CCM endeleni kujidanganya mmesahau kabla 2015 mlikuwa mnazomewa na sare zenu za kijani!

sambulugu

JF-Expert Member
Jun 1, 2021
3,906
7,169
Serikali hii iliingia kwa mbwembwe mara chanjo ikadunda! Mara kufungua nchi na safari kibao lakini hamna la maana linaloonekana kwenye maisha halisi!

Kurudisha wezi na wababaishaji kama akina Makamba! Mara Royal tour ujinga huu wa ajabu kabisa usio na tija kwa taifa letu!

Bila kujipanga kutatua Shida za wanchi kama mambo ya umeme,maji, mbole nk Kwenye korosho mmeboronga kweli kweli ni uppuzi mtupu mlimsema sana JPM lakini mkasau wanaowaibia wakulima ni wanasiasa!

Bashiru kashauri mnalalama eti anamkosoa Rais inamaana wasikosolewe mbona kipimdi cha Magufuli akina Mbowe na Zitto kila mda walikiwa wanaitisha press conference lakino baada ya kupata kibuyu cha asali walo kimya!

Sasa kwenye uchaguzi wenu eti mwenyekiti anatengeneza team ya 2025 na ndo maana anachagua tu watu wasio na sifa ngoja liende!

Etu wanaojibu hoja za Bashiru ni Kibajaji na Musukuma wote hawa ni vichwa maji wasiojitambua! Hivi CCM hamuoni kuwa mahangaiko ya wan achi huu ya maji na umeme hamuyaoni mnashupaza shingo eti?

Magufuli aliwakera sana na sasa amekuja wa kuwaachia mlambe asali!

Namba tukutane 2025 na mugombea wenu Samia! I tell you are going to fail ile mbaya! Na bahati yenu hata hawa CHADEMA hawana mtu makini wana vilaza tu kama akina Tundu Lisu!
 
Siasa za ccm ndo hizi za kuwapumbaza wanachi, saiv kuna mgao mkubwa wa umeme tunaletewa hoja za kupumbaza

Bahati mbaya na upinzani wanaingizwaga cha kike wanatlowa kwenye reli wakifikili ccm wako siliazi,
Hapo siyo ajabu bashiru akavuliwa uanachama na upinzani wakafanya mapokezi makubwa na kumpa nafasi za kugombea nafasi za juu na uongozi wa juu

Tuna nchi ya ajabu sana
 
Mkuu, sikio la kufa halisikii dawa. CCM kupitia makada wake wananeemeka na kugawana vyeo huku kila mtu akila kutokana na urefu wa kamba yake.

Hawahangaishwi na uhalisia wa baadhi ya vyeo huhitaji uzoefu, stadi, mafumzo, elimu utaalamu, weledi na maarifa. Wao kwao kuwa mwenzetu ama mtu kegezo kikuu cha kugawana na kujimilikisha vyeo, maliasili, na utajiri wa taifa letu.

Kauli ya Dkt. Bashiru imewashtusha sana kwa kuwa hawakuitarajia kutoka kwa mtu wa kariba yake. Hawakutegemea kauli yake ya kutaka kuwaamsha wenye nchi, ambao wao wamewabatiza kwa jina la "wanyonge" huku wao wakiwa wanyongaji wenyewe.

Tunapoelekea 2024 - 25 pengine ile kauli wa Mwl. Nyerere itatimia. Kauli kuwa chama halisi na cha kweli cha upunzani kitatoka ndani ya CCM yenyewe.

Falsafa ya jumla ya JPM ya kiujamaa imezindua akili ya watu wengi, na inaonekana ni dhahiri yenye manufaa kwa watu waliokuwa wengi, ukiondolea mbali "elements" za udikteta alizokuwa nao. Falsafa ya JK ni ya kibwanyenye, hazikubaliki kwa sasa hata ndani ya CCM yenyewe, kwa kuwa ni yenye kutaka kupora mali za taifa, kumilikisha na kufaidisha watu wachache.

Mabwanyenye sasa wameshika chama, na wanataka kuwaengua wajamaa wote ndani ya chama. Wanawataka ama watoe utiifu au wakae kimya na kufyata mikia yao chini.

Uhasimu wa falsafa hizi mbili ambazo zimepelekea kuwapo kwa kambi kuu mbili, zisipo thibitiwa mapema, hakika zitakuja kukigawa chama hiki.

Kauli ya KM Taifa inataupa tafakari kubwa, pale anaposema kuwa baadhi ya makada ndani ya CCM ni kama mifugo iliyofungwa kamba isizirure. Kama kutoa maoni binafsi hata kama ni kwa njia ya kukosoa imegeuka sasa kuwa ni kosa ndani ya CCM, basi sasa kila kada itampasa kusifu na kuabudu tu mbele ya Mwenyekiti Taifa.
 
Back
Top Bottom