Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,884
- 6,885
Mfumo wa utawala wa kidemokrasia unatofautiana mno na mfumo wa utawala wa kijeshi au unaoongozwa na wenye kujengeka na wenye kasumba za kijeshi. Siasa ni mfumo wa demokrasi unaowaruhusu watu kuamua wanavyotaka kwa utaratibu wa wengi wape. Jeshi ni kuamrisha tu na waliopewa amri ni kutekeleza wanayoamriwa bila argument.
Kinachoitesa CCM sasa hivi ni jukwaa lao kujaa na waandamizi wa kijeshi. Tunachoshuhudia matokeo yake ya mfumo wa kijeshi ndani ya nchi ya kidemokrasia. Na walio ndani ya CCM ambao wanatumia haki yao ya kikatiba katika kutoa maoni yao wanapingwa vikali kwa kuwa wanapambana na mfumo usiofanya kazi kwa uwazi, ila amri na kufuata utekelezaji.
Akina Makamba, Chilingati, na Mwenyekiti wao ni Wanajeshi, kwa utaratibu wa jeshi waliolelewa ni utekelezaji wa maagizo wanayopewa na wa juu na katika jeshi hakuna meza ya majadiliao ila meza tu ya kupanga mikakati ya utekelezaji wa amri toka mamlaka husika.