MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,991
Kilichotokea katika uchaguzi wa serikali za mitaa ni matunda ambayo CCM Mkoa wa Dar es Salaam imeyavuna kwa haki. This change has been a long time coming!
Nimewaona na kuwasikia viongozi wa CCM Mkoa wa Dar wakilalamika na kufanya ulaghai wa kisheria.
CCM Mkoa wa Dar es Salaam wanatakiwa wawashukuru wakaazi wa Dar Es Salaam kwa kuwapa nafasi ya kipekee ya kuongoza Jiji kwa muda mrefu bila kurudisha fadhila hasa ikichukuliwa ni Jiji ambalo ni mfano na kioo nchini. Wana Dar wamepiga kelele kuanzia mwaka 2000 lakini CCM Mkoa wa Dar ikawa imeziba masikio. Wenye hekima na busara wakawaambia CCM Dar, One day you’re going to wake up and notice that you should’ve tried.
Kwa mujibu wa Sheria za Serikali za Mitaa sura 287 na 288, Mamlaka za Serikali za Mitaa zimepewa madaraka mbalimbali ya kisheria kwa kuzingatia misingi, kanuni na taratibu ili kuingia katika mikataba, kusamehe kodi, kukodisha wakala, kutwaa ardhi, kuwa na hazina na vyanzo vya mapato na kuuza na kumiliki mali katika maeneo yake.
CCM Mkoa wa Dar kwa kupitia Madiwani wake kuanzia mwaka 1995 wametumia sheria hizo katika msingi wa kujinufaisha kibinafsi huku wengine wakigeuka na kuwa mawakala na madalali wa watoa rushwa na mafisadi nchini.
Miradi ya usafiri ndani ya Jiji walibinafsisha au kuiuza kimagumashi, viwanja vya wazi wakawapa matajiri ili wajenge nyumba na vitega uchumi huku masikini wakiruhusiwa kujenga kwenye mabonde hatarishi. Vituo vya afya na hospitali za watu binafsi wakazifanya kama hospitali za kuhudumia wananchi wote kiasi kwamba wananchi wa Dar wasio na pesa za kutosha wakajikuta wako nje ya huduma ya afya. Huduma na miradi ya Maji safi na salama ikawekwa mikononi mwa wafanyabiashara wa maji. Kwa ujumla Jiji likawa chafu na hatari kwa maisha ya watu wa kipato cha chini.
Jiji ambalo lilikuwa linatakiwa liwe ni mfano wa kuigwa nchini, badala yake limegeuka kuwa mfano wa kutoigwa nchini. Mapato na vyanzo vya mapato haviendani na huduma ya kijamii kama shule, hospitali, miundombinu(majengo, barabara, majitaka) inayotolewa na Jiji.
CCM Dar es Salaam waliendelea kuichukua na kuitumia fadhila ya wana Dar for granted.
Wananchi wengi baada ya kuamua kuichukua fadhila yao na kuwapa wapinzani kwa njia ya kura, kwa sasa CCM Dar wameanza utapeli na ulaghai kwa kutumia taratibu na sheria ambazo haziko wazi. It’s too late.
Waingereza walisema, ‘’You’ll never know what you have until it’s gone’’
Kilichobaki kwa sasa kaeni chini ili wapinzani wenu wawaonyeshe thamani ya kuongoza Jiji la mfano kama Dar.