CCM Dar kwafukuta; Mwenyekiti UWT agoma kuitisha uchaguzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM Dar kwafukuta; Mwenyekiti UWT agoma kuitisha uchaguzi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Sep 5, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Sep 5, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  JUMATANO, SEPTEMBA 05, 2012 05:38 ADMINISTRATOR

  *Mwenyekiti UWT agoma kuitisha uchaguzi
  MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita, ameitaka Jumuiya ya Wanawake (UWT), mkoani humo kuitisha mara moja uchaguzi wa jumuiya hiyo katika Wilaya ya Kinondoni.

  Mbali na hilo, Mwenyekiti wa jumuiya hiyo, Zalina Madabida na Katibu wake, Tatu Malyaga, wanatarajiwa kuhojiwa na Kamati ya Maadili, Kamati ya Siasa na Halmashauri ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam, ili waeleze ni kwa nini wamepuuza maagizo ya kuitisha uchaguzi katika jumuiya hiyo.

  Guninita pia amewaagiza viongozi wa UWT Wilaya ya Kinondoni, kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika mara moja, vinginevyo chama kitawachukulia hatua za kinidhamu na vikao husika.

  Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Guninita, alisema CCM Mkoa wa Dar es Salaam, kimesikitishwa na uongozi wa UWT wa mkoa huo, kwa kuwa umevunja utaratibu na maelekezo ya chama yaliyotaka uchaguzi wa jumuiya zote ufanyike kati ya Agosti 31 na Septemba 2, mwaka huu.

  "Katika kikao cha Halmashauri ya Mkoa wa Dar es Salaam, kilichokaa Agosti 29 mwaka huu, tulipitisha wagombea wa nafasi zote, zikiwamo za jumuiya mbalimbali za chama.

  "Kikao hicho kiliagiza chaguzi zote za jumuiya ziwe zimefanyika na kumalizika kati ya Agosti 31 hadi Septemba 2, mwaka huu.

  "Lakini cha ajabu ni kwamba, kwa uzembe na sababu wanazozijua wao, Mwenyekiti na Katibu wa UWT Mkoa wa Dar es Salaam wamezuia kufanyika kwa uchaguzi wa Jumuiya yao Wilaya ya Kinondoni.

  "Kwa masikitiko makubwa, pamoja na chama mkoa kutoa maagizo hayo, uchaguzi wa UWT Wilaya ya Kinondoni haukufanyika kwa sababu zao binafsi, yaani wameamua kusimamisha uchaguzi bila sababu za msingi.

  "Viongozi hao wawili wamezuia chama kisifanye kazi zake kupitia vikao, nawasihi wanachama na viongozi wafuate taratibu za chama, wasivunje kanuni na maadili ya CCM.

  "Katika suala hili, nasema chama kitawachukulia hatua kali za kinidhamu ili liwe fundisho kwa wengine wanaotaka kuongoza jumuiya bila kufuata utaratibu," alisema Guninita.

  Zalina alipotafutwa kwa njia ya simu ili kuzungumzia suala hilo, alisema yuko kwenye kikao na kutaka mwandishi wetu ampigie simu baadaye.

  Hata hivyo, alipopigiwa tena, simu yake haikuwa hewani.  05 SEPTEMBER 2012


  Guninita amtaka Madabida, Katibu wake wajieleze

  Na Heri Shaaban

  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam kimeiagiza Kamati ya Maadili ya CCM Mkoa huo, kuwaita na kuwahoji Mwenyekiti, Bi.Zalina Madabida na Katibu wake, Bi.Tatu Malihega (UWT) Dar es Salaam kwa kukiuka kanuni na sheria za chama kwa kuzuia chaguzi za Jumuiya za CCM Wilaya ya Kinondoni zisifanyike.

  Tamko la kuwaita viongozi hao wahojiwe na Kamati ya Maadili CCM lilitolewa Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa, Bw.John Guninita wakati wakizungumza na waandishi wa habari.

  Bw.Guninita alisema Agosti 29, mwaka huu chama hicho kilifanya uchaguzi wa Jumuiya zote, lakini Umoja wa Wanawake wa Wilaya hiyo, uchaguzi haukufanyika baada ya Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Mkoa wa Dar es Salaam, Bi.Zalina Madabida na Katibu wake Bi.Tatu Malihega kuweka pingamizi.

  "Naagiza kamati ya maadili kuwaita na kuwahoji Mwenyekiti wa UWT, Bi.Zalina Madabida na Katibu Bi.Tatu Malihega kutokana na kukiuka taratibu za chama ili chama kiweze kutoa adhabu kali iwe fundisho kwa viongozi wengine," alisema Bw.Guninita.

  Alisema kuwa ameshangazwa na viongozi hao wa UWT kuingilia maamuzi ya kuzuia chaguzi za jumuiya, wakati wao hawana maamuzi yoyote ndani ya CCM.

  Aliwaagiza Bi.Madabida na Malihega kuhakikisha uchaguzi huo waliozuia unafanyika kama ulivyopangwa, Pia wasiingilie taratibu za chama, kwani chama hakiwezi kuzuiwa na mtu mmoja kufanya jambo lake.

  "Maagizo ya Halmashauri Kuu hayakutekelezwa kutokana na viongozi hao kukiuka sheria za chama, Katiba za CCM na kukwamisha mipango ndani ya chama hiki, naachia kamati hiyo iweze kuwahoji na kuwapa adhabu," alisema.

   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Sep 5, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Kazi za Guninita ? Madabida's Hawa walikuwa East Africa MP's Sasa Wapo NEC ni full FORCE ?
   
Loading...