CCM Dodoma: Hakuna haja ya Katiba Mpya Tanzania kwa sasa, Katiba ya Mwaka 1977 bado inafaa

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
6,273
6,637
Mkanwa.jpg

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma, Godwin Mkanwa​

HALMASHAURI Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma, imesema hakuna haja ya kuwa na Katiba Mpya kwa sasa kwa kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 bado inafaa.

Kimesema katiba hiyo imewezesha kufanyika kwa mabadiliko ya uongozi wa juu serikali, Rais Samia Suluhu Hassan, akishika madaraka bila kuwapo na mgogoro wowote baada ya kutokea kwa kifo cha Rais John Magufuli.

Akizungumza jana na waandishi wa habari mara baada ya kufanyika kikao cha halmashauri kuu hiyo, Mwenyekiti wa CCM mkoani humo, Godwin Mkanwa, alisema:

"Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Dodoma tunaona Katiba hii ya toleo la 1977 bado inafaa sana na hakuna ulazima wa kuichokonoa, hakuna ulazima wa kutafuta Katiba Mpya wakati hii imetupitisha salama."

Mkanwa alisema katika Katiba Pendekezwa, kuna kifungu kinasema kuwa endapo Rais akifariki dunia akiwa madarakani, lazima zipite siku 90 na baada ya hapo uitishwe uchaguzi wa kujaza nafasi hiyo.

"Halmashauri Kuu inaona kama Katiba Pendekezwa ingekuwa ndiyo Katiba inayotumika sasa, isingetutoa salama,” alisema.

Zikiwa zimebaki siku nne kabla ya kufanyika Mkutano Mkuu wa CCM wa kumpitisha Rais Samia kuwa Mwenyekiti wa chama hicho, halmashauri kuu hiyo ya Dodoma imewaomba wajumbe wa kumpitisha kwa asilimia 100 kutokana na uwezo alionao.

Mkutano huo maalum unatarajiwa kufanyika Aprili 30 mwaka huu jijini Dodoma.

Mkanwa aliwaomba wajumbe kumchagua kwa kishindo ili kumpa nguvu ya kutekeleza majukumu yake.

"Kama ambavyo tumemsikia kwa siku hizi 37 tangu awe Rais wetu, ameonyesha mwelekeo ambao kila mtanzania amekubali, tumchague kwa asilimia 100 ili sasa tumpe nguvu ya kutekeleza majukumu yake ipasavyo," alisema.

Vilevile, alisema halmashauri kuu hiyo imetoa azimio la kumpongeza Rais Samia na kumpa pole ya kuondokewa na aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati Dk. Magufuli.

Chanzo: Gazeti la Nipashe
 
Hoja mojawapo ya Vyama vya Upinzani iliyotakiwa kujadiliwa Ikulu ishajibiwa na Kamati Kuu,
Ngoja tuzidi kuvuta subira kwakuwa siku zote inavuta kheri!!!
 
Kuna watu ndani ya CCM, nadhani wana uwendawazimu. Wananchi walishatamka, kufuatia rasimu ya Jaji Warioba, kuwa wanataka katiba mpya. Sasa hao Halmashauri ya CCM Mkoa wa Dodoma, ni wendawazimu wasuojua kuwa mamlaka iliyo kuu kuliko wote ni wananchi?

Kweli ndani ya CCM kuna wajinga wengi!

Wananchi walikwishatamka wanataka katiba mpya, kinachosubiriwa ni utaratibu wa kumalizia mchakato wa katiba, siyo kujadili kama kunahitajika katiba mpya au hapana.
 
Back
Top Bottom