Elly B
JF-Expert Member
- Jan 11, 2011
- 1,194
- 906
Ndugu zangu,
Mjumbe mmoja wa Baraza la Wazee la CCM Taifa amependekeza kikaoni Dodoma kuwa dawa kuu ya wapinzani ni kuwaonesha wananchi mafanikio ya chama tawala kwa matendo. Mjumbe huyo ambaye alikuwa Makamu wa CCM Tanzania Bara amesema kuwa wapinzani kama CHADEMA hawatakuwa na la kusema ikiwa wananchi wataona mafanikio yaliyoletwa na CCM kwa macho yao wenyewe....
Binafsi nimeshangazwa sana na wazo hili. Najiuliza ni mafanikio yapi ambayo CCM inaweza kuyaonyesha kwa vitendo mpaka wananchi waelewe?
Hawa watu bana!
Tangu hapo wananchi wa nchi hii walichokuwa wanalilia ni ustawi wao na unafuu wa maisha! Kwani nini jipya hapo? Wananchi wanaomba nini kila siku? Ni yaleyale ya tangu miaka ya 60....Maji, matibabu, barabara, umeme na uthibiti wa bei!
Na tatizo limekuwa ni lipi? Lilelile....Serikali na chama fisadi. Mapato ya taifa kwa asilimia kubwa yanapotelea kwenye mifuko ya watendaji wa serikali binafsi, rushwa imekithiri kila kona , haki imepotea na uhuru unatoweka kwa kasi ya kutatanisha!
Sasa tuongelee kuonyesha mafanikio kwa vitendo!...
Kwamba CCM itaonyesha jinsi ilivyofaulu kuwaibia wananchi kwa kuongeza kodi na bei za mafuta, hivyo kuwasababishia ongezeko kubwa la gharama za maisha??!
au CCm ionyeshe wananchi jinsi inavyochukulia mzaha suala la maendeleo vijijini kiasi kwamba pembejeo hakuna, na zikipatikana zinakuwa kwa uchache na kwa kuchelewa...masoko hakuna na inafikia sehemu hata mazao hayana bei elekezi. Mafanikio yanaextend mpaka mpaka kwenye kuwazuia wananchi wasiuze mazao nje ya nchi ambako kuna maslahi kwao! Yaani masoko ya ndani ovyo bei kila mlanguzi awanyonye anavyojua na nje ya nchi Msiuze. Sawa na kusema wakulima ni haki yao kuwa maskini!
au CCM ionyeshe mafanikio ya kushindwa kusimamia rasilimali zetu mpaka wanyama wanatoroshwa nje ya nchi kupitia viwanja vya ndege vyenye ulinzi masaa yote...au mafanikio katika kuwapa misamaha ya kodi wawekezaji kwenye sekta za madini na utalii hii ikiendana na kuwaachia wamiliki wa makampuni hayo na mahoteli kubadilisha majina kila muda wa kulipa kodi unapofika, sawa na kusema CCM na serikali yake inazidi kufanikiwa katika kupokea rushwa!
au CCM na serikali iwaonyeshe wananchi jinsi ilivyoweza kuwabaini mafisadi, kutangaza vua gamba na hatimaye kufeli jumla katika hilo? kimevuliwa kipi ? mikwara yote nani kashughulikiwa? So mniwie radhi ntakaposema ni sera isiyo rasmi ndani ya CCm kuwalinda wahalifu na wahujumu uchumi nchini!
au labda CCM ionyeshe mafanikio ya serikali yake katika kujiteulia Makandarasi wa kujenga barabara ambazo zimetokea kuwa chini ya kiwango mpaka kufikia kutomaliza mwaka mmoja kabla hazijayeyuka na kubanduka na kisha kuwalipa kwa gharama za juu,..gharama zinazohusisha ukaguzi wa barabara zenyewe......Mafanikio?
au CCM na serikali yake ionyeshe mafanikio ya kutumia Vyombo vya dola kwa maslahi ya kisiasa kuwatishia wapinzani na kuwadhuru wanaoipinga? ni mafanikio ya kuacha watu wafundishwe namna ya kudhuru wenzao kwa mapanga, visu na tindi kali eti kwa sababu tu ni wapinzani au wanaoikosoa serikali? ...au kuwaua waandishi na kuwang'oa kucha na meno huku polisi wakilazimisha kujichunguza ili kupindisha haki na ukweli?
CCM na serikali vionyeshe nini kwa watanzania? Jinsi kulivyopatikana mendeleo ya kutisha kwenye sekta ya elimu huku wanaofeli ni sawa na wanaofaulu( kwamba ukifelei umefaulu na ukifaulu umefaulu)? kwamba ukifanya mtihani na usipofanya unafaulu tuu hata kama umeshindwa kuandika hata jina lako??! ..kwamba kuna shule kibao za kata,walimu, madawati na maabara hakuna? jinsi rushwa hasa za ngono zinavyoamua viwango vya ufaulu wa vyuo vikuu huku wahadhiri wake na wasaidizi wao wakiachiwa uhuru wakusema nani kafaulu na nani kafeli bila kujali ufaulu umepatikanaje?
Ni hivi, CCM haina sauti ya kuonyesha wala kusemea chochote ambacho kitaitwa mafanikio ndani ya nchi. Labda kitu pekee ambacho CCM inawezafanya ni kuwa wakweli kwa wananchi wa Tanzania....Kuwa imewadanganya kwa muda mrefu, imewasababishia adha na madhila kwa muda mrefu na imeshindwa kuongoza, hivyo inaomba radhi kwa wananchi wa Tanzania kwa yote hayo na iahidi kutorudia tena, pia iahidi kuachia nchi haraka sana na kwa amani ili wanaoweza waiendeshe mpaka wao watakapojifunza kuwajibishana bila kuangaliana sura, kuwa WAZALENDO NA WAKWELI, ndiyo warudi kuomba ridhaa ya wanachi wa Tanzania tena. Hapo tutakuwa tunaelekea kuelewana kidogo. Vinginevyo mimi naona "ARI ZAIDI, NGUVU ZAIDI NA KASI YA HATARI KUELEKEA KUZIMU YA HAPAHAPA DUNIANI, KAMA CCM HAITAONDOKA MADARAKANI!
Nisamehewe kama kuna asiyenielewa! Mimi naishi uswazi, wazazi wangu na washkaji wengine wako kijijini na nayaona kwa macho!