CCM endeleeni kutumia dola vizuri ili muendelee kuwatumikia watanzania na kuwaletea maendeleo

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
6,273
6,637
Kwanza natoa pongezi kwa chama cha CCM kwa kazi nzuri ambayo kimekuwa kikiifanya tangu kilipokadhiwa kukamata dola. Ccm imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha inawatumikia watanzania na kuwaletea maendekeo.

Kila Mtanzania ni shahidi maana karibu kila sekta imeimarishwa na imekuwa imara. Miundombinu, elimu, afya , ulinzi na
salama wa raia na mali zao.

Hii ni kwa sababu Ccm imekuwa ikitumia dola vizuri kwa manufaa ya taifa letu. Tumeona jinsi polisi wanavyopambana na uhalifu kila siku. Na sasa takwimu za unyag'anyi wa kutumia siraha zimepungua hii ni kwa sababu serikali ya CCM inajali usalama wa raia wake na mali zao na imeimarisha jeshi la polisi.

Pia tumeona Takukuru jinsi wanavyopambana na rushwa na ubadhirifu na hii kuzuia wizi wa pesa na mali za umma na sasa miradi mingi imetekelezwa kwa muda mfupi sabau Serikali imeweza kuwa na pesa za kutekeleza miradi hiyo. Pia, kwa upande wa ulinzi wa mipaka yetu tumeona jinsi jeshi letu linavyoilinda na Watanzania wanaishi bila hofu ya kuvamiwa na adui yoyote.

Hivyo CCM iendelee kutumia dola kwa manufaa ya taifa letu ili iweze kubaki madarakani maana ndio chama pekee kinachowajali Watanzania. Sio kama vibaraka wa mabeberu ambao sidhani wanaweza kutumia dola vizuri kama CCM.
 
Uliosema yana harufu ya ukweli ispokuwa kwenye hofu embu jaribu kufafanua vizuri maana hapa mm nina hofu nikijaribu kuchambua maelezo yako naweza kujikuta sehemu ya mateso.
 
Uliosema yana harufu ya ukweli ispokuwa kwenye hofu embu jaribu kufafanua vizuri maana hapa mm nina hofu nikijaribu kuchambua maelezo yako naweza kujikuta sehemu ya mateso
Unahofu ya nini? Kama ni msongo wa mawazo nenda ukanywe valium.
 
Sku CCM ikitoka madarakan watanzania tutaisoma namba Sana walah hasa upande wa Aman
 
We utakosa amani ?izo ni fikra mfu
aliekwambia Ccm ikitoka madarakani
Basi mifumo yote ya nchi ina colapse nani
Ccm ni chama sio nchi , ni kama dini kwa
mba unaweza kua dini yoyote ili hali
ukijua mungu yupo na hawezi badilika
kisa umeamua kua mfuasi wa imani
nyingine
 
Hata kuandika hujui aise hivi nyie ndio chama kinawapa kabisa buku Saba kwa upuuzi huo au usukuma umekubeba?shenzi kabisa huna Griefs n nchi hii zaidi ya kutafuta uteuzi wa viti maalumu
Buku saba ndio nini? We ni useless.
 
We utakosa amani ?izo ni fikra mfu
aliekwambia Ccm ikitoka madarakani
Basi mifumo yote ya nchi ina colapse nani
Ccm ni chama sio nchi , ni kama dini kwa
mba unaweza kua dini yoyote ili hali
ukijua mungu yupo na hawezi badilika
kisa umeamua kua mfuasi wa imani
nyingine
Kama isingetumia dola vizuri amani ingekuwepo. Watu wangekatana mapanga hovyo. Majambazi wagepora watu mchana kweupe. Tumia akili wewe kamanda.
 
Kwanza natoa pongezi kwa chama cha CCM kwa kazi nzuri ambayo kimekuwa kikiifanya tangu kilipokadhiwa kukamata dola. Ccm imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha inawatumikia watanzania na kuwaletea maendekeo.

Kila Mtanzania ni shahidi maana karibu kila sekta imeimarishwa na imekuwa imara. Miundombinu, elimu, afya , ulinzi na
salama wa raia na mali zao.

Hii ni kwa sababu Ccm imekuwa ikitumia dola vizuri kwa manufaa ya taifa letu. Tumeona jinsi polisi wanavyopambana na uhalifu kila siku. Na sasa takwimu za unyag'anyi wa kutumia siraha zimepungua hii ni kwa sababu serikali ya CCM inajali usalama wa raia wake na mali zao na imeimarisha jeshi la polisi.

Pia tumeona Takukuru jinsi wanavyopambana na rushwa na ubadhirifu na hii kuzuia wizi wa pesa na mali za umma na sasa miradi mingi imetekelezwa kwa muda mfupi sabau Serikali imeweza kuwa na pesa za kutekeleza miradi hiyo. Pia, kwa upande wa ulinzi wa mipaka yetu tumeona jinsi jeshi letu linavyoilinda na Watanzania wanaishi bila hofu ya kuvamiwa na adui yoyote.

Hivyo CCM iendelee kutumia dola kwa manufaa ya taifa letu ili iweze kubaki madarakani maana ndio chama pekee kinachowajali Watanzania. Sio kama vibaraka wa mabeberu ambao sidhani wanaweza kutumia dola vizuri kama CCM.

Hapo unaona ndio umetupoteza maboya kuhusu matumizi ya vyombo vya dola. Ule ujinga alioongea Bashiru Ally unadhani hatukuufahama, basi hapa unaona ndio umefafanua kumbe ni upuuzi mtupu. Ni hivi, ccm inatumia vyombo vya dola kufanya uhayawani na ukatili wa wazi ili kunajisi box la kura, hilo halihitaji degree kulitambua. Huo ufafanuzi wa eti kutumia dola ulioutoa ili kubadilisha mantiki, kawape watu wa vijijini wasiojua lolote.
 
Kama isingetumia dola vizuri amani ingekuwepo. Watu wangekatana mapanga hovyo. Majambazi wagepora watu mchana kweupe. Tumia akili wewe kamanda.

Kwa taarifa yako hivyo vyombo vya dola ndio vinavyotumika kuficha maovu ya watawala dhidi ya wakosoaji wao. Mfano lile Kundi lenu la watu wasiojulikana, linalindwa na hivyo vyombo vya dola katika kufanya unyama wao fullstop.
 
Naomba ushahidi wa vyombo vya dola kunajisi box la kura. Zaidi ya kufanya kazi zao.
 
Amna lolote chama chochote kinaweza ongoza hii nchi wote ni wa Tanzania...hivo iwe ccm madarakani au chama chchte kile naona ni sawa tu....
 
Kama watu wanaanza kula ruzuku mil 360 na kulipa madeni hewa. Itakuwaje wakipewa nchi?
 
Naomba ushahidi wa vyombo vya dola kunajisi box la kura. Zaidi ya kufanya kazi zao.

Unaomba ushahidi ww kama nani, unadhani ule uhayawani na ukatili wa wazi unaofanywa nyakati mbalimbali dhidi ya wapinzani, hasa hasa wakati wa uchaguzi huwa hatuoni? Au kwakuwa hivyo hivyo vyombo vya dola ndio hutumika kudhibitisha uchafu wao, ndio tutakuwa hatujui kile kinachofanyika dhidi ya wapinzani?

Kwa macho yangu nimeshuhudia kwenye chaguzi mbalimbali za marudio vijana wa ccm wakiwapiga na kuwaachia vilema wapiga kura wa upinzani, tena polisi wakiwa hatua chache ili kuwapa backup vijana hao wa ccm iwapo watazidiwa. Nimeona kwa macho yangu mgombea mmoja wa upinzani akipigwa vibaya sana na vijana wa ccm, huku polisi wakilinda unyama huo ufanyike, kisha mgombea yule wa upinzani ndio akafunguliwa mashitaka na jeshi la polisi kwa kuleta fujo kwenye uchaguzi! Ushenzi huu unafanyika mbele ya macho ya wananchi, na wananchi wananyamaza kwa hofu, kwani polisi ndio wasimamizi wa ukatili huo. Huo ushenzi ndio umekuwa ukifanyika mara zote ili kuipa ccm ushindi, kisha ccm inajitokeza kushangilia kwa mbwembwe kuwa inakubalika, lakini zaidi ya nusu ya ushindi wa ccm hupatikana kwa njia hii. Na inapotokea watu kuhoji hubambikiwa kesi, wakati mwingine kuuwawa. Na mataifa ya nje yakihoji uchafu huo ccm husema sisi ni nchi huru, na tuna namna yetu ya kutatua changamoto zetu. Tabia imekuwa ni hii hii miaka yote. Na niwasihi wapinzani, kama hawatatumia mbinu ya jino kwa jino na kuleta machafuko, hiki chama kikongwe kitaendelea kukaa madarakani kwa hizi mbinu chafu zinazohusisha vyombo vya dola.
 
Kama watu wanaanza kula ruzuku mil 360 na kulipa madeni hewa. Itakuwaje wakipewa nchi?
aliekula 360 si ni mtu tu au kikundi cha watu, kwani Kuna chama kimoja tu nje ya ccm.....mbona hata ccm tangu wawe madarakani mpaka leo ndio wanaoongoza kutafuna hela za umma sembuse Hawa ambao hata awajaapa mbele ya msafu
 
Kama isingetumia dola vizuri amani ingekuwepo. Watu wangekatana mapanga hovyo. Majambazi wagepora watu mchana kweupe. Tumia akili wewe kamanda.
Mkuu so aliekwambia kwamba chama
Kingine kikiwa madarakani nje ya ccm
vyombo vya ulinzi havifanyi kazi yake nani
? Tanzania kama inchi chama chochote
Kikikamata dola mifumo lazima iendelee
kama kawa.
 
Kwa taarifa yako hivyo vyombo vya dola ndio vinavyotumika kuficha maovu ya watawala dhidi ya wakosoaji wao. Mfano lile Kundi lenu la watu wasiojulikana, linalindwa na hivyo vyombo vya dola katika kufanya unyama wao fullstop.
Mh..
 
Mkuu so aliekwambia kwamba chama
Kingine kikiwa madarakani nje ya ccm
vyombo vya ulinzi havifanyi kazi yake nani
? Tanzania kama inchi chama chochote
Kikikamata dola mifumo lazima iendelee
kama kawa.
Tofautisha kufanya kazi yake na kutumiwa vibaya. Kuna nchi watawala wanatumia vyombo vya dola kuiba mali za umma. Lakini hapa wewe mwenyewe unaona.
 
Back
Top Bottom