Elections 2010 CCM Dar watangaza maandamano na kuahirisha ndani ya dakika 5

SG8

JF-Expert Member
Dec 12, 2009
3,955
2,125
Wadau nini kimetokea kwa CCM mkoa wa Dar es Salaam kutangaza maandamano na kuahirisha ndani ya dakika tano?. Kiufupi katika siku chache ambazo nimeangalia Channel Ten taarifa ya habari nimekutana na kioja. katibu wa CCM Mkoa wa Dar Bw. Kilumbe Ng'enda ameonekana akitangaza maandamano ya wana CCM wa Dar kulaani kile alichokiita kudhalilishwa kwa M/kiti wa CCM na wabunge wa Chadema. Wakati nikiwa na hasira kwamba kumbe na chadema nao wangeandaa maandamano kupinga uchakachuaji wa NEC ghafla msomaji wa habari akaja na Breaking News kwamba maandamano hayo yameahirishwa hadi wakati mwingine. Nini kimetokea? Tafakari

SOURCE CHANNEL TEN NEWS at 1900 HRS TODAY 20th Nov 2010
 
Nadhani watu wanaofikiria kwa kutumia ubongo, wametambua madhara ya hayo maandamano. Ninaamini kwamba kundi kubwa sana la watanzania linaunga mkono kile kilichofanywa na wabunge wa chadema. Kitendo cha CCM kuandamana kupinga hilo kingeamsha hasira miongoni mwa mashabiki wa chadema ambazo zingesababisha uvunjifu wa amani. Nadhani watu wenye akili timamu watakuwa wamewashauri CCM wasifanye utoto huo.
 
Wangewasha moto mkubwa sana , ambapo kuuzima ingekuwa balaa, yaani kiufupi SISI CHADEMA tungeandamana NCHI NZIMA, na hapo ndo ingekuwa MSHIKEMSHIKE
 
Nasikia yamehairishwa kwa kuwa malori ya kubeba watu na kuwaleta Dar bado hayajakubaliana mshiko. Kwa hiyo ccm bado wanatafuta malori ya kubeba wajingajinga ili waonekane kuwa ni wengi kwenye maandamano.
 
du nilikuwa nimeshaanda panga langu wakipita tu mimi na wao. mimi sina mabomu ya machozi bali jambia, shuwaini
Haki ya Mzungu hasira zingine zinanifanya nicheke huku machozi yananitoka. I don't get a photo kwa kweli. Mungu aepushie mbali
 
Kama CCM wanafikiri M/kiti wao amedhalilishwa? Basi wafanye uamuzi kama aliosema mtu wao jana. Hakika we are tired, nini maana ya democrasia?

The message is sent, then majukumu mengine yataendelea.

KAMA MPO SERIOUS WAFUKUZENI WABUNGE WA CHADEMA BUNGENI THEN MKUBALI KUPOKEA MATAKACHOKUWA MMEPANDA.
 
Wadau nini kimetokea kwa CCM mkoa wa Dar es Salaam kutangaza maandamano na kuahirisha ndani ya dakika tano?. Kiufupi katika siku chache ambazo nimeangalia Channel Ten taarifa ya habari nimekutana na kioja. katibu wa CCM Mkoa wa Dar Bw. Kilumbe Ng'enda ameonekana akitangaza maandamano ya wana CCM wa Dar kulaani kile alichokiita kudhalilishwa kwa M/kiti wa CCM na wabunge wa Chadema. Wakati nikiwa na hasira kwamba kumbe na chadema nao wangeandaa maandamano kupinga uchakachuaji wa NEC ghafla msomaji wa habari akaja na Breaking News kwamba maandamano hayo yameahirishwa hadi wakati mwingine. Nini kimetokea? Tafakari

SOURCE CHANNEL TEN NEWS at 1900 HRS TODAY 20th Nov 2010
Hivi CCM wanatambua kuwa hawana miji Dar penyewe wako nusu nusu, wakianzisha Dar watapokelewa na maadamano ya Chadema Arusha kabla hayajaenda Mbeya na Moshi mjini na kuishia Musoma na Mwanza watayaweza? Halafu watakumbushia kura moja ya Shinyanga nafikiri patakuwa hapatoshi, ndiyo maana CCM wachache wenye busara zao wameona hayalipi.
 
Ooh tumeimarisha demokrasia kwa sasa watz wana uhuru za kuongea na kutoa maoni yao. Kama hiyo ni kweli ni wazi demokrasia hiyo itakuwa imeletwa na serikali ya CCM ikishirikiana na wadau wengine. Iweje sasa wabunge wa CDM kufanya kitendo cha kidemokrasia iwe nongwa?

Tumeshamskia Chiligati akichemka (nafikiri kuonyesha yupo hasa kipindi hiki cha mgawo wa vyeo). CCM pia heka heka. Jamani wana CCM Raisi JK amesema serikali yake imeimarisha demokrasia nchini. Wana CCM na wengine mnaopata tabu kuelewa kitendo cha wabunge wa CDM kutoka nje ya mkutano ni njia moja ya haki kabisa ya kujieleza. Get it
 
na waandamane, kwa hasra sis CDM tuingegoma kula sku mbili mfululzo... Kuonesha Rais wao hatumtambui!
 
Jamani nani tena kawastua CCM naona polisi imeanza kuwaonea naomba waingie mitaani tuchukulie advantage ya maandamano yao. Heko Chadema kwa kucheza karata zenu vizuri maana CCM hawalali.
 
Hivi CCM wanatambua kuwa hawana miji Dar penyewe wako nusu nusu, wakianzisha Dar watapokelewa na maadamano ya Chadema Arusha kabla hayajaenda Mbeya na Moshi mjini na kuishia Musoma na Mwanza watayaweza? Halafu watakumbushia kura moja ya Shinyanga nafikiri patakuwa hapatoshi, ndiyo maana CCM wachache wenye busara zao wameona hayalipi.

I Salute u mkuu,

Hii umeiweka vizuri, unajua hawa jamaa wanasahau kuwa hawana miji/majiji tena. Hii kitu bado haijakaa sawa akilini mwao ndio maana wanakimbilia kutoa maagizo ya mwaka 47, naona kuna muungwana mmoja amewastua kuwa wao si watu wa mujini tena...:teeth:
 
Jamani CCM ingieni bana mtaani muandamane enh! Aiih nyiee, msighairi CCM andamaneni nasi tuandamane...
 
TANZANIA KAZI IPO, sikuwahi kushuhudia maandamano ya kupinga mafisadi, maandamano ya kudai MUAFAKA wa RICHMOND lakini leo hii watu wa CCM wanataka kufanya maandamano, jamani KUWENI SERIOUS KIDOGO.
 
Kuna watu hawaelewi uchaguzi 2010 ulikorogwa na ccm? Nchi imetumia hela nyingi kwenye uchaguzi ili taifa lipate viongozi kulingana na matakwa ya wananchi. Wahuni wachache wameteka nyara matakwa ya wananchi na kupandikiza viongozi wasiochaguliwa. Mabillion ya pesa za uchaguzi zimepotea bure, sasa wahuni wakishilikiana na mafisadi wataendelea kutawala na kudidimiza maendeleo ya nchi. Hivi kweli mtu anaweza kuandamana ili kuunga mkono huu ufilauni? Huu ni wakati ambao watanzania wote inabidi watafute ukweli badala ya kuja na hisia za kiushaabiki. Tutafute ukweli juu ya madai ya wizi wa kura na namna ya kuzuia matatizo kama haya katika chaguzi zifuatazo. ONLY the truth shall set Tanzania free!
 
Namshangaa Chiligati na kudai eti wanaweza kupiga kura eti kwasababu wapo wengi Mbowe ameshawajibu kuwa hawana Haki Kisheria na hawana mamlaka hiyo ivi wanafikiri CHADEMA wanakurupuka kama wao, na watakua wa kwanza kupiga kura katiba ibadilishwe

Mzee Gomezi
 
Hayo maandamano wanakurupuka thubutu jaribuni muone na ole wenu katiba ibadilishwe hamrudi tena 2015 lazima ile kwenu

Mzee Gomezi
 
just stup*d.. wanaacha kuandamana mifumuko ya bei wanaandamana ujinga.
halafu wakishaandamana ndo inakuwaje?
 
Back
Top Bottom