VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,802
Huku kikiwekwa roho juu na harakati za CHADEMA kujiimarisha hadi vijijini,CCM imeapa 'kula sahani moja' na Dr. Slaa,Katibu Mkuu wa CHADEMA. Vikao mbalimbali vya kimkakati ndani ya CCM vimeapa kumweka 'busy' Dr. Slaa kwa hoja za majibizano ili kumpunguza kasi ya kiutendaji ndani ya chama. ' Utulivu na kuimarika kwa chama ni uongozi hasa Katibu Mkuu. Hoja ziwe ni kadi za CCM,Zitto na Urais na nyinginezo. Hizi zitatusaidia. Dr. Slaa lazima atatingwa nazo tu' alisema Mjumbe wa CC kwenye kikao ambacho hata Nape Nnauye alikuwepo jana.