CCM demokrasia zaidi 2010 kumekucha!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM demokrasia zaidi 2010 kumekucha!!!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by MzalendoHalisi, Mar 8, 2009.

 1. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #1
  Mar 8, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  JF

  Kuna hii outcome ya Mkutano wa Halmashauri Kuu CCM Dodoma: je mnasemaje?

  Yaani kura za wagombea Ubunge na Madiwani zitapigwa na wanachama wote matawini tofauti na wajumbe wachache kuwapigia kura wagombea Wilayani!

  Hii inaonekana inaimarisha demokrasia!

  Je huku matawini watu hawatapewa kanga na wali?

  Vipi Katibu (W) ataaminika? Je akipokea rushwa na kujumlisha kura kiupendeleo au kuweka kura hewa kuna njia zipi kuhakiki?

  Vipi gharama la zoezi hili?

  HabariLeo: Gwiji la habari Tanzania | Mafisadi wabanwa kuwania ubunge
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Mar 8, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,681
  Likes Received: 82,533
  Trophy Points: 280
  Mbona wagombea Urais hawakuwekwa na wao wapigiwe kura na wanachama wote Tanzania nzima!? Kulikoni!?
   
 3. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #3
  Mar 8, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mzalendohalisi,

  Hii ni habari nzuri sana. Waliokuwa wamezoea kuwahonga wajumbe, sasa kama wana pesa wahonge wilaya nzima.

  Hii naona itakuwa kama ilivyo kura ya maoni USA. Itafanya wanaowania nafasi sera zao zilijulikane vizuri kwa wananchi na sio udanganyifu na usanii wa siku moja kwenye mkutano wa uchaguzi.

  Mimi ningetaka utaratibu huu utumike hata kwenye kumpata mgombea urais wa chama. Na yeye apigiwe kura za maoni na wanachama wote wa CCM.

  Mnaowania 2010 jiandaeni vizuri maana ngoma itakuwa nzito hasa! Unaweza kufanya usanii siku moja lakini kufanya usanii kwenye viijiji au kata 50 sio rahisi sana.
   
 4. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #4
  Mar 9, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mafisadi wabanwa kuwania ubunge
  Martha Mtangoo, Dodoma
  Daily News; Sunday,March 08, 2009 @19:17

  Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeamua kuanzia sasa kuwa wagombea wa ubunge, Baraza la Wawakilishi na madiwani, watakuwa wakipigiwa kura za maoni na kila mwanachama badala ya utaratibu wa zamani uliokuwa ukiruhusu wajumbe wachache kupitia mikutano mikuu ya majimbo.

  Uamuzi huo umepitishwa na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya chama hicho, kwenye kikao chake kilichofanyika juzi mjini hapa. Utaratibu huo unafuta uliokuwepo ambao kura za maoni zilikuwa zikipigwa na wajumbe wachache kupitia mikutano mikuu ya majimbo.

  Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, John Chiligati alisema kuwa utaratibu huo utaondoa tabia mbaya iliyojitokeza katika siku zilizopita kwa baadhi ya wagombea kutoa rushwa kwa wapiga kura ili kujipatia ushindi kwa kuwa chini ya utaratibu mpya, haitakuwa rahisi kuwahonga wanachama katika matawi yote jimboni bila ya kubainika.

  Chiligati alisema leo kwamba uamuzi huo ni azma ya kupanua demokrasia ndani ya chama, na kuwashirikisha wanachama katika kupiga kura za maoni. Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa, Chiligati alisema utaratibu huo utaanza kutumika katika uchaguzi mkuu ujao.

  Chini ya utaratibu huo mpya, kabla ya kura za maoni, wagombea watapata fursa ya kutembelea matawi yote na kukutana na wanachama wa CCM kwa lengo la kujitambulisha na kuomba kura. Alisema ziara hizo zitaandaliwa na CCM ngazi ya Wilaya na wagombea watasafiri kwa pamoja kwa usafiri ulioandaliwa na kugharimiwa na chama, hatua ambayo ina lengo la kutoa haki sawa kwa kila mgombea kutembelea matawi yote na kujitambulisha.

  Aidha, Chiligati alisema baada ya ziara ya kujitambulisha kukamilika, itapangwa siku moja ambayo wanachama wote watapiga kura kwenye matawi yao. Upigaji kura utaanza saa 2 asubuhi hadi saa 8 mchana na kamati ya siasa ya tawi itaweka utaratibu wa kuhakiki kazi hiyo.

  Alisema kura zitahesabiwa katika kituo husika na matokeo kutangazwa siku hiyohiyo na nakala ya matokeo hayo itabandikwa hadharani nje ya ofisi ya tawi au mahali ambapo kura zitapigiwa ili yawe wazi. Alisema kila mgombea atakuwa na haki ya kuweka wakala wa kusimamia upigaji kura na kazi ya kuhesabu huku wilaya ikiweka wasimamizi wa uchaguzi katika kila tawi.

  Katibu huyo wa itikadi na uenezi, alieleza kuwa katika utaratibu huo baada ya kura kuhesabiwa katika kituo na matokeo kutangazwa, msimamizi wa kituo atatakiwa kupeleka matokeo hayo haraka kwa Katibu wa Chama wa Wilaya. Alisema baada ya matokeo kutoka katika matawi yote na kufika wilayani, Katibu wa chama atajumuisha kura za kila mgombea na kwamba kila mgombea atakuwa na haki ya kuwepo mwenyewe au mwakilishi wake.

  Kwa mujibu wa Chiligati, baada ya kazi hiyo kukamilika, vikao vya ngazi ya wilaya, mkoa na taifa vitakaa kuchambua kwa undani zaidi juu ya sifa za wagombea na kuzingatia kura za maoni walizopata na hatimaye yatawasilishwa kwenye Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi na ratiba ya tume ya uchaguzi.

  Alisema kuwa NEC inaamini kuwa utaratibu huo utatoa nafasi kwa kila mwanachama kushirikishwa katika mchakato wa kuwapata wagombea na pia watashiriki kuwaunga mkono wagombea wa CCM kupata ushindi katika uchaguzi mkuu. Aidha alisema halmashauri kuu imeagiza kamati za usalama na maadili katika ngazi zote kuwa macho wakati wa kura za maoni ili kubaini vitendo vya rushwa.

  Alisema atakayebainika kukiuka kanuni za uchaguzi ataenguliwa katika kugombea na iwapo atajihusisha na rushwa atafikishwa mbele ya vyombo vya sheria. Wakati huo huo, Serikali ya Muungano na ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) zimeelekezwa kubadili katiba na sheria ya uchaguzi ili kuweka ukomo wa idadi ya wabunge na wawakilishi kufikia idadi inayohitajika.

  Chiligati alisema NEC imeelekeza ukomo wa idadi ya wabunge katika Bunge la Muungano kuwa 360 na idadi ya Wawakilishi kuwa 86. Serikali hizo zimetakiwa pia kuhalalisha kisheria utaratibu mpya wa kuwapata wabunge wanawake kupitia viti maalumu.

  Imeshauriwa Katiba ya SMZ ifanyiwe marekebisho ili kumwezesha Rais kuteua wanawake wasiopungua watano katika nafasi 10 alizonazo kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar. Alisema utaratibu wowote wa kuongeza idadi ya wabunge wanawake lazima izingatie ukomo huo na kuongeza kuwa utaratibu uliopo wa kuwapata wabunge na wawakilishi wanawake wa viti maalumu, utaendelea isipokuwa idadi yao katika kila chombo itapatikana kutokana na asilimia 50 ya wabunge wote wa majimbo 232.

  Iwapo Bunge litakuwa na ukomo wa viti 360 wakati idadi ya majimbo yaliyopo sasa ni 232, wabunge wanawake watakaopatikana watakuwa 116 ambayo ni sawa na asilimia 50 ya wabunge wote wa majimbo. Hata hivyo, katibu huyo alifafanua kuwa kuna wabunge wanawake saba ambao watapatikana kwa mujibu wa katiba ambapo kwa utaratibu huo, wanawake 109 ndio watakaopatikana kupitia viti maalumu.

  Chiligati alisema kuwa katika kuandaa orodha ya wagombea wanawake kwa nafasi 109 za Bunge na nafasi 20 za uwakilishi zitakazogombewa, NEC imependekeza wapigiwe kura na vikao vya Umoja wa Wanawake (UWT). Alisema kupitia utaratibu huo, wagombea ubunge na uwakilishi watapigiwa kura na mkutano mkuu wa UWT mkoa huku kwa upande wa wagombea udiwani viti maalumu, wanawake watapigiwa kura na mkutano mkuu wa wilaya.
   
 5. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #5
  Mar 9, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Jamani tunarudia ule mfumo wa wakati wa Nyerere wa ''Chama kushika hatamu"? Hivi chama kimojawapo katika msururu wa vyama kinakuwa na uwezo wa kuziagiza serikali kufanya mabadiliko ya Katiba? Mbona kilio hiki cha kufanya marekebisho ya Katiba ya nchi kimeshapigiwa kelele na Wananchi na Taasisi mbali mbali za haki za binaadamu lakini maoni hayo yamekuwa yakipuuzwa. Leo CCM kwa utashi wake kinasema kufanyike marekebisho ya kuwapata wabunge na wawakilishi na bila shaka hilo litatimizwa.
  Hili la kubadilisha katiba ili kupatikane uwakilishi wa wanawake lisiwe linafanyika eti CCM ndio imeagiza hivyo. Hili ni suala la Kitaifa na kunahitajika maoni yao na sio maoni ya Wajumbe wa NEC peke yao.
  Tuwe waadilifu,wanachama wa CCM na vyama vyengine vya siasa ni wachache mno kuwakilisha maoni na matakwa ya wananchi kwa jumla na kwa mantiki hiyo NEC ya CCM isiwe mtowa maagizo kwa serikali bali wananchi wasikilizwe haja yao ya Marekebisho ya Jumla ya Katiba.
   
 6. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #6
  Mar 9, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135

  Nionavyo mimi hili lingekuwa lenye faida sana kwa Watanzania kama uwazi wa kuhesabiwa na kutangazwa kura wanaopendekeza CCM wangeagiza tume za uchaguzi kufanya uwazi kama huo wakati wa mchakato wa uchaguzi wa Kitaifa . Ile tabia ya usiri na kusafirisha masanduku ya kura eti kwenda kuhesabiwa sehemu fulani si utaratibu sahihi na CCM inaelewa hilo ndio maana chaguzi zake inataka ziwe huru kwa vile wanaoshindana ni wao kwa wao. Inashangaza hasa kule Zanzibar idadi ndogo tu ya wapiga kura matokeo yanachukuwa masiku kutangazwa.
   
 7. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #7
  Mar 9, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,681
  Likes Received: 82,533
  Trophy Points: 280
  Mtanzania una mawazo kama mimi, sielewi kwanini wagombea Urais nao hawakutakiwa washiriki katika kura hizi. Hili likitokea litaondoa mambo ya aibu ya kununua wajumbe tena kwa $ yaliyofanywa na the so called wana mtandao katika kupata mgombea wa CCM mwaka 2005.
   
 8. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #8
  Mar 9, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  1. Ila ktk vikao vyote vya CCM kwa karibuni mawazo ya huu mkutano yameenda shule! Mafisadi watakoma!

  2. Mabadiliko ya katiba ni swala kubwa nadhani ni swala la Kitaifa zaidi..tuwe na tume huru ya kuhakiki mapungufu ya katiba iliyopo na kutoa mapendekezo ya katiba mpya..na baadae kura ya maoni ya wanainchi wote!
   
 9. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #9
  Mar 9, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Laiti haya mabadiliko wanayopendekeza, wangeyatumia hata kwenye uchaguzi mkuu, nina uhakika ingepunguza matatizo mengi sana hasa kule Zanzibar.

  Kumbe CCM wanaelewa nini maana ya kuendesha uchaguzi huru, ila wanashindwa kufanya kweli kweli chaguzi kuu kwasababu ya kulinda maslahi yao binafsi badala ya nchi.

  Hili tamko la leo naona linajenga demlokrasia kubwa sana ndani ya chama. Suala ni je lini wataandaa utaratibu mpya wa kujenga demokrasia kwenye chaguzi kuu?

  Wameharibu tu kuondoa uchaguzi wa rais kwenye mchakato huu.

  Kumekucha 2010 kwenye chaguzi za CCM, nina uhakika kuna watu watadundana ngumi kwenye gari zitakazokuwa zinawachukua wagombea.
   
 10. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #10
  Mar 9, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Kwa hili la CCM yaonekana JK angalau amepania kupunguza ufisadi ktk mchakato wa kutafuta wagombea CCM!

  Je ni kwa nini CCM walijua kuwa kuna mchezo mchafu wa kuhonga wajumbe Wilayani mda wote bila kuchukua hatua kama hizi? Yaani mda wote tangu 1977, 1992 hadi leo hii?

  Why a U turn ktk CCM now?
   
 11. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #11
  Mar 9, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mzalendohalisi,

  Utaratibu uliotangazwa ndio ulikuwa unatumika huko nyuma ingawaje kuna tofauti kidogo.

  Nakumbuka nilipokuwa seconday mwaka 1985 nilishuhudia mpambano mkali kati ya mama Weja na Ditopile pale Ilala. Walikuwa wanazunguka pamoja kwenye matawi kuomba kura. Jinsi Ditopile alivyokuwa anamtukana yule mama, nikamchukia |itopile toka siku hiyo.

  Huu utaratibu wa sasa nadhani ulianza 1995 japo sina uhakika.

  Tutafaidi kweli 2010.
   
 12. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #12
  Mar 9, 2009
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Maamuzi mazuri so far, hata hivyo tungoje details za utekelezaji kama itakavyoelezwa kwenye mwongozo wa huu utaratibu mpya.
   
 13. Sura-ya-Kwanza

  Sura-ya-Kwanza JF-Expert Member

  #13
  Mar 9, 2009
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 561
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35


  Nimefurahi kuliko!

  Nilishanena humu ndani kuhusu demokrasia ndani ya chama chetu mtanzania:D
  CCM!
  Kweli huu ni mpito mzuri kabla ya 2010 na 2015 kwani wameona itakuwa vigumu kupata wanachama wanaochagulika kiufiadi-fisadi:rolleyes:

  Nafikiri hili linabidi lifurahiwe na Watanzania wote.:cool:

  Kidumu!
   
 14. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #14
  Mar 9, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  CCM ya miaka hiyo ya nyuma haikuwa na rushwa kama hii ya leo. Sioni kama kulikuwa na sababu. Mazingira ya chaguzi zetu, fikra za wapiga kura na ccm yenyewe wamebadilika...na haya ndio matokeo yake.
   
 15. A

  August JF-Expert Member

  #15
  Mar 9, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,509
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  hiyo demokrasia wange iongezea pia katika kuchagua viongozi wa chama, sio pendekezo la mwenyekiti, ndio watapata viongozi vibrant, na si puppet
   
 16. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #16
  Mar 9, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  Jamani muda umefika kila lililo jema na liwekwe lifanye kazi.....itafikia muda hata uraisi nao itabidi apatikane kama ilivyo wenzetu ambako demokrasia imekoamaa....tupige kura nchi nzima.....itasaidia sana kupunguza ufisadi wa kuhonga wajumbe wachache wa mkutano mkuu kama ilivyokuwa mwaka 2005.........maana kuna wapambe walitoa pesa mingi sana kwa wajumbe na malazi chakula muda wote waliokaa dodoma.
   
 17. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #17
  Mar 9, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mtanzania, Bubu AK et al.

  Huu ni mwanzo mzuri kwa CCM kujijenga na kurudia misingi ya kuanzishwa kwake. Mimi naona mnakuwa na haraka mnaposema utaratibu huu ungejumuisha wagombea uraisi. Ni wazo zuri ila tukiangalia kwa mapana utekelezaji wake, inaonekana ni mgumu mno.

  Wagombe ubunge, mfano wagombea ubunge Jimbo la Ilala watalazimika kutembelea matawi 150-200 katika jimbo lao. Je, Mgombea uraisi itamlazimu kutembelea kila tawi katika kila mkoa..!!?? Au ndio itamlazimu atumie wapambe? Akishatumia wapambe, lengo la wazo hili linakuwa halina maana tena. Tuwape muda CCM huenda baada ya utekelezaji wa utaratibu huu mpya kwa Wabunge etc 2015 wanaweza kujumuisha nafasi ya Uraisi.

  Hata hivyo, ni muhimu kukumbuka kuwa utaratibu huu ukiwezesha Bunge kuwa na wabunge wengi waadilifu basi Raisi na Serikali watakuwa hawana ujanja wa kuliburuza Bunge.

  Tangu CCM na Serikali yake walipokubali kuanzishwa kwa vyama vingi Tanzania 1992 hii habari ni njema kuliko zote. Veri gud nyuzi indidi.
   
 18. C

  Chuma JF-Expert Member

  #18
  Mar 9, 2009
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  nani atabeba cost za huo uchaguzi...? CCM pesa zote wanapata wapi? wao wanatumia pesa za Umma kujinufaisha...how?

  Vyama vya upinzani bila kurudi ktk Maoni ya Jaji Kisanga kuna kazi ya kushinda uchaguzi...Benefits walizokuwa wanapata CCM before Vyama vingi ndio wanaendelea kuvitumia after Vyama Vingi. Vyama vinasubiri pesa za uchaguzi zifanye kampeni wataweza wapi?..na huku wafanya biashara washabanwa wanaambiwa ukitaka biashara zako ziende chagua CCM, ukiwa mfanya biashara mpinzani JOTO ya JIWE utaijuwa...!!!

  Kwa sytle tunayokwenda nayo, Upinzani unaingia ktk chaguzi huku tayari ni vilema wa Funds...
   
 19. W

  WildCard JF-Expert Member

  #19
  Mar 9, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Kura zitaendelea kununuliwa na wagombea kwa kutumia mawakala wao. Hapa wamewaongezea gharama wagombea wao. Njia nzuri ya kuwapata wagombea safi pamoja na kura hizi za wanachama ni kwafahamu kwa undani wagombea wetu na mema na mabaya yao yakawekwa hadharani. Vinginevyo tuendelee kutumia umasikini wa wapiga kura wetu kushinda kwa kishindo.
   
 20. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #20
  Mar 9, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Kwa hili CCM imefanya jambo jema!

  1. Kwa kura ya Uraisi wanatakiwa kufanya marekebisho kidogo sana... baada ya kuzunguka nchi nzima wagombea wote kwa pamoja kwenye magari ya chama , kwenye vikao mfano vya kamati za siasa za mikoa (au vikao vinaitwa vya wajumbe wawakilishi wa wawapiga kura). Nadhani ingekuwa poa kama kura ingetengewa siku moja kwa mikoa yote.

  2. Nadhani vile vikao vya matawi, vingechagua wapiga kura wawakilishi,,, kwa ajili ya kupiga kura ya mgombea wa urais. Kwa maana kila tawi labda litafute watu watano ambao linaona watawakilisha mawazo ya wapiga kura wao... na hawa ndio wanaunda wajumbe wa kupiga kura ya mgombea wa urais kwenye kikao cha mkoa.
   
Loading...