CCM haina Makubaliano na Wananchi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM haina Makubaliano na Wananchi!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by SYLLOGIST!, Oct 7, 2009.

 1. SYLLOGIST!

  SYLLOGIST! JF-Expert Member

  #1
  Oct 7, 2009
  Joined: Dec 28, 2007
  Messages: 306
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 45
  Hivi karibuni kumekuwa na matamshi kuhusu CCM na utamaduni wake waku wachagua viongozi wake kwa mihula miwili miwili. Katika kutafakari hayo nilikaa na kujiuliza CCM wana makubaliano na wanachama wake katika chaguzi mbali mbali za viongozi?

  Makubaliano ya wanachama wa CCM na chama chao ndio ridhaa ya Wananchi wote?

  Piga-Ua jibu nililolipata ni hivi 'CCM haina Makubaliano na Wananchi' ya moja kwa moja bali kupitia kwa wanachama wake na hivyo sio lazima, si lazima kuwachagua kwa muhula mwingine....nasema hivi kwa kuwa wanachama wake wengi waliokuwa na makubaliano na chama chao wameingia makubaliano au mikataba mibovu kwa kutuhadaa- endapo watachaguliwa muhula wa pili wataweza kubatilisha hayo makubaliano/mikataba mibovu?

  Nawasilisha
   
 2. M

  Mkandara Verified User

  #2
  Oct 7, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu hata sikuelewi kabisa...
  Nachofahamu mimi ni kwamba CCM haina makubaliano na wananchi isipokuwa wanachama wake. Ni hivyo hivyo ktk vyama vyote wala sii CCM pekee isipokuwa ni wewe mwananchi unayetakiwa kukubaliana na chama kimojawapo ktk upigaji kura wako..Chama kinatoa Ilani, sera na mwongozo wake ambao wewe mwananchi unautazama na kuuchunguza kabla hujaingiza kura yako.

  Ni kweli kabisa kwamba CCM hawataweza kubadilisha kitu ktk mikataba..Leo hii dhabau kwa mara ya kwanza imefikia dollar 1035 kwa Ounce ongezeko kubwa sana ktk GDP yetu lakini mfuko wa Taifa unaambulia ukoko kutokana na mkataba mbaya..Mh. Zitto hawezi kubadilisha kitu zaidi ya kubadilisha vipengele fulani fulani ambavyo haviwezi kuathiri pato la mashirika kama Barricks, isipokuwa katika madini mengineyo kama Copper na kadhalika ambayo pato na mchango wake ni mdogo sana.

  Njia pekee kwetu sisi Watanzania ni kutafuta mgombea Independent, kichaa mmoja kama Chavez ambaye anaweza kubadilisha kila kitu hata kama nchi yetu irudi ktk Ujamaa kwa miaka mitano ijayo. lakini sidhani kama Wadanganyika wanaweza kusimama nyuma ya kiongozi huyo kwa mwaka mmoja tu..Licha ya hivyo sioni chama wala kiongozi yeyote anayeweza kusimama nyuma ya Ujamaa kama itikadi inayoweza kuleta maendeleo.
  Hivyo, swala la mikataba mibovu hilo tusahau!..kwani tumesha UZA nchi. Ukiuza kitu hata iwe nyanya sokoni sidhani kama unaweza kudai kurudishiwa ati makubaliano yalikuwa mabaya!
   
 3. SYLLOGIST!

  SYLLOGIST! JF-Expert Member

  #3
  Oct 7, 2009
  Joined: Dec 28, 2007
  Messages: 306
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 45

  Ahsante Mkandara
   
 4. SYLLOGIST!

  SYLLOGIST! JF-Expert Member

  #4
  Oct 8, 2009
  Joined: Dec 28, 2007
  Messages: 306
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 45
  “


  Utaratibu huu ni wa CCM peke yake-na sio makubaliano na wananchi wengi ambao sasa wamechoshwa nyoyo na bongo zao.

  Waachiane wenyewe huko CCM na siyo kupeana nafasi za uongozi serikalini

  hebu fikiria, baada ya papa anapewa kidagaa naye awe papa kwa mgongo wa kura ya mwananchi?
   
 5. L

  LaVerite Member

  #5
  Oct 8, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Hivi leo mkichagua chadema au cuf kuongoza tz bara hiyo itakuwa serikali au vichekechesho, hata kama ccm hatuitaki lazima kwanza kitokee chama kijijenge kiwe na ukubwa (grassroots support, popular support, na uwingi wa vigogo) kama wa ccm. Hapo tutapata alternative. Mlioko nje mnajua kuwa labour na conservative au republicans na demacrats ni vyama karibu vinavyolingana ukubwa, sio sawa na cmm na chadema au ccm na cuf huku bara.
   
Loading...