CCM Dodoki ni Chimbuko la Ufisadi...? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM Dodoki ni Chimbuko la Ufisadi...?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bill, Jul 10, 2008.

 1. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #1
  Jul 10, 2008
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,167
  Likes Received: 1,251
  Trophy Points: 280
  Taratibu CCM imebadilika kutoka Chama cha Wakulima na Wafanyakazi kinachopigania maslahi na usawa wa Wananchi wote bila kujali dini, rangi wala kabila. Badala ya kuwa Chama sasa kimekuwa ni genge la wezi na madalali wa nchi na mali asili ya nchi huku ikiweka kando misingi ilyoanzishwa na kuwekwa katika Azimio la Arusha.

  Nchi imekosa dira, Viongozi hawajui taifa linakoelekea kila kukicha wako busy na ukuwadi wa kuuza nchi kwa maslahi binafsi.

  Ufisadi tunaoushudia leo ulianza siku nyingi mara mwalimu JK Nyerere alipotoka Ikulu. CCM ikaanza kupoteza mwelekeo.

  Mafisadi walianza na vyama vya ushirika, wakaja kwenye Viwanda vyetu, Wakaanzisha SUKITA wakaila, wakageukia mashirika ya UMMA wakala, wakaja kwenye mikataba ya Ujenzi wa Barabara, IPTL nk, Ikaja benki kuu (EPA), wakaanzisha mashirika fake kama Richmond ili kuchota fedha.

  Nyerere alisema kuwa CCM imekuwa ni Dodoki linalobeba Uchafu na limebeba uchafu kwelikweli. Mafisadi wote wako Ndani yake na ndio wanatoa maamuzi katika CC na NEC.

  JF katika hili CCM itakana kuwa ndio chimbuko la Ufisadii na Kinara wa ufisadi hapa nchini?
   
 2. Dx and Rx

  Dx and Rx JF-Expert Member

  #2
  Jul 28, 2017
  Joined: Jul 16, 2017
  Messages: 873
  Likes Received: 2,309
  Trophy Points: 180

  huu uzi tangu uanzishwe haujawahi kujadiliwa
   
Loading...