CCM Hakuna asiye Fisadi; Hata Akiwepo Atabadirika na Kuwa Fisadi Mwandamizi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM Hakuna asiye Fisadi; Hata Akiwepo Atabadirika na Kuwa Fisadi Mwandamizi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by eedoh05, Sep 17, 2012.

 1. e

  eedoh05 JF-Expert Member

  #1
  Sep 17, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 633
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  Ukiwachunguza viongozi wa CCM hutashindwa kung'amua ufisadi ulivyowakolea hadi kwenye kope zao. Ukiziangalia na kuchunguza pua zao utagundua zinacheza cheza kama za sungura zikinusanusa uwepo wa rushwa na ufisadi.

  Kwa nini wote wamekuwa mafisadi hasidi. Moja, ili kupata au kugombea nafasi za uongozi wa ngazi yo yote ile ''pesa'' hutumika. Kwa hiyo, kila mtarajia kugombea uongozi ndani ya chama na hata nje ya chama, rushwa humiliki mchakato mzima wa kumpata mgombea hata kushiriki uchaguzi wenyewe.

  Hapa ndipo chama chote hufuka ufisadi.

  Mbili, CCM kina makundi lukuki ndani yake. Kila kundi hujitengenezea '' territory of influence''. Kanuni yao ni ile ile kama ya simba mnyama kujitengenezea territorial ya kuwindia.Tofauti ni kwamba simba hutumia nguvu, makundi ndani ya CCM hutumia fedha.

  Tatu, kuna kundi la wafanyabiashara wasiozidi 18 ambao wanaki-remote chama cha mapinduzi. Kundi hili limeshika uchumi wa nchi hii. Kundi hili linapenda kuona milele CCM wanashika dola ili wao waendelee kuifirisi nchi hii. Hawa ndio wafadhiri wa mlango wa nyuma wa CCM tangu mfumo wa vyama vingi uanze.

  Kwa hiyo, usishangae kuona hata yule mama aliyedai yeye ni mpambanaji dhidi ya ufisadi, wiki hii yote ameripotiwa kugawa mlungula mno mno ili awashawishi wapokea mlungula huo wamchague yeye kupata uenyekiti wa jumuiya moja ya CCM.

  Kwa kweli, hakuna asiye na harufu ya ufisadi ndani ya CCM kwa kadiri ya mfumo wao ulivyo kiutawala tangu Mwl.Nyerere afariki dunia. CCM NI KIINI CHA DEMOKRASIA YA KIFISADI NCHINI.
   
 2. LE GAGNANT

  LE GAGNANT JF-Expert Member

  #2
  Sep 17, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 1,247
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Chama cha wakulima na wafanyakazi wa zamani na mafisadi wa sasa.
   
 3. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #3
  Sep 17, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,810
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  Mkuu umelonga, Bila ya Rushwa, no cheo
   
 4. K

  KakindoMaster JF-Expert Member

  #4
  Sep 17, 2012
  Joined: Dec 5, 2006
  Messages: 1,349
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Ukiangalia kwa makini ufisadi ni huruka ya watanzania. Hebu angalia ni watanzania wangapi wako nchi nyingine wamelizwa na ndugu zao/ Kaka zao/ dada zao? Umeona jinsi watanzania wenzetu ktk makampuni yaliyoko hapa nchini yanavyo fanya uhalifu kama huu? Naona wengi ndo walivyo. Kuna haja ya kubadilika jamani. tuone aibu. Badilikeni.
   
 5. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #5
  Sep 18, 2012
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Mkuu hii sio tetesi, ni kweli kabisa hata zomba na ritz ni mafisadi
   
Loading...