa Kheri James
Chanzo: Mwenyekiti wa UVCCM Taifa
Ndugu Kheri James
Goli la mkono katika ubora wake
 
Back
Top Bottom