Elections 2010 CCM, CUF waungana kumsaka muuza shahada za kura Tanga

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,293
33,078
Katika hali isiyo ya kawaida, wafuasi na wakereketwa wa Chama cha Wananchi (CUF) na Chama Cha Mapinduzi (CCM), jana walilazimika kuweka itikadi zao za vyama pembeni na kuungana baada ya kupewa taarifa kwamba kuna mwanamke alikuwa akigawa fedha na

shahada za kughushi mithili ya njugu.
Tukio hilo lilitokea katika Kata ya Ngamiani Kusini wakati wafuasi hao wakiwa katika foleni ya kupiga kura jambo ambalo liliwalazimu kuahirisha zoezi hilo kwa muda na kuanza

kumsaka mtuhumiwa huyo.
Hali hiyo iliyozua taharuki kwa wanachama hao ambao kiujumla ni wapiga kura walidai kwamba taarifa walizopokea ni kwamba tayari takriban watu wasiopungua 10 walikuwa tayari wamepewa fedha na shahada hizo.
“Taarifa tumezipata hapa hapa kwamba anagawa shahada za kughushi na noti za Sh. 5,000. Ni bora tusipige kura lakini tumpate,” alisema kijana mmoja kati ya wanachama hao.

Hata hivyo, hali hiyo ya utata iliendelea kutawala katika kituo hicho ambapo mwanamke mmoja alikutwa akiwa na shahada mbili za kupigia kura, kitendo kilichomfanya polisi waliokuwapo eneo hilo kumweka chini ya ulinzi.

Wakati mwanamke huyo akiwa ndani kwa mahojiano na wasimamizi wa kituo hicho, baadhi ya wapiga kura walionekana kukerwa na kitendo hicho na kuanza kufoka wakitaka wamtoe nje ili wamshughulikie.

Akizungumza na NIPASHE, mtuhumiwa huyo alidai kuwa shahada moja alipewa mwaka 2005 wakati wa uchaguzi mkuu na nyingine alikabidhiwa wakati wa uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura mapema mwanzoni mwa mwaka huu.

Kwa upande wake, Msimamizi Msaidizi wa kituo hicho, Grace Masanyika, alisema wanafanyia kazi tatizo hilo ili kujua kama anaruhusiwa kisheria kupiga kura au la.
“Bado tatizo lake tunalifanyia kazi na kama itabainika sheria inaruhusu atapiga kura na iwapo ataonekana amekiuka sheria, basi hatua za kisheria zinazosimamia uchaguzi zitachukuliwa…hivyo kwa sasa bado tunatafuta suluhu.” alisema Masanyika.



CHANZO: NIPASHE
 
Ina maana zile fedha kutoka Conservatives wa Uingereza zilikuwa "zinaiba" kura!!!!!!
 
Back
Top Bottom