Ccm haina ubavu wa kujibu hoja za chadema kwa wananchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ccm haina ubavu wa kujibu hoja za chadema kwa wananchi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Japhari Shabani (RIP), Mar 7, 2011.

 1. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #1
  Mar 7, 2011
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Baada ya mikutano na maandamano ya CHADEMA, kuwafikishia ujumbe mbalimbali kuhusiana na matatizo yanayowakabili walalahoi yanayosababishwa na utawala wa mbovu CCM.Tumeshuhudia chama tawala na serikali badala ya kutafakari na kujibu hoja za CHADEMA au kujaribu kuyatafutia matatizo yanayowakabili walalahoi,wanakja na vitisho na kukilaumu CHADEMA kwa kauli zisizo na msingi.Tishio la amani na kuleta machafuko,udini,ukabila,uchochezi,wanapata pesa kutoka nje kuleta machafuko,uchaguzi umekwisha maandamano ya nini n.k.Kitu walichokifanya ni kuwaendea wananchi na kua nao karibu na kuwaelezea na kujadiliana na wananchi kuhusu matatizo yao na si kufanya kama ilivyozoeleka kwa viongozi wa CCM ambao uwatembelea wananchi wakati wa uchaguzi,kufungua au kuweka mawe ya misingi miradi (Ambayo mingi ufa baada ya kuwekewa majiwe ya misingi au baada ya kufunguliwa)Na kutoa ahadi nyingi za uongo.Kwa maana hiyo CHADEMA ni tishio kwa Watawala CCM na mafisadi.CCM imekaa kimya kwa sababu haina cha kuwaambia wananchi.Nini wataenda kuwaambia ari bora,maisha bora,elimu bora?,uongozi bora?????!!Hali ilivyo wanaogopa hata kuwaendea wananchi kwani nchi walikoifikisha wakienda huko wataambulia kipigo kutoka kwa wananchi na askari watafanya jitihada za kuwalinda viongozi hao dhidi ya wananchi.Wananchi wamechoka.Kwa hiyo kwao wameamua kuja na kauli za ajabu ajabu kupitia vyombo vya habari.Baba wa taifa alisema katika moja ya hotuba zake ya kua viongozi wanaoenzi udini na ukabila HOJA ZIMEFIRISIKA hili tunaliona kwa CCM na viongozi wao.Hakuna umoja na kauli moja kwa nayotokea Rais anasema hili,Waziri mkuu lile,katibu kata ,waziri,mkuu wa mkoa ,mkuu wa wlaya n.k kila mtu anasemalinalomwijia kinywani vurugu tupu.Hali ilivyo hivi sasa NI VIGUMU KUAMINI KUA TUNAE RAIS NA TAASISI NZIMA YA UONGOZI!Kama CCM hailioni hili,hili ni tatitizo ambalo linaweza kusababisha upotevu wa amani.Na sio Dr.Slaa,Mbowe au CHADEMA wananchi wamechoka ENOUGH IS ENOUGH MUNGU IBARIKI TANZANIA.
   
 2. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #2
  Mar 7, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,468
  Likes Received: 3,740
  Trophy Points: 280
  Hawawezi kujibu hoja maana zina ukweli mtupu, mtoto akimwambia babake funga zipu ya suruali badala baba kufunga zipu anaanza kumtukana mtoto na kumpiga kwenzi. ndicho wanachofanya CCM. nawashauri CCM wapitie ahadi walizoahidi wakati wa kampeni waanze kuzitekeleza pindi wananchi watakapoona matunda watarudisha imani. kuendelea kutishia wananchi kwamba CDM wanavuruga amani sio suluhisho ya matatizo yao.
   
 3. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #3
  Mar 7, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,710
  Trophy Points: 280
  Nilipoisoma ile taarifa ya uvccm kuhusu cdm nkajua kweli ccm ni shake well before use!
   
Loading...