CCM haihusiki mauaji ya Tarime - Tambwe (Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Propaganda cha CCM) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM haihusiki mauaji ya Tarime - Tambwe (Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Propaganda cha CCM)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jun 1, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jun 1, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Wednesday, 01 June 2011 12:45 newsroom  NA MWANDISHI WETU
  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeelezea kusikitishwa kwakwe na tuhuma zinazotolewa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Tundu Lissu kwamba imehusika katika mauaji ya wananchi katika mgodi wa Nyamongo, Tarime. Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana, ilisema kuwa CCM haihusiki kwa namna yoyote na mauaji hayo na kwamba habari zilizoandikwa na gazeti la Tanzania Daima la Mei 30, mwaka huu, ni uzushi. "Tuhuma hizi ni nzito na za kusikitisha, lakini zinastahili kupuuzwa na wananchi wenye akili timamu, kwani mtoa habari hizo siku zote amekuwa ni mwongo," ilisema taarifa hiyo iliyotiwa saini na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Propaganda cha CCM, Richard Tambwe.

  Tambwe alisema CCM kwa muda mrefu imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha nchi inakuwa na amani na imekuwa ikifanya hivyo kabla CHADEMA haijaanzishwa, lakini ni mambo ya kusikitisha kuona kuwa chama hicho ndicho kimekuwa kikichangia kubomoa hali ya amani na utulivu uliopo.

  Alisema Lissu amekuwa akitumia maneno ya uchochezi kwa sababu za kisiasa kwa nia ya kutaka kuungwa mkono na wananchi.
  Aliliomba Jeshi la Polisi nchini kuendelea kuwatafuta wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine katika tukio la Tarime, wakiwemo viongozi ambao wamekuwa wachochezi.
  Tambwe aliwakumbusha wananchi kuwa serikali iliyopo madarakani imetokana na CCM, ambayo ilishinda baada ya wananchi kuonyesha imani kwa Chama.
   
 2. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #2
  Jun 1, 2011
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Au Hiza Tambwe ambaye hukuzipuuza ukaamua kuzijibu umejiona kuwa huna akili timamu! Maana umetuomba wenye akili timamu tuzipuuze huku wewe hukuzipuuza ukazijibu!

  Tukisema CCM hakuna mtu tutakuwa tunakosea kweli!

  Je walipooua kule Pemba walikuwa Chadema ndio waliolianzisha! Mbona Tambwe uliwalaumu CCM walipoua Pemba!
  Kweli CCM Wanatunza amani mpaka Chadema walipokuja ndipo wakaanza kuua!

   
 3. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #3
  Jun 1, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Mwananchi mwenye akili timamu anajua kuwa vyombo vya dola (serikali) vimeshiriki katika mauaji ya wananchi Tarime. Vilevile, mwananchi mwenye akili timamu anatambua kuwa serikali hiyo inaongozwa na ccm. Hivyo basi, mwanachi mwenye akili timamu anaweza kuunganisha na kujua kuwa serikali ya ccm ndiyo iliyofanya hayo mauaji. Tambwe amesema mwenyewe, "...serikali iliyopo madarakani imetokana na CCM, ambayo ilishinda baada ya wananchi kuonyesha imani kwa Chama..."
   
 4. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #4
  Jun 1, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Sina uhakika na hapo
   
 5. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #5
  Jun 1, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,635
  Trophy Points: 280
  Duh nilidhani Tambwe kaondoka na Mzee Makamba kumbe bado yupo CCM kweli imefilisika.
   
 6. Dr wa ukweli

  Dr wa ukweli JF-Expert Member

  #6
  Jun 1, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 892
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  tambwe kumbe hukujivua gamba na mumeo Makamda?
   
 7. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #7
  Jun 1, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,849
  Likes Received: 474
  Trophy Points: 180
  Muulizeni kama alishamshughulikia mama yake mzazi, aliahidi atafanya hivyo kabla ya kurudi CCM.
   
 8. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #8
  Jun 1, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Lissu huyu si amefukuzwa nyamongo mpaka kesi iishe? nadhani amechanganyikiwa kwani nasikia polisi walimfanya kitu mbaya sana huyu
   
 9. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #9
  Jun 1, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Huna akili Timamu!
   
 10. L

  LAT JF-Expert Member

  #10
  Jun 1, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  Habari za Abbottabbad .... umeponea chupuchupu ..... !
   
 11. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #11
  Jun 1, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Na mwananchi mwenye akili timamu anajua kabisa kuwa CDM ndio walio chochea mauaji na kisha kujinufaisha kisiasa kwa kujitafutia umaarufu kwenye maiti
   
 12. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #12
  Jun 1, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Lissu hawezi kuwaambia ukweli ila polisi walimfanya kitu mbaya huyu nyie acheni walimwingizia vidole m*u*d*n*
   
 13. G

  Galula Jr Member

  #13
  Jun 1, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  AKILI YAKO HAINA AKILI, wewe ni TAMBWE na kajivue gamba haraka
   
 14. G

  Galula Jr Member

  #14
  Jun 1, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Na wewe uko hapa unajiita great thinker kabisa?????????????????
   
 15. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #15
  Jun 1, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Mkuu ongea mambo ya maana ya kuwasaidia watanzania waondokane na umaskini na sio habari hizi za kiajabu ambazo hata mtoto mdogo hawezi kuongea
   
 16. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #16
  Jun 1, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,704
  Trophy Points: 280
 17. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #17
  Jun 1, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Mkuu unapoteza maana nzima ya kuchangia hii post maana aliyeitoa ni mtu wa kwako huko bado unaingiza mambo ya kijinga na kipuuzi mpaka inakosa maana
   
 18. Raimundo

  Raimundo JF-Expert Member

  #18
  Jun 1, 2011
  Joined: May 23, 2009
  Messages: 13,552
  Likes Received: 10,940
  Trophy Points: 280
  Mfa maji haachi kutapatapa, nasubiri tamko la mrembo (handsome) wa nchi.
   
 19. D

  Domo Zege JF-Expert Member

  #19
  Jun 1, 2011
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Join Date : 3rd November 2010
  Posts : 1,260
  Thanks0Thanked 66 Times in 49 Posts

  Rep Power : 23

  Mkuu heshima mbele, yani umenifurahisha kweli umefikisha post 1,260 bila hata watu kukugongea ka thanks,unaonesha jinsi gani post zako hazina mshiko kama maelezo yako hapo juu ni balaa.
   
 20. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #20
  Jun 1, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Mkuu sikuliona hilo bora hata nisingehangaika kumjibu
   
Loading...