CCM: Elimu bure HAIWEZEKANI! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM: Elimu bure HAIWEZEKANI!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by jaxonwaziri, Oct 27, 2010.

 1. jaxonwaziri

  jaxonwaziri JF-Expert Member

  #1
  Oct 27, 2010
  Joined: Feb 17, 2010
  Messages: 378
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 45
  Hawa jamaa wameanza kuchanganyikiwa, angalia yafuatayo:

  Kinana: Elimu Bure haiwezekani
  Kikwete: Elimu Bure haiwezekani
  Prof. Magembe: Elimu bure ni sera ya CCM, wanafunzi wakimaliza darasa la saba wooote watakwenda sekondari bila kufanyiwa mchujo(a.k.a kufanya mtihani)

  My Take: Hawa jamaa wana nia ya dhati kwa maendeleo ya Taifa? Hawa jamaa wana nia ya dhati kuimarisha elimu yetu ili iwe "ELIMU BORA" na wala si "BORA ELIMU"?

  CHONDE CHONDE WATANZANIA TUKAPIGE KURA JUMAPILI 31ST OCTOBER 2010 TUUONDOE UDHALIMU HUU WA CCM NA MASWAHIBA WAKE

  TUMCHAGUE DR SLAA KWA WINGI KUWA RAIS WETU KWA MIAKA MITANO IJAYO!
   
 2. kiraia

  kiraia JF Gold Member

  #2
  Oct 27, 2010
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 1,614
  Likes Received: 268
  Trophy Points: 180
  Ndio wanafuata maagizo ya Dr. Slaa kama kawaida
   
 3. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #3
  Oct 27, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  achana nao hao wajinga

  huyu magembe ndo bogaz kabisa yaani basi tu
   
 4. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #4
  Oct 27, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Hivi mnajua kuwa maghembe ana nyumba yake ndogo ambayo alianza naye uhusiano tangu binti akiwa primary??? ni kule shighatini, alimzalisha kabla hajamaliza shule. just miaka saba iliyopita. na maghembe amemjengea na amemhalalishia unyumba ndogo kwa kila kitu.
  Huyo binti ni sawa na mjkuu wake.

  Ndo maana maghembe hana uchungu na elimu ya tanzania
   
 5. WiseLady

  WiseLady JF-Expert Member

  #5
  Oct 27, 2010
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 3,248
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
   
 6. T

  The King JF-Expert Member

  #6
  Oct 27, 2010
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 357
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Elimu bure inawezekana kabisa kama tukiwa na serikali inayojali Watanzania. ufisadi ukidhibitiwa wawekezaji wakilipa kodi na royalties zinazostahili, Serikali ikiachana na matumizi ya anasa basi tutaweza kabisa kutoa ELIMU BURE tena ya hali ya juu. Penye nia pana njia. Mpigie kura Dr Slaa na Wabunge wa Chadema.
  :peace:
   
 7. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #7
  Oct 27, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,947
  Likes Received: 2,093
  Trophy Points: 280
  Wanajali namba kuliko ubora. Basi hata kwenye ajira kutakuwa hakuna interview. Lakini mtaji wa CCM ni ujinga, na anachosema Maghembe ndio capital yenyewe hiyo.

  Kwa kifupi Prof. Maghembe kifikra kwa elimu bure amehamia Chadema na kwa upande wa kufuta mitihani bado yuko CCM. National Examinations Council ya nini basi?
   
 8. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #8
  Oct 27, 2010
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,214
  Likes Received: 316
  Trophy Points: 180
  Ni kweli kabisa kwamba chini ya serikali ya CCM Elimu Bure haiwezekani, kwani wanatumia fedha vibaya. Serikali ikitumia fedha vizuri basi huwa zinatosha kwa Elimu bure.

  (1) Tanzania ilikuwa na Elimu Bure miaka ya nyuma.

  (2) Kenya na Burundi zina Elimu Bure sasa. Na serikali za nchi mbili hizi haziruhusu ununuaji wa magari makubwa ya kifahari kwa ajili ya serikali.

  Serikali ya CCM ambayo inapiga rangi Ikulu kwa bilioni 29, inatengeneza nyumba ya Gavana wa Benki Kuu kwa bilioni 3 (tena huku akiwa na nyumba nzuri tu), inachimba vyoo Bagamoyo kwa bilioni 3, inampangishia Spika nyumba kwa dola 8,000 kwa mwezi (huku akiwa na nyumba nzuri tu nyingine) na inakumbatia viongozi wanaopokea "vijisenti" ili waruhusu ununuzi wa mali ya dola milioni 12 kwa malipo ya dola milioni 40, haiwezi katu kusomesha Watanzania bure.

  Tukitaka Elimu Bure tutaipata, lakini itabidi tubadilishe chama tawala kwanza.
   
 9. T

  The King JF-Expert Member

  #9
  Oct 27, 2010
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 357
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Samehe la kodi tu kwa mwaka ni karibu shilingi Trilioni moja (734 billioni)
   
 10. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #10
  Oct 27, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Hahahahha form four hakuna mtihani!?????? Hiii tamu eeeeh
   
 11. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #11
  Oct 27, 2010
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Mbona chedema wametuambia inawezekana?
   
 12. Tonge

  Tonge JF-Expert Member

  #12
  Oct 27, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 696
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hawa jamaaa JK, KINANA NA MAGHEMBE ni kama mabendera fulani hivi, kazi yao kujichanganya na kulipinga kila jambo analosema Dr Slaa (RAIS), sielewi hii ni serikali ya CCM kila kitu hakiwezekani maana wao akili zao ni MGANDO na hawako makini kwa kila jambo. CCM sera yake muhimu ni Tanzania bila Rushwa na Ufisadi Haiwezekani.Jama tunahitaji mabadiliko, tujitokeze tarehe 31 ili tumchague Dr Slaa atuletee mabadiliko.
   
 13. cabhatica

  cabhatica JF-Expert Member

  #13
  Oct 27, 2010
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 1,074
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Anayosema Maghembe yananichanganya. Kwanza yeye anaomba kura kuwa mbunge wakati huohuo anaongea kama waziri!!!!!!!!!!!!! Kazi mojawapo ya mbunge ni kuibana serikali (waziri). Huyu prof nadhani hata hajui kazi ya mbunge. Nina mashaka na huo uprof wake. Impossible!!
  Kuna viongozi ambao wakishatoka madarakani wanatakiwa kucharazwa bakora.:doh::bowl:
   
 14. j

  jotamini Member

  #14
  Oct 27, 2010
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Kwa CCM Elimu na Matibabu bure haviwezekani kwa sababu wamefungwa kwenye hila ya kupora na hao mafisadi. Hivyo hawako tayari kutupa wananchi matunda ya rasilimali zetu, mafisadi wameikaba koo haiwezi kufurukuta, inabidi tuiokoe CCM kwa kuiondoa madarakani. Iweje fisadi agharamie uchaguzi, muafaka, awagharamie waajiriwa wake kugombea, nk. na atafanya hivyo mpaka mabilioni ya wananchi aliyopora yaishe? Tutasubiri karne ngapi kabla ya kujikomboa? Vinginevyo ina maana atakuwa anatuchagulia maraisi na baadhi ya wabunge kwa muda mrefu sana. Na anayemlipa mpiga zeze ndie anayechagua wimbo sivyo? Tuchague kujikomboa 31 October.
   
 15. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #15
  Oct 27, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,071
  Likes Received: 338
  Trophy Points: 180
  msiwasikilize hao hawajitambui,mabogas wanadai elimu bure haiwezekani lakini ufisadi unawezekana,maghembe nae ameshazeeka bora arudi huko upareni akapumzike na mama watoto tumemchoka na habari zake za blaablaaa
   
 16. F

  Froida JF-Expert Member

  #16
  Oct 27, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,903
  Likes Received: 1,330
  Trophy Points: 280
  Mbona waziri wa viwanda aliamrisha nondo zipungue bei ha ha ha ila strategist wa CCm ni sipukupuku kweli hana akili kabisa katika kipindi hiki cha kampeni wanathibitisha kwamba ni waongo hovyo kabisa
   
 17. GFM

  GFM JF-Expert Member

  #17
  Oct 27, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 708
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  hawana dira hawa. kila mmoja anakurupuka tu
   
Loading...