Wadau nini kimetokea kwa CCM mkoa wa Dar es Salaam kutangaza maandamano na kuahirisha ndani ya dakika tano?. Kiufupi katika siku chache ambazo nimeangalia Channel Ten taarifa ya habari nimekutana na kioja. katibu wa CCM Mkoa wa Dar Bw. Kilumbe Ng'enda ameonekana akitangaza maandamano ya wana CCM wa Dar kulaani kile alichokiita kudhalilishwa kwa M/kiti wa CCM na wabunge wa Chadema. Wakati nikiwa na hasira kwamba kumbe na chadema nao wangeandaa maandamano kupinga uchakachuaji wa NEC ghafla msomaji wa habari akaja na Breaking News kwamba maandamano hayo yameahirishwa hadi wakati mwingine. Nini kimetokea? Tafakari
SOURCE CHANNEL TEN NEWS at 1900 HRS TODAY 20th Nov 2010
SOURCE CHANNEL TEN NEWS at 1900 HRS TODAY 20th Nov 2010