CCM: Flagyl Haitibu Malaria kamwe, bado Mtaendelea kuumwa mwisho Mtadai Mmerogwa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM: Flagyl Haitibu Malaria kamwe, bado Mtaendelea kuumwa mwisho Mtadai Mmerogwa!

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Arafat, Apr 12, 2011.

 1. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #1
  Apr 12, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  CCM Mnatia uzuni kila mkiibuka na matamko yenu na maoni yenu juu ya matatizo na mstakabali wa Chama chenu Kikongwe kabisa hapa Africa Mashariki.

  Kama ningekuwa mwanazuoni katika kada ya Sayansi ya Jamii na Siasa ninge fanya tafiti kujua iwapo chama cha siasa pia kinaweza kuzeeka na kuwa kikukuu na hivyo kuchoka kama binadamu, kukosa nguvu, kupungua uwezo wa kufikiri, kudhoofika mifupa na hata kufa kifo cha asili kama binadamu, hili ni eneo la changamoto kwa "Case study ya CCM".

  CCM walipo kuwa Dodoma Juzi na Jana wameibuka na mambo ambayo kwangu mimi naona kama kutokana na umri wa chama hicho labda hawana tena uwezo wa kutambua na pengine wamechoka naona kama kuchoka kwao kuna shabiana na umri wao hivyo wamedhoofika mfumo wa ufahamu. Waliposema wanajivua magamba neno hilo lilitafsiriwa na Watanzania kwa maana yake halisi na kusubiri kwa hamu CCM kujivua magamba lakini kumbe hata hawajui ni magamba gani waliyo nayo amabayo yanatisha Jamii na Watanzania wote kwa ujumla, nimeshangaa sana kuona kuwa RA, EL, Dowans, Richmond, IPTL, Ufisadi, Mchakato mbovu wa Katiba, Uteuzi mbovu wa Viongozi wa kisiasa na Watendaji, Ukosefu wa sera za kukuza uchumi na kutoa ajira kwa vijana, Shule duni na elimu duni katika shule za kata, n.k. siyo sehemu ya magamba ya CCM.

  Nimeshangaa kuona kuwa CCM haina ufahamu kuwa Mukama ni mstaafu mwenye miaka takribani 60 hivyo hawezi kuwa gamba jipya! Nimesikitika sana kuona kuwa safari nyingine tena CCM bado inashindwa kusumbua akili zao kujua majibu ya matatizo yanayokera jamii na kuperekea Umma kuichoka Serikali ya CCM, nimechoka zaidi kusikia Kikwete hajui kuwa mswada wa mchakato wa katiba mpya haikubaliki kwa kila Mtanzania yeyote mwenye akili timamu na kuwa CCM inajiandaa kuinadi nchni nzima!

  Inashangaza kuona kuwa vikao vyote vya CCM Dodoma havikuwa na tija yoyote kwa maslahi ya Chama hicho na Serikali kwa ujumla ingawa wao wote hawajui na pia hawaoni hilo! Nilitegemea Kikwete awaombe Watanzania samahani kwa kuwadanganya katika sherehe za kilele cha kuzaliwa kwa CCM kuwa hawajui wamiliki wa Dowans ili kujenga heshima yake binafsi na Chama chake hivyo kuonyesha njia ya kujivua gamba badala yake safari hii wameibuka na Mpya kuwa JF ni mali ya CDM na hipo kwa ajili ya kuibomoa CCM! Napata hisia kuwa CCM imezeeka na kupoteza ufahamu maana wamesahau Kikwete alipo waadaha watanzania 2005 kuwa yeye ni JK (Julius Kambarage) mpya kafufuka kuliperekea JF kujaa mada lukuki za kumnadi Kikwete na kumpigia kampeni, kuwa CCM hawawezi kutambua kuwa Watanzani wanahitaji Rais/Chama hasiye waogopa Mafisadi, wauza madawa ya kulevya, Majambazi, Wahujumu Uchumi na wala hawataki Rais/chama mwenye ushirikiano na watu kama hao.

  Kwakuwa CCM wamekaa Dodoma kwa kauri mbiu ya kujivua magamba, kwa maana ya kujisahisha lakini hawakuweza kuona mambo muhimu yanayo litafuna taifa ambayo yamepereka CCM kukosa mvuto mimi naona kama CCM wame meza Flagyl kutibu Malaria, hawata pona, 2015 watasema wamerogwa!

  Alamsiki,

  Sikio la kufa halisikii dawa.
   
 2. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #2
  Apr 13, 2011
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,180
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  CCM wanawashwa?
   
 3. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #3
  Apr 13, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  mkuu, Flagyl ni dawa nzuri kwa anayeharisha...........!!!!!!!!!!!!!!
   
 4. A

  Anyambilile Member

  #4
  Apr 13, 2011
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakuunga mkono mkuu, wamejsahau sana badala ya kudeal na matatizo ya wananchi wao wanabadilishana madaraka kwao hii si salama kama wanavyofikiri
   
 5. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #5
  Apr 13, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Mkuu kwanini wana kunywa dawa ya kuharisha wakati wanaumwa Malaria!!
   
 6. d

  damn JF-Expert Member

  #6
  May 2, 2011
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 585
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  nadhani wanaharisha maana tumbo la kuhara likikushika unaweza ukamwaga hata hadharani. Si unaona UVCCM wanavyomwaga mbele ya vyombo vya habari? hiyo si malaria ni kuhara
   
Loading...