Kwa wafuatiliaji wazuri wa JF watakubaliana na kuwa katika mtandao wetu huu pendwa hasa katika masuala ya siasa, wengi wetu tukiona ID ya mtu hata kabla ya kuangalia alichoandika uanajua moja kwa moja huyu ni mpenzi wa chama gani kati ya CCM na CHADEMA. Katika uchunguzi wangu nimegundua wapenzi wengi wa CCM humu hawapo Consistency (hawana kumbukumbu) wa wanayochangia kwenye mada zao mara nyingi hujichanganya kati ya yale waliondika kabla na michango yao ya mbeleni, mfano vijana wengi wa Lumumba nyuzi zao za nyuma waliaandika sana CHADEMA kuwa haina ubavu wa kumfukuza Zitto, cha kushangaza watu walewale badala kusimamia haja hiyo wamesahau kusimamia hoja yao kama vile hawajawahi kuandika hivyo. Hi ni tofauti na wapenzi wa CHADEMA ambao wanakumbukumbu na mada zao kabla na baada hazipingani. Wapenzi wengi humu wa CHADEMA wako analytical wanaongoza kwa mada za kufikirisha tofauti na mahasimu wao mada zao nyingi utasikia chama cha wachaga, mzinzi, aliiba sadaka, hana elimu. Kwa msingi huu usipate tabu kujua ni chama gani kinakufa tazama michango ya wapenzi wao hapa hapa JF.