CCM haina mpinzani! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM haina mpinzani!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MwanaFalsafa1, Dec 11, 2009.

 1. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #1
  Dec 11, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Ijulikane kabisa kwanza hapa natoa maoni yangu kwa jinsi ninavyo ona hali halisi. Najua kuna watakao pina na watakao kubaliana na mimi. Either way huu ni mtsxsmo wangu.

  Tatizo kubwa ambalo tunalo nchini ni kwamba tuna chama kimoja chenye nguvu (the hegemonic party) na vyama vingine ambavyo vina sindikiza. Kwa maana hiyo Kila wakati ina julikana CCM ndiyo itachukua nafasi ya kwanza na vyama vingine vita gombania nafasi zilizo baki (uipende au uichukie CCM huu ndiyo ukweli). Kwa hiyo kunge kua na chama walau kimoja tu chenye uwezo wa kushika serikali basi mambo yasinge kua kama yalivyo.

  Ni ukweli usio pingika kwamba mtu anapo ona ana mpinzani mwenye uwezo wa kumshinda basi anaongeza bidii. Ni kama mbio vile. Kama mkimbiaje ana jua ana mpinzani ambae anaweza kumshinda basi anaongeza bidii na hapunguzi mwendo. kama hamna mpinzani basi hata spidi ya ukimbiaji wake uta pungua. Kama CCM haina mpinzani ina maana gani wao kuji kimbiza na kuji chosha? This is a challenge to the opposition.

  Pia ni hali ya ubinadamu kwamba mtu akiwa na mafanikio sana na akijua hana mpinzani basi ana kua na aconfidence fulani. Hii hali utaiona kwenye kila mtu mwenye mafanikio makubwa. tatizo ni kwamba kuna msitari mwembamba sana kati ya kujiamini na kujisikia. Labda kujiamini kwa CCm sasa kumekua kujisikia. Lina rudi pale pale kwamba hawana mpinzani.

  Wengi wata lalamika humu ndani kwamba CCM ina tumia faulo, upinzani unaonewa nk. Ukweli ni kwamba vyama vya upinzani ni power contenders dhidi ya CCM. Tokea lini ukaona mtu anamsaidia mpinzani wake kushinda? Hapa nataka upinzani tu wajua kwamba mafanikio yao yata tegemea sana na juhudi zao binafsi lakini kama ni kusubiria mpinzani wao awa saidie basi wata subiri mpaka kesho.

  Narudia tena. Tanzania ina hitaji walau vyama viwili vyenye uwezo wa kushindana na kupokeana madaraka (Kama vile Democrats na Republicans Marekani) na siyo chama kimoja chenye nguvu na msuluhu wa vyama visindikizaji.Ukiachana na ushabki wangu wa kichama nimekaa na kutafakari na kuona hili lita kua na manufaa makubwa kwa Taifa letu.

  Tanzania ni nchi changa na jinsi tunavyo komaa vyama hovyo vita jifia na vyama vyenye nguvu vita baki.
   
 2. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #2
  Dec 11, 2009
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Naafikiana nawe kwa kiasi kikubwa.Lakini hudhani kuwa nguvu ya umma inaweza kuiondoa CCM madarakani?Na kwa vile mie ni muumini wa Antonio Gramsci (na umegusia suala la hegemony) bado najipa matumaini kuwa pindi hasira za tabaka tawaliwa zikiweza kuwa consolidated then CCM's days of umafioso would be numbered!
   
 3. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #3
  Dec 11, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Ndiyo mkuu nguvu za umma zinaweza kuiondoa CCM. Lakni pia naamini kila kitu kina fanya kazi ndani ya mfumo fulani. Kwa Tanzania tuna chagua viongozi wetu kupitia vyama. Ina maana chama moja kikiondolewa kinaingia kingine. Sasa hicho chama kingine kina takiwa kuwa na nguvu za kutosha kushinda. Kuna msemo usemao "Chance favors the prepared". Upinzani una takiwa uwe tayari kupokea madaraka. Kwa mfano tungekua na upinzani wenye nguvu na maskendo yote yaliyo tokea awamu hii basi hapa tunge kua tuna zungumzia swala jingine kabis.Bado naamini as long as hakuna chama cha upinzani chenye nguvu bado CCM itaendelea kuwa juu.
   
 4. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #4
  Dec 11, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Matatizo ya vyama vya siasa vya upinzani
  Njaa za vyama vya upinzani hawana vyanzo vya mapato vya maana na hakuna mkakati wowote wa kufanya hivyo hivi karibuni,

  uwezo mdogo wa kiakili na hata kiuongozi, wananchi wamekosa imani nao na wala hawana jitahada za kutafuta viongozi wa kitaifa zaidi ya majungu na kuhudhuria maelezo na operation za zima moto for only and only one agenda ufisadi shame!

  Vyama vimekuwa mali binafsi ya koo anzilishi au mwenyekiti wa chama mwanzilishi..demokrasia kwenye vyama vya upinzani ni ndogo kuliko hata kwa ccm wao kwa wao..so hawawezi kuhubiri kitu ambacho hawawezi kuki-practice..wananchi wanatambua mapungufu haya na wanabaki na mshangao...ni vigumu kuunga mkono vyama vya upinzani

  Sijawahi kusikia wakitumia fursa wanazopata kwenye media, mkakati mbadala kwenye mambo ya maana kama vile elimu,afya, barabara, uchumi etc..kila kukicha wanajaza media na ku-critize tabia na mwenendo wa CCM...utegemee nini kutoka kwa aina hii ya upinzani?
   
 5. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #5
  Dec 11, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  "Sijawahi kusikia wakitumia fursa wanazopata kwenye media, mkakati mbadala kwenye mambo ya maana kama vile elimu,afya, barabara, uchumi etc..kila kukicha wanajaza media na ku-critize tabia na mwenendo wa CCM...utegemee nini kutoka kwa aina hii ya upinzani?"

  Tumain, I can't agree with you more. I was thinking the same thing.
   
 6. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #6
  Dec 11, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Hawa jamaa hawajui maana ya upinzani so far, ikiwa wananchi watapata elimu sahihi ya uraia then kwa aina hii ya upinzani wanaweza kukosa kura zaidi kuliko wanavyotegemea..four years wanazungumzia ufisadi basi how about elimu, afya, roads, housing, pensions etc..
   
 7. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #7
  Dec 11, 2009
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,503
  Likes Received: 2,744
  Trophy Points: 280
  Ni kweli CCM bado imeshika utamu, si unaona jinsi gani SG wa CC anavyotamba kumshinda PM mpaka anadiriki kuwaita watu wehu na wana wivu!!!!!????
   
 8. K

  Kinyikani Member

  #8
  Dec 12, 2009
  Joined: Dec 5, 2006
  Messages: 65
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hakuna lolote nguvu waliyonao CCM ni Tume ya Uchaguzi na kama kweli wanajiamini basi nakuomba washauri tume ya uchaguzi isiwe ya CCM watupu. Ama kusema upinzani hawana nguvu hiyo ni kweli kwasababu bila ya kutumiya nguvu za umma wasahau kushinda uchaguzi kwa kupitiya yume ya uchaguzi ya CCM.
   
 9. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #9
  Dec 12, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,688
  Likes Received: 82,553
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana nawe Tume ya uchaguzi ni kitengo kingine cha CCM. Hawa huangalia pembeni wakati CCM inakiuka taratibu mbali mbali za chaguzi kwa kuogopa "kitumbua chao kuingia mchana" pamoja na vitengo vingine vya CCM alias vyombo vya dola Polisi, Jeshi na FFU ambavyo vyote hutumika katika kuwatisha na kuwanyanyasa viongozi na wanachama wa vyama vya upinzani.

  Pamoja na hayo Wapinzani nao wanahitaji lawama kwa kiasi fulani. Angalia sasa hivi CHADEMA kinavyokatisha tamaa mamilioni ya Watanzania ambao walikuwa wanafikiria kukipigia kura chama hicho katika uchaguzi ujao. Ikiwa imebaki miezi michache kabla ya uchaguzi mkuu ujao badala ya kuhamishia nguvu katika kupanga mikakati ya kampeni zao za 2010 badala yake nguvu zao wamezielekeza katika kufukuzana ndani ya chama na kutoleana maneno ya kashfa hadharani. Hao CUF bara wapo kwa sababu sheria za vyama vingi zinawalazimisha hivyo, vinginevyo wangependa wawe ni chama cha visiwani tu.

  Nchi nyingine kwa utendaji dhaifu wa CCM toka waliposhinda 2005, basi viongozi wengi wa chama hicho wangekuwa wanajiandaa kuhama chama hicho kabla na baada ya uchaguzi wa 2010 kwa kujua kwamba wapika kura watakipiga chini vibaya sana katika uchaguzi ujao, lakini CCM wanajua watatumia vyombo vya dola kuiba, kutoa rushwa, kunyanyasa, kuwatisha Viongozi na wapiga kura wa upinzani na hatimaye kuibuka tena na "ushindi wa kishindo"
   
 10. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #10
  Dec 12, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,372
  Likes Received: 3,136
  Trophy Points: 280
  nasubiri chama kipya cha kitaifa..................naona vilivyopo vyote vinajenga mitandao ya kuchuma cash...cash...cash..tu.
  chama imara cha upinzani kitatoka ccm nacho chaja nami nakisubiri
   
Loading...