CCM: Dawa na maji safi siyo anasa kwa wananchi

SautiYaMnyonge

JF-Expert Member
May 13, 2018
439
742
Na Mwandishi Wetu,
Mbozi-Songwe.

Chama Cha Mapinduzi kimesema kwa hali inavyokwenda nchini kunataka kujengeka tabia ya kuonekana kuwa dawa na maji safi kwa wananchi ni suala la anasa wakati ni mahitaji muhimu kwa uhai wa maisha na uchumi.

Kimesema changamoto za upungufu mkubwa wa dawa, maji safi na salama pamoja na wawekezaji kucheleweshewa huduma za msingi za wao kuanza uzalishaji zimebainika jambo ambalo CCM haiwezi kuyavumilia.

Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo ameyasema hayo wakati wa majumuisho ya ziara yake na sekretariet mkoani Songwe katika ukumbi wa Mkonongo mkoani hapa.

Amefahamisha kuwa wananchi wanalipa kodi na wanachangia huduma hizo haiwezekani waliopewa dhamana wasiwasikilize na kufanya bidii ya kutatua kero walizo nazo.

"Kote tulikopita kilio ni dawa na maji safi, naomba niwahakikishie ndani ya wiki !moja baada ya kurejea Dodoma nitaziita wizara zote zinazohusika kutueleza hili limekaaje maana serikali inatenga mabilioni ya fedha na kila wakati kauli za tunazo dawa za kutosha zinatolewa wakati haziakisi uhalisia kwenye maeneo ya huduma kwa wananchi. Tunataka kujua tatizo ni nini, ili kutatua changamoto hii. Vivyo hivyo kwenye maji safi" alisema Chongolo

Chongolo amewataka wataalam wa halmashauri zote nchini kuhakikisha pale wanapoibua miradi ya kimkakati yenye kulenga kusisimua uchumi na kuongeza mapato kwenye maeneo yao wahakikishe inazingatia mahitaji na matakwa halisi ya watumiaji wa makundi mbalimbali ya kijamii na kiuchumi hususani wananchi wa kipato cha chini na kati.

"Unapenda kubaki au kuendelea na cheo au dhamana uliyoaminiwa timiza wajibu kwa kuhakikisha wananchi wanaona fahari ya wewe kuwepo katika nafasi uliyopo vinginevyo hatutakubali kukuona hapo wakati unatugombanisha nao, hii ndio kazi ya CCM." Alisema Chongolo

Hata hivyo kizungumza kwa kutoa mfano Chongolo amesema haiwezekani unajenga mradi wa soko halafu jengo lenyewe la ghorofa unataka mama mbogamboga akauzie ghorofa ya kwanza, halafu mradi wa aina hiyo hauna eneo la bodaboda, bajaji, machinga na mama/baba lishe kufanya shughuli zao lazima utakuwa mradi kero.

"Hakuna raia wa daraja teule, sote tuna hadhi sawa. Miradi hii izingatie mahitaji na mazingira halisia ya watumiaji yakiwemo makubwa mbalimbali ya kiuchumi yanayoweza kunufaika nao ili kuimarisha mnyororo huo wa uchumi vinginevyo serikali itawekeza fedha kwenye miradi isiyoleta matokeo yaliyotarajiwa." Alisema Chongolo

Katibu Mkuu wa CCM na Sekretarieti yake wanaendelea na ziara yao mkoani Mbeya kuanzia leo tarehe 11 Julai, 2021.

IMG_20210711_120917.jpg
 
Chongolo hapo kwenye masoko umenigusa sana.
Nchi yetu na tamaduni zetu zauuzaji was bidhaa haujafikia kupanga kwenye magorofa ni usumbufu sana,masoko yote yaliyojengwa kwa mfumo huo sio rafiki kwa wapangaji/wanunuzi.

Maji:Ni aibu kubwa kuzungumzia maji 60yrs wakati mito,mabwawa na maziwa yamejaa.
Ni dharau kubwa sana kwa wananchi.
Hesabu ya Magazijuto:
Kununua ndege kwa cash ndani ya miaka 3 imewezekana.
Kwanini haiwezekani kupata maji ndani ya miaka hiyo 3 nchi nzima?

Wanaotumia maji ni wengi kuliko watumiaji wa usafiri wa ndege.
Tens ndege zinatupa hasara huku mwananchi asiye na haduma ya maji anakatwa kodi.

Chongolo una kauli zinazoakisi uhalisia wa maisha,ila pole hutakaa kwenye hiyo nafasi mda mrefu.
MFUMO WA CHAMA NA SERIKALI KWENYE VIPAUMBELE NITOFAUTI.

Ziara njema
 
Chongolo hapo kwenye masoko umenigusa sana.
Nchi yetu na tamaduni zetu zauuzaji was bidhaa haujafikia kupanga kwenye magorofa ni usumbufu sana,masoko yote yaliyojengwa kwa mfumo huo sio rafiki kwa wapangaji/wanunuzi..
Bora umemwambie akae akijua anapiga ngoma tofauti na style ya wachezaji. Hakuna taasisi ya wajinga nchi hii kama bunge. Ni bungeni ndiko utakuta kauli za "tumesambaza maji asilimia 78 vijijini 84 Mjini. Unajiuliza ni Mji gani huo ambao maji yanapatikana asilimia 84? Au neno Mji lina maana tofauti siku hizi?
 
Ni KWELI ILA MISHAHARA ya MAMILIONI NA MAGARI YA KIFAHARI KWA WABUNGE NA VIONGOZI NDIO ANASA
 
Back
Top Bottom