CCM Haikumsaidia Samson Kipepe?

Sikonge

JF-Expert Member
Jan 19, 2008
11,537
6,028
WanaJF,
Nilisoma huu ujumbe kutoka FORUM nyingine. Muandishi kama unakuja kusoma humu NAOMBA msamaha kwani sikukuuliza kama naweza kuutumia ila sikufanya hivyo kwa sababu fulani fulani.
Kama ni kweli basi CCM WAPAMBE na Wapiga debe wajue kuwa YAKIWAFIKA watakufa peke yao na labda ni WAPINZANI watakuja kuwajulia hali. Hivyo wawapo jukwaani wajue kuwa WAPINZANI ni ndugu zao kabisa ila kila mtu anagombea KULA ahh, KURA. Ila Matusi yasiwe mazito kama haya yaliyoandikwa hapa chini.Hali zenu,
Samson Kipepe ameungua kwa muda wa miezi miwili, ambapo mauti yake yametokana na ugonjwa wa ini.
Baada ya kugundulikana kuwa ana tatizo hilo, na bila msaada wowote,ililazimu wenyeji wote wa Mbeya waishio Dar, kufanya fundraising kwa ajili ya kwenda kutibiwa India.
Pesa zilipatina za matibabu,kulipia ticketi za watu watatu na pesa ya kuacha nyumbani.
Wiki jana ndio ilikuwa safari ya kwenda India, ghafla hali yake ikabadilika na kulazimika alazwe kwanza Regency Hospital na kama hali yake itarudi kuwa afadhali basi safari ya India iendelee.
Tukiwa tunasubiria hali hiyo, Jumanne ghafla ikawa mbaya sana na akahamishiwa Hospitali ya Lugalo siku ya Jumatatu na Juamatano mauti yakamfika. [Siasa ni mchezo mbaya watu wanasema, wapo wanaoucheza wanashida.

Kipepe alikuwa kada mzuri na shupavu sana wa CCM. Kipepe hakiwa anapigania uhai wake Kitandani hakuna msaada wowote kutoka chama chake alioupata, zaidi ya watu kujikusanya na kutafuta michango.

Wakati akina Makamba wanatumia pesa kibao kwenda kwenye Check up nje ambazo zinaweza kufanywa hata ktk mahospitali yetu, CCM inashindwa kutoa pesa za kuokoa maisha ya kada wake shupavu, ambaye alikuwa akisimama majukwani kukipamba chama chao na huku akiwatukana wapinzani kwa lugha zote anazojua yeye, leo hao CCM wameshindwa kuweka nyuso zao mbele ya Kipepe na wapinzani wakawa wa kwanza kumsaidia Kipepe.
 
Last edited by a moderator:
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom