Uchaguzi 2020 CCM haikupaswa kutumia nguvu nyingi kupambana na CHADEMA

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
6,273
6,637
Wananchi wanafanya tathmini ya chama kilichopo madarakani kimewafanyia nini, kisha wanatoa majibu.

Wananchi wanafanya tathmini ya chama kinachoomba ridhaa ya kukamata Dola, je kina uwezo huo? Kisha wanatoa majibu.

Kwa maoni yangu, CHADEMA ilishadharauliwa na wananchi kwa kuwa na itikadi ya kupinga maendeleo ya wananchi, wao wanapinga kila kitu, mfano kwa wakazi wa ziwa Nyasa nani atachagua mgombea wa CHADEMA ambae ujenzi wa meli mbili za abiria na mizigo umekuja kuwa mkombozi kwa watu wa eneo hilo?

Kutumia nguvu nyingi na kutumia pesa nyingi kupambana na chama ambacho hakina sifa ya kutawala na kuwaletea maendeleo wananchi ni sawa na kumuua Ngedere kwa SMG.

Kama chama kinakuwa na viongozi ambao walikuwa wanatafuna ruzuku kama vile pesa zao, wakati ni mali ya umma. Je, kulikuwa na haja ya kupambana nacho kwa nguvu kama inayotumika sasa? Hawa walitakiwa waachiwe makatibu wa Ccm wa kata wapambane nao kuliko kutumia nguvu kama ilivyofanyika.


1985616_IMG_20190128_212057.jpg
 
Kwa akili yako kipo hai?
Hata mie Nadhani kwa kweli!! Maana naona ni nyomi mpaka basi kwenye mikutano ya mgombea wao Lissu , naona watu wanakaaa hadi usiku kumsubiri mgombea wao Lissu!!

Mbaya zaidi naiona tume ikiwakata kwa nguvu wagombea wao alafu polisi wakiwakamata na kuwabambikia makesi wagombea wao. Sijui tatizo ni nini?
 
Jiwe Linapiga hadi Magoti kuomba kura.

Mbingu na Ardhi zimemkataa jiwe kwa Unyama wake
 
Back
Top Bottom