Mtu wa Pwani
JF-Expert Member
- Dec 26, 2006
- 4,191
- 674
CCM haitowavua uwanachama wanaotuhumiwa kwa ufisadi
2008-03-26 09:47:03
Na Mashaka Mgeta
Chama Cha Mapinduzi (CCM), hakina mpango wa kuwanyang`anya kadi, waliokuwa viongozi wa Serikali na wabunge, wanaotuhumiwa kuhusika katika kashfa mbalimbali za ufisadi nchini.
Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Yusuf Makamba, aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam, alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) utakaofanyika Machi 29 na 30, mwaka huu, kijijini Butiama, mkoa wa Mara.
Alisema kuibuliwa kwa tuhuma za ufisadi, kulifanyika bungeni na Serikali iliagizwa kusimamia utekelezaji wa mapendekezo ya Kamati Teule ya Bunge, iliyoongozwa na Dk. Harrison Mwakyembe.
``Hawa watu kama walishutumiwa kwa ufisadi na wao kujiuzulu, si inatosha, kwa maana sisi kama Chama tuliwapongeza kwa kujiuzulu kwao... Sasa mnataka wanyang`anywe hadi kadi?`` Alihoji.
Baadhi ya viongozi waliohusishwa katika kashfa hiyo na kutajwa kwenye mkutano wa Bw. Makamba na waandishi wa habari jana, ni pamoja na aliyekuwa Waziri Mkuu, Bw. Edward Lowassa.
Wengine ni waliokuwa Mawaziri, Dk. Ibrahim Msabaha, (Afrika Mashairiki), Bw. Nazir Karamagi (Nishati na Madini) na Mbunge wa Igunga (CCM), Bw. Rostam Aziz.
Aidha, Bw. Makamba alisema hatua ya CCM kufanyia mkutano wa NEC kijijini Butiama, haina maana ya kwenda kufanya matambiko kwenye kaburi la Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere.
Alisema hivi sasa, kuna fikra potofu miongoni mwa watu kuhusisha mkutano huo na matambiko ama kuomba radhi kwenye kaburi la Mwalimu Nyerere, suala alilosema halimo katika ajenda za mkutano huo.
``Hatuendi kutambika wala kuomba radhi, kama ni radhi tungeiomba kanisani, lakini hiyo haitatuzuia kuzuru kaburi hilo na kumuombea,`` alisema.
Alizitaja ajenda za mkutano huo kuwa ni hali ya kisiasa nchini, kutoa taarifa ya mazungumzo ya mwafaka kati ya CCM na Chama Cha Wananchi (CUF) kuhusu mgogoro wa kisiasa visiwani humo.
Kwa mujibu wa Bw. Makamba, ajenda nyingine ni kutathmini hali ya uchumi wa nchi kwa njia ya semina itakayoendeshwa na Gavana wa Benki Kuu, Profesa Benno Ndulu, taarifa za uchaguzi mdogo wa ubunge jimboni Kiteto, sherehe za miaka 31 ya CCM na maendeleo ya shughuli za chama.
Bw. Makamba alifafanua kuwa hatua ya kufanyia mkutano wa NEC mikoani ilianza tangu 1967, ulipofanyikia mkoani Arusha, mahali lilipozaliwa Azimio la Arusha.
Pia alisema mikutano mingine iliwahi kufanyika Iringa, Musoma, Handeni mkoani Tanga, kijijini Mkongo huko Rufiji na Zanzibar.
Naye Mweka Hazina wa CCM, Bw. Amos Makalla, alisema chama hicho kitatumia rasilimali zake kufanikisha mkutano huo, bila kutegemea msaada wa watu ama taasisi za kijamii.
Alisema mkutano huo upo katika kalenda ya CCM, ikiwa na bajeti iliyoanishwa kama ilivyo katika shughuli nyingine za CCM.
Bw. Makalla, alikuwa akifafanua kuhusu swali kama kuna wafanyabiashara waliojitokeza kutoa msaada wa usafiri kwa wajumbe wa NEC kwenda kijijini Butiama.
SOURCE: Nipashe