CCM haitowavua uwanachama wanaotuhumiwa kwa ufisadi

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,184
671
CCM haitowavua uwanachama wanaotuhumiwa kwa ufisadi
2008-03-26 09:47:03
Na Mashaka Mgeta

Chama Cha Mapinduzi (CCM), hakina mpango wa kuwanyang`anya kadi, waliokuwa viongozi wa Serikali na wabunge, wanaotuhumiwa kuhusika katika kashfa mbalimbali za ufisadi nchini.

Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Yusuf Makamba, aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam, alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) utakaofanyika Machi 29 na 30, mwaka huu, kijijini Butiama, mkoa wa Mara.

Alisema kuibuliwa kwa tuhuma za ufisadi, kulifanyika bungeni na Serikali iliagizwa kusimamia utekelezaji wa mapendekezo ya Kamati Teule ya Bunge, iliyoongozwa na Dk. Harrison Mwakyembe.

``Hawa watu kama walishutumiwa kwa ufisadi na wao kujiuzulu, si inatosha, kwa maana sisi kama Chama tuliwapongeza kwa kujiuzulu kwao... Sasa mnataka wanyang`anywe hadi kadi?`` Alihoji.

Baadhi ya viongozi waliohusishwa katika kashfa hiyo na kutajwa kwenye mkutano wa Bw. Makamba na waandishi wa habari jana, ni pamoja na aliyekuwa Waziri Mkuu, Bw. Edward Lowassa.

Wengine ni waliokuwa Mawaziri, Dk. Ibrahim Msabaha, (Afrika Mashairiki), Bw. Nazir Karamagi (Nishati na Madini) na Mbunge wa Igunga (CCM), Bw. Rostam Aziz.

Aidha, Bw. Makamba alisema hatua ya CCM kufanyia mkutano wa NEC kijijini Butiama, haina maana ya kwenda kufanya matambiko kwenye kaburi la Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere.

Alisema hivi sasa, kuna fikra potofu miongoni mwa watu kuhusisha mkutano huo na matambiko ama kuomba radhi kwenye kaburi la Mwalimu Nyerere, suala alilosema halimo katika ajenda za mkutano huo.

``Hatuendi kutambika wala kuomba radhi, kama ni radhi tungeiomba kanisani, lakini hiyo haitatuzuia kuzuru kaburi hilo na kumuombea,`` alisema.

Alizitaja ajenda za mkutano huo kuwa ni hali ya kisiasa nchini, kutoa taarifa ya mazungumzo ya mwafaka kati ya CCM na Chama Cha Wananchi (CUF) kuhusu mgogoro wa kisiasa visiwani humo.

Kwa mujibu wa Bw. Makamba, ajenda nyingine ni kutathmini hali ya uchumi wa nchi kwa njia ya semina itakayoendeshwa na Gavana wa Benki Kuu, Profesa Benno Ndulu, taarifa za uchaguzi mdogo wa ubunge jimboni Kiteto, sherehe za miaka 31 ya CCM na maendeleo ya shughuli za chama.

Bw. Makamba alifafanua kuwa hatua ya kufanyia mkutano wa NEC mikoani ilianza tangu 1967, ulipofanyikia mkoani Arusha, mahali lilipozaliwa Azimio la Arusha.

Pia alisema mikutano mingine iliwahi kufanyika Iringa, Musoma, Handeni mkoani Tanga, kijijini Mkongo huko Rufiji na Zanzibar.

Naye Mweka Hazina wa CCM, Bw. Amos Makalla, alisema chama hicho kitatumia rasilimali zake kufanikisha mkutano huo, bila kutegemea msaada wa watu ama taasisi za kijamii.

Alisema mkutano huo upo katika kalenda ya CCM, ikiwa na bajeti iliyoanishwa kama ilivyo katika shughuli nyingine za CCM.

Bw. Makalla, alikuwa akifafanua kuhusu swali kama kuna wafanyabiashara waliojitokeza kutoa msaada wa usafiri kwa wajumbe wa NEC kwenda kijijini Butiama.

SOURCE: Nipashe
 
Makamba is back!

Naona sasa wamempa uhuru wa kuongea na wanahabari tena!
Shughuli mbele huko mbele ya safari na yangu macho....!
 
Huyu makamba anaongea ujinga.. Kama bunge lilitoa mapendekezo kwa Serikali na wao (watuhumiwa) waka jiuzulu... inamaana ni politcal accountability... Bado legal, wachunguzwe na kuchukuliwa hatua zaki Sheria as per the Penal Code and other Laws governing Public Officials' practices..

CCM kama chama inabidi wawajibishe Kichama... completely separate from the Political and Legal accountability.. Aache mambo yakiswahili.. Kazi kupiga porojo tu.. ndio maana alinunuliwa ilenyumba yake ya serikali na Yusuph Manji. Mtu mchafu anatuchafulia Nchi. Chama Cha Mapinduzi inabidi kiset a new precedence kwa kuonyesha kuwa kikotayari kujitakasa... Kuondoa corrupt elements.. vinginevyo chenyewe kitakufa. Kama vingine vilivyokufa baada ya kupoteza imani ya wananchi...
 
Ukweli ni Kwamba watanzania ndio hatujakaa sawa CCM nani amwajibishe nani wote karibia asilimia themanini ya viongozi kwa njia moja au nyingine wameisha kosa dira(Malima, 199...). Wamejiingiza kwenye biashara. Sasa inatakiwa wapenda CCM(asilia) ya baba wa taifa wajitenge na wenzao. Hivyo makamba bado yake macho tu hana mahamuzi
 
Hakuna cha kushangaza, maana wakifanya hivyo itabidi wafute chama maana hakuna atakayebaki kwa wale wenye nyadhifa za juu.
 
Itakuwa down to uvivu wa kufikiri kama kuna yeyote angekuwa anategemea hawa vingunge wa CCM wangeanza kuvuana uanachama kwa sasa!
 
Back
Top Bottom