CCM, CUF wapigana

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,820
287,890
CCM, CUF wapigana

na Mwandishi Wetu

UHASAMA kati ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF), umefikia hatua mbaya, baada ya jana wafuasi wa vyama hivyo jijini Tanga kuzusha vurugu zilizosababisha watu kadhaa kujeruhiwa.

Aidha, vurugu hizo zilikuwa kubwa kiasi cha kuwalazimisha polisi kurusha risasi hewani, ili kutuliza hali ya mambo.

Habari kutoka Tanga zinaeleza kuwa vurugu hizo zilitokea jana jioni katika Barabara ya 20, ambako CUF walikuwa wanafanya mkutano wa hadhara, uliokuwa umepewa baraka na Jeshi la Polisi mkoani humo.

Labda kitu ambacho polisi hawakukizingatia wakati wanatoa kibali cha kufanyika kwa mkutano huo, ni ukaribu wa ofisi za CCM katika eneo hilo.

Habari zinaeleza kuwa mzungumzaji mkuu katika mkutano huo, Mkurugenzi wa Vijana wa CUF Taifa, Said Miraaj, alianza kuzungumza katika mkutano huo, lakini CCM nao walipandisha sauti za vipaza sauti vilivyokuwa katika ofisi zao, na kusababisha kutosikilizana katika mkutano wa CUF.

Inaelezwa kuwa kutokana na hali hiyo, viongozi wa CUF walitoa taarifa kwa Jeshi la Polisi, lakini hawakupata msaada wowote, hali iliyowalazimu kuahirisha mkutano huo.

Baada ya viongozi wa CUF kuahirisha mkutano huo, walibaki wanachama, ambapo mmoja wao alipanda jukwaani na kuanza kuhutubia, hali iliyowafanya wanachama wa CCM nao kumtaka baba wa kijana huyo naye kujibu mapigo kwa kukibeza chama hicho.

Kutokana na hali hiyo, chokochoko zilianza miongoni mwa wanachama hao na ndipo vurugu kubwa zilipozuka.

Mkuu wa Upelelezi (RCO) wa Mkoa wa Tanga, Seleman Nyakipande, alipoulizwa kuhusiana na tukio hilo, alikanusha kutokea kwa vurugu hizo, ingawa alikiri kuwa wanachama hao walirushiana maneno katika mkutano huo.

“Wanachama wa vyama hivyo walipokutana walianza kurushiana maneno, lakini hakukutokea vurugu za aina yoyote,” alisema RCO huyo.

Hata hivyo, alipotakiwa kueleza kwa nini polisi walirusha risasi hewani wakati wafuasi hao walikuwa wakirushiana maneno tu, RCO huyo alimtaka mwandishi wa habari hizi kumpigia baada ya muda, ili awasiliane na ‘vijana’ wake kwa kuwa hakuwepo eneo la tukio.

Alipopigiwa simu baadaye, Nyakipande alisisitiza kuwa hakukuwa na vurugu, ila kulikuwepo na kurushiana maneno ya kutambiana kati ya wanachama hao.

“Sasa katika hali kama hiyo utamwambia nani aache…mambo ya siasa utayaweza mama? Na hali hii inachangiwa na elimu ndogo waliyonayo viongozi wa kisiasa nchini,” alisema.

Pia alisema hali hiyo inachangiwa na ukosefu wa viwanja na kusema watu wanalazimika kufanyia mikutano katika viwanja vya kuchezea watoto.

Kwa muda sasa wanachama wa vyama hivyo wamekuwa katika vita ya kurushiana maneno na hata Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), ulifika hatua ya kusema utaanza kutumia nguvu katika suala hilo.

Hali hiyo inatokana na CUF kutoa hadharani miniti za vikao vya kusaka muafaka wa mpasuko wa kisiasa Zanzibar katika ya vyama hivyo, ambazo zilikuwa siri.

Umoja huo ulisema kuanzia sasa hautakaa kimya pale viongozi wa CUF watakapotoa maneno makali dhidi ya viongozi wa CCM na kwamba hakuna maana wala haja ya kuendelea na mazungumzo hayo kwa sababu CUF imedhihirisha haikuwa na nia njema ilipoingia katika mazungumzo hayo.

Msimamo huo ulitolewa na Katibu Mkuu wa umoja huo, Francis Isaac, alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu msimamo wao juu ya mazungumzo hayo.

Alisema wamechoshwa na mazungumzo yasiyokwisha, ambayo viongozi wa CUF wameyachukulia kisiasa na kushindwa kuonyesha dhamira ya wazi ya kutatua mpasuko wa kisiasa visiwani Zanzibar.

“Muda wa kuwabembeleza CUF umepita na UVCCM inawasubiri uwanjani katika uchaguzi mwaka 2010 na si kulilia ushindi wa mezani,” alikaririwa Isaac.

Kwa kuonyesha uzito wa kile alichokuwa anakisema, Isaac alibainisha kuwa UVCCM ndio injini ya CCM, na hawaoni sababu ya kuendelea kwa mazunguzo hayo na kama CCM inaona mazungumzo hayo yana umuhimu, basi wafikirie kuvihusisha vyama vingine na wala si CUF pekee.

“CUF ni mufilisi wa mawazo na wamejawa na madikteta wasiopenda kuona maendeleo ya Zanzibar.

“Nguvu tunazo, uwezo upo, na kuanzia sasa kama noma na iwe noma, tutapambana na wale wote wenye nia ya kuwachafua viongozi wetu,” alikaririwa Isaac.

Alisema ni ajabu kwa CUF kuimba wimbo wa kutaka kuundwa kwa serikali ya mseto, lakini inahofia kura ya maoni.

Aidha, Isaac alisema si kweli kuwa anayepinga kupatikana kwa suluhu visiwani Zanzibar ni CCM, bali Maalim Seif (Katibu Mkuu wa CUF), ambaye kuwapo kwa hali hiyo ni mtaji wa maisha yake kisiasa.

Hata hivyo, siku chache baadaye Rais Jakaya Kikwete alilazimika kuvunja ukimya katika suala hilo na kusema baada ya vyama hivyo kuweka misimamo yao kuhusu muafaka wa Zanzibar hadharani, sasa ni wakati wa kurudi mezani kuendeleza majadiliano.

Rais Kikwete alisema anaamini majadiliano hayo hatimaye yatazaa matunda mazuri kwa mustakabali wa Tanzania.

Alitoa kauli hiyo katika mazungumzo yake na Waziri wa Nchi wa Ufaransa anayeshughulikia mahusiano ya kimataifa na nchi zinazozungumza Kifaransa, Alain Joyandet.

“Naamini mambo yatakwenda vizuri. Hatimaye tutafanikiwa katika hili la mazungumzo ya muafaka,” alisema Rais Kikwete na kuongeza kuwa, kimsingi, CCM na CUF vinakubaliana kuhusu mambo ya kufanyika juu ya muafaka, na kuwa tofauti ni katika utekelezaji wa hayo yaliyokubaliwa.Maoni ya Wasomaji
Maoni yanayotolewa na wasomaji wa safu hii ni ya kwao na sio maoni ya kampuni ya Freemedia Ltd. Aidha sio maoni ya mtunzi au mwandishi wa habari au makala husika hapo juu. Maoni haya hayajahakikiwa wala kuafikiwa na kampuni ya Freemedia Ltd.
Maoni 26 yameshatolewa. (Nawe toa maoni yako!)
Hii inaashiria hali mbaya ya kisiasa nchini, na hali hii imetengenezwa na viongozi wetu wanaopenda madaraka kuliko amani na utulivu nchini. Viongozi hawa wanajua kikitokea cha kutokea wao watakuwa salama kwani ni wa kwanza kukimbia nchi na kuwaacha wananchi wakiuawa. Muda umefika kwa wananchi kuwasema viongozi hawa wabinafsi bila kuchoka, kwani sauti ya wananchi siku zote ina nguvu pale panapokuwa na umoja. Tuungane wananchi tuiokoe nchi yetu.

na Mtz, Dar, - 19.05.08 @ 09:14 | #11801

Chondechonde watani zangu,Msikurupukie mambo,waachieni wenyewe wa unguja na pemba.Ninyi mnachokitafuta nininini?Mnaogopa kuwaambia ukweli Mafisadiukweli,Mnaogopa kuwaeleza Wezi wa maliza uma kinagaubaga,Mnaanza kulumbana kuhusu vyama mapema ,Mnaonyesha nini kwa kizazi chenu kinachokuja ,Nawasihi watani zangu acheni UCCM NA uCUF angalieni maendeleo ya mkoa wenu.Bado uko nyuma kwa kila kitu.Mwanzo ilikuwa unapozungumzia Tanga basi ilikuwa Tanga kweli.Klichoiangusha mnakijua,Watani zangu hayo ya kulumbana kuhusu vyama waachieni wenyewe Wazanzibar,Uzanzibar na uzanzibara Upemba na UUnguja ,Maana wao waliupata uhuru kwa kutumia umwagaji wa damu toka kwa Sultani aliyekuwa anawafanya wananchi watumwa,na kumiliki aridhi pamoja na kodi zote kuzipeleka Uarabuni.Hawa hata wakiwekeana ubabe ni haki kabisa kwani walipata uhuru kwa sababu ya vizazi vyao vikae kwa uhuru.Je,ninyi watani Zangu cha kulumbania nininini?Kwani ikiwa kilamtu akikaa vikao vya chama bila ya kumbughudhi mwingine tatizo lipkowapi.Nawasihi watani zangu tujenge nchi na tupigane na mafisadi na sio chama fulanikigombane na chamafulani huo ni ukosefu wa elimu.Huu ni usia kwenu watoto wangu.Msilete fujo Nikija huko mtaniambia.

na SMwenyego, tz, - 19.05.08 @ 10:17 | #11809

Haya ni matokeo ya ubinafsi na uroho wa madaraka. CCM wamekuwa wakieleza kwamba CUF na hasa Maalim Seif wanalilia madaraka, lakini ukweli umejionyesha kwamba wao ndio wanaong'ang'ania madaraka.

Ni upuuzi kwa UVCCM kudai kwamba CUF wanapenda mazungumzo yasiyokwisha wakati wao ndio wanataka yaendelee mpaka kwenye kura ya maoni!! Kama CCM wanataka mazungumzo yaishe kwa nini wanazua ajenda mpya baada ya makubaliano? Hapo ni nani anapenda mazungumzo yaendelee? Ni dhahiri CCM wanataka yaendelee ili waendelee mpaka 2010 ambapo watajihakikishia tena madaraka kwa njia za kupinda.

CCM wanapaswa watambue kwamba watanzania wameamka na wanaweza kuelewa nini kinaendelea, nani mkweli na nani ******. Wamechoka na kuchezewa wao pamoja na haki zao.

Wajue kwamba wanajitia doa kubwa kwa kuwatuma vijana wao watishie amani ya nchi kimchezo. Matamshi ya UVCCM yanapaswa kulaaniwa kwa nguvu zote na wapenda amani wote bila kujali itikadi za vyama vyao. Amani sio mali ya mtu wala chama. Mpaka sasa hivi hajatokea kiongozi yeyote wa CCM akakemea yaliyosemwa na vijana, kwa hiyo kuna ukweli kwamba vijana hao walitumwa au walisema kinachokubalika kwenye chama chao.

Mzigo mkubwa unashushwa mabegani mwa Rais ambaye Tiafa linamtegemea afanye kil kinachotegemewa na Watanzania, wenye nchi. Kazi kwako Mheshimiwa Rais: ama uache uozo uendelee kwa kuwanyamazia na kuwalinda wahuni na mafisadi wa kisiasa au uwe mwaminifu kwa Taifa hili lililolazimishwa kuwa maskini na watu haohao ambao hawaoni haja ya kuwaheshimu.

Kumbuka: vita ikianza haitachagua kuyu ni CUF au huyu ni CCM; sanasana mtatuumiza sisi tusiohusika. Je sisi nani anatulinda?

na Amk, Dar, - 19.05.08 @ 10:17 | #11810

mimi nawashangaa sana hawa CUF wao sera za chuki na uhasama ndio wanapenda Mimi naomba sana viongozi wa CUF waache sera za chuki nani asiyemfahamu Maalimu seif kipindi akiwa kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar hadi akaondololewa madarakani CCM walijua hayo kuanzia kitambo hivyo CUF aacheni Vurugu

na mkula, Namanga, - 19.05.08 @ 10:45 | #11814

HIVI LEO WAZANZIBAR HAWANA KWANINI WAMEKUWA WANANYIMWA HAKI ZAO HATA ZILE ZA KISHEREA INAPOKUJA KUDAI HAKI ZAO MARA WANAULIWA AU KUFUNGWA MAGEREZANI MNAKUMBUKA WAKATI SEREKALI YA PILI YA MR RAIS ABOUD JUMBE WALIPOAMUWA KUWE NA SEREKALI TATU WAKAFUKUZWA NA KUFUNGWA HII LEO TUSINGWEKUWA NA HALI KAMA HIII INAONESHA DHAHIRI KUWA WAZANZIBAR WANAONEWA KWA MASLAHI YA WATU FULANI NA NDIO MAANA LEO HII UKWELI WA WIZI WA KILA AINA NDANI YA CHAMA NA SEREKALI UMEJITOKEZA ULIYOKUWA UNAFICHWA KWA KILA HILA NA HUKU WANANCHI KWA KUTOKUWA NAUPEO WA KILIMWENGU HUWA WANAPIGA MAKOFI KILA WANALOAMBIWA KWA WAKATI ULE SASA WAKATI UMESHABADILIKA CCM HAMTAKI KUBADILIKA

na Albert, TANZANIA, - 19.05.08 @ 10:48 | #11815

Tunapojadili masuala yanayohusu binadamu tuacheni ushabiki usio na kichwa wala miguu. CUF waliomba kibali cha kufanya mukutano wa hadhara na kukubaliwa. Kitendo cha CCM kupandisha vipaza sauti ili CUF wasisikilizane ilikuwa ni kuvuruga mkutano wenye kibali kwahiyo walihatarisha amani. Kwa kuepusha shari viongozi wa CUF waliamua wauvunje mkutano wao. Sasa hapa mpenda amani ni nani na mchokozi ni nani? Kama kawaida yao Polisi (CCM B) walishindwa kuwadhibiti CCM na laiti kama waliovuruga mkutano ule walikuwa ni CUF basi hapa tusemapo tungesikia wana-CUF kibao wamesweka ndani.
Sheria kuhusu mkutano inasema kwamba vyama vya siasa havitakiwi kuomba ruhusa kwa Polisi bali ni kuwaarifu ili waweze kuwapa ulinzi. Hata hivyo Polisi hujifanya kwamba wao ndiyo wenye amri ya kumruhusu nani afanye mkutano na nani asifanye mkutano, hasa inapokuwa muombaji anaipinga CCM. Sasa hata pale Polisi wanapotoa hiyo ruhusa, endapo CCM ndiye anayevuruga mkutano hakuna hatua inayochukuliwa.
Kwa mfano kule kwenye kampeni za kule Kiteto Mheshimiwa Komba alivamia uwanja wa kampeni ambao ulikuwa utumiwe na CHADEMA na akakataa kuondoka mpaka hamu yake ilipomwisha. Kafanywa nini? Kuna wale vijana wa CCM kutoka Dar es Salaam waliowavamia viongozi wa CHADEMA na kuwajeruhi. Mpaka sasa wamefanywa nini.
Tatizo la serikali ya Tanzania kutumia vyombo vya dola kwa manufaa ya CCM liko kila mahali na inatuathiri sote. Mahali popote CCM inapozidiwa nguvu lazima watumie vyombo vya Dola. Wamemfanyia hivyo Bwana Mapesa (Cheyo) kule Magu katika uchaguzi mdogo, wamewafanyia CUF kule Tunduru katika uchaguzi mdogo, na sehemu nyingine nyingi tu.
Sasa kama tunaguswa na watatizo ya Kenya, kama tulikerwa na Nduli Idd Amin, kama tuliikomboa kusini yote ya Afrika iweje tatizo likiwa Pemba ama Unguja tunasema si letu tuwaachie wenyewe? Wenyewe wapi? Historia inatwambia kwamba mipaka ya Zanzibar ni pamoja na maili 10 za ukanda wote wa pwani ya Tanzania Bara. Hebu muulizeni Zakhia Meghji mama yake alitoka wapi (Kilwa)? Juzi tumemsikia Mohamed Seif Khatib akisema katokea Tanga, Naambiwa hata komandoo Salmin Amour pia katokea Tanga. Huyo Seif Shariff Hamadi ana ndugu zake wa damu hapo Kwanjeka Tanga walioishi huko kabla ya Mapinduzi ya Zanzibar. Mzee Ruhusa na Kuchi Mloo si Wazaramo wale na vijiji vyao vyenye ndugu zao vinajulikana. Huyo Ramadhani Nzori si mtu wa Duga ya kwa Mwanzori Tanga (Mdigo). Sasa mwafikiri misiba ikitokea Pemba na Unguja watalia Wapemba tu na Waunguja? Mtu kama hana hakika na jambo bora ake kimya.

na Al Assad, Sungai Pusu, - 19.05.08 @ 08:15 | #11817

WATANZANIA WENYE NIA NJEMA KATAENI KUPIGANA.TUSITUMIWE KATIKA JANJA YA CCM WANATAKA VURUGU IPAMBE MOTO ILI KUZIMA KELELE ZA UFISADI WAO.BAKINI NA AJENDA YA UFISADI,WAMEFILISIKA WATUMIA TATIZO MOJA KUFICHA LINGINE.MSIKUBALI KAMWE.CCM,CUF HATUTAKI VITA HAPA TUNATAKA NCHI YENYE AMANI.KWA SASA HIVI VITA NI YA MAFISADI TU NAO WANAJIJUWA VEMA.TULIENI ZUNGUMZENI KWA AMANI.
CUF IONENI JANJA YA CCM KUVURUGA AMANI ILI AJENDA YA MWAFAKA ISIJADILIWE.
WEKENI BOLI CHINI MUONE WANAVYOKURUPUKA
,HAMKUONA MLIPOTOA HADHARANI UKWELI WALIVYOKURUPUKA NA KUSEMA NGUVU TUNAZO KUPITIA KWA VIJANA WAO WA CCM.
WAMEISHIWA HOJA PANUENI MAPAMBANO YA HOJA MUONE WANAVYO WEWESEKA.
KATAENI KUCHEZA NGOMA YAO YA VURUGU.

na yuli - 19.05.08 @ 08:18 | #11818

na yuli - 19.05.08 @ 08:19 | #11819

mkula, Namanga! wewe unayaelewa mambo au umegubikwa na ufisadi wa CCM tu? unajuwa sababu ya msingi kwa maalim seif na wenzake kwa pamoja kufukuzwa uanachama na chama cha mapinduzi? ndugu yangu wewe uko mbali sana na huelewi kilichoko zanzibar ni kheri unyamaze tu kuliko kuandika vitu vya namna hii.unaposema CUF waache vurugu una maanisha nini? au hukuelewa hii article ya mwandishi? article imeandikwa kwa kishwahili fasaha, basi hata kiswahili rahisi huelewi? ama kweli mzee bongo mafisadi wataendelea kula maisha sana kwa namna wananchi wengi kama mkula walivyo wengi.pole sana ndugu yangu mkula Mungu atakuasaidia na kufunua upeo wako na kuna siku utawafahamu mafisadi.

na vundo, zanzibar, - 19.05.08 @ 08:28 | #11821

Inasikitisha pia inauma kuona mambo haya ya hujuma, ubinafsi, vurugu, majigambo nk, yanajitokeza hapa Tz nchi inayojivunia amani na utulivu. Napenda lawama zangu zimfikie Ndg Seif shariff Hamad kwa kuwa chimbuko la vurugu na migongano visiwani Zanzibar chini ya kivuli ya Chama cha CUF!! Kama Seif ananisikiliza namwomba ajiondoe kwenye chama au aachane na siasa ili ufumbuzi upatikane au chama cha CUF ifutwe ili migongano ipate suluhu. Seif ulishindwa kuikomboa kisiwa hicho ukiwa na umri unaostahili iweje leo uanze kuleta chokochoko? Yafaa ubanwe ili hivyo virusi vyako vyenye chuki visienee zaidi.

na Samaki, Ziwani-Tz, - 19.05.08 @ 08:48 | #11823

Maganga, Maalim seif ni mzanzibar halisi mwenye uchungu na zanzibar, alikataa kuburuzwa zanzibar na Tanganyika Mzee Amani na wenzake ni mapandikizi tu! Hawana uchungu wowote na zanzibar. Zanzibar imepoteza hazi na heshima yake kupitia vawala wa ccm. Cuf ina nia ya kuirudishia zanzibar hadhi yake na kuwashughulikia mafisadi na vibaraka walio itosa zanzibar.

na Znz - 19.05.08 @ 09:13 | #11824

Inasikitisha sana jinsi hali ngumu ya maisha inavyotutafuna sisi walalahoi mfumko wa bei usiseme hasa vifaa vya ujenzi.Maisha bora tuliyoahidiwa ndoto kuyapata kwani walichokitaka wanasiasa kutoka kwetu wameshakipata hivyo wametusahau.Hongereni kwa kutunyanyapaa sisi waajiri wenu muda tena utafika mtakuja kutudanganya.Tunatamani kujenga nyumba bora na za kudumu tupunguzieni mfumko wa bei ya saruji hasa kwa kupunguza kodi na gharama za umeme kwenye viwanda vya saruji ili nasi tuwe na maisha bora kama nanyi wanasiasa,la sivyo nchi itageuka kwani hatufurahi mafisadi wa awamu ya nne kutumega tukiwa hai.

na Emmanuel, Dodoma,Tanzania, - 19.05.08 @ 09:50 | #11829

SADAKTA MZEE ABDEID KARUME HAKUWA MZANZIBARI BALI KULI TU AMEKUJA KUT0KA NYASALAND ( MALAWI ) KUJA KUTAFUTA RIZKI ALWATAN ZINJIBARI NA NDIO MAANA HAKUWA NA UCHUNGU NA ZANZIBAR NA KUIFISIDI KUUNGANA NA ******** NYERERE LAANATUYLLAH ALAYHI ( HUKO KABURI ANAPAGWA MARUNGU UZURI KWA USHENZI WAKE ) NA HIII NDIO TIJA SASA KUNA MTOTO WA HUYO NYOKA ANAJARIBU KUENDELEZA YA BABAYE KUZIDI KUIFISIDI ZANZIBAR ALWATAN AL GHALI , ALKINI TUNAMWAMBIA KUWA ZANZIBAR ITAKOMBOLEWA NA WAZANZIBARI KUTOKA KWENYE MAKUCHA YA KANISA LA TANGANYIKA INSHALLAH

na Mpemba, Zanzibar, - 19.05.08 @ 10:01 | #11830

ccm wanajiandalia bomu litakalo walipukia mda si mrefu.waache jeuri yao.watanzania sasa wameshaelimika.ccm wasome alama za nyakati.tembelea mashuleni na vyuo vikuu usikie jinsi vijana walivyochoshwa na sera za ccm.tatizo la ccm hawataki kuambiwa ukweli.hata mwananchi wa kawaida sasa ameamka.ccm nawashangaa mnapokataa watu wasiwaiteni MAFISADI.eti mnasema chama ni safi na kisihukumiwe kwa ufisadi wa mtu mmoja.hivi chama ni nini?chama ni watu wanaokiunda.LOWASA na CHENGE ni moja kati ya wana ccm.inakuwaje mtuhumiwa wa kula pesa za wananchi apokelewe na viongozi wa mkoa na wilaya kama vile ni shujaa!mbona viongozi wa juu ccm hamjakemea hili swala waziwazi?inaonyesha mmebariki uozo huo.ndo maana wananchi wameaanza kuwachokeni.ccm ndo mmesababisha mpasuko uliopo zanzibar.kumbukeni maneno ya mwl NYERERE mara tu baada ya uchaguzi wa 1995.nyie viongozi wa CCM HISTORIA ITAWAHUKUMUNI

na dsm, dar, - 19.05.08 @ 10:32 | #11839

Hizi siasa za kutunishiana misuli hazitatufikisha popote.kila mtu anajiona mwenye haki,na ndipo hapo tunapokwama, kiini cha tatizo hili.Mimi kwa upande wangu ninaamini kabisa kwa hii miaka miwili iliyobaki kabla ya uchaguzi mkuu, CUF na CCM wanaweza wakatulia na kupanga mikakati ya kumaliza mikakati yao.na kwa kuanzia, ni utekelezaji wa kuwa na tume huru ya uchaguzi, ambayo wajumbe wake watatoka pande zote,hata kama mwenyekiti lazima ateuliwe na Rais.na huku kukosa tume huru ndiko kunakosababisha matatizo katika chaguzi zetu Afrika nzima

na David, Dar, - 19.05.08 @ 10:39 | #11840

S MWENYEGO KWEL KABIS WAKIN SHEMEJI NIN MNAONYESHA UKO TANGA?TUNAKA MTAFURUKU WA MAENDELEO KWENYE MKOA WA TANGA,SI PICHA NZURI KAMA MUANDISH ALIVYO ANDIKA BABA NA MWANA WALIVYOKUWA WAKIJIBISHANA HATWENDI HIVYO JAMAN KAMA MTAANZA HAKIKA MTAANZA KUSUSIANA KWENYE SHUGHULU ZA KIJAMII KAMA HARUSI NA MAZIKO.KWA SIFA TANGA INA KILA KITU UBINADAM DIN HATA HAWA WAKE ZETU MENGINE SIJUI!HAYO MAMBO TUWE NA MAKIN NAYO SANA
Mtz mashariki ya mbali

na mtz mashariki ya mbali, far weast, - 19.05.08 @ 11:43 | #11853

MTOA MAONI KWA JINA LA MPEMBA NO.11830
LABDA UKO KATI YA WATU WANAOTAFUTWA SANA WAKIWA HAI AU KICHWA NA FBI.
MAONI YAKO HAYAWEZI KUSAIDIA WATU WA PEMBA KUISHI KWA RAHA NA AMANI!! MAONI YAKO YAWEZA KUIFANYA PEMBA IWE KAMA AFGHANISTAN AU IRAQ!!!
PIMA MANENO YAKO!!!UNAISHI TANZANIA KWENYE NCHI YA WASTAARABU NA WAPENDA AMANI.

na Sammy - 19.05.08 @ 11:50 | #11855

sammy wewe hujuwi unocho ****** kuhusu wabemba bora usichagiye funga mtaro wako ok kuhusu FBI nyiyo waloitosa USA ikaDharaulika na kufilisika kisiasa hata viogozi waFBI WEGI WAMETIMULIWA KAZI KWAKUTOA UONGO NA UPOTOSHAJI NA AMANI UNAYOZUGUMZAWEWE NI IPI?KWANI AMANI BILA YA MATENDO SAWA NA MFU,KUHUSU USTAARABU WAKUWANAJISI WATOTO WADOGO KUWAUWA ,KUBAKA WAKE ZAO

na ABORIGINAL, usa dc, - 19.05.08 @ 12:44 | #11869

from Dar Leo
16.05.2008 0440 EAT (1304 GMT)

CUF, CCM, WASUSIANA MAZISHI, HARUSI

Na Mwandishi Wetu

ATHARI za kuparaganyika kwa mwafaka kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama Cha Wananchi (CUF) uliolenga kumaliza mpasuko wa kisiasa kisiwani Zanzibar zimeanza kujitokeza kwa kasi katika visiwa vya Unguja na Pemba.

Shirikika la Utangazaji la Uingereza (BBC) leo asubuhi limeripoti habari za wakazi wa visiwa hivyo kuanza kubaguana katika shughuli za kijamii ikiwemo, misiba, harusi, kuuza na kununua bidhaa madukani pamoja na kwenye vyombo vya usafiri.

Pia limeripoti kuwepo kwa vitisho katika visiwa vya Unguja ambapo baadhi ya wakazi wenye asili ya Pemba wamedai kuwa wamekuwa wakikuta vipeperushi kibao vimebandikwa kwenye nyumba zao zao, vikiwataka warudi kwao Pemba.

Akizungumza kwa uchungu mkazi mmoja wa Unguja ambaye hakujitaja jina amesema hali hiyo imewachosha na kwamba anaona ni bora warudi Pemba kwa kuwa watakuwa hawaishi Unguja kwa usalama.

Alipoulizwa kwamba inawezekana hali hiyo ya kuwepo vipeperushi imechangiwa na Wapemba kusema kuwa hawatapeleka vyakula vyao Unguja kwa kuwa wanaona wao wanatengwa, amesema maamuzi hayo ni yao wenyewe (Wapemba), ndiyo silaha wanayoona wanayo kwa kuwa wao hawana mamlaka.

Amelalamika kuwa ingawa vitisho na vipeperushi vimekuwa vikitolewa, Serikali haijaonyesha kukemea hali hiyo na haijaeleza hatua inazochukua ili kukomesha.

Mkazi mwingine wa Pemba amesema mgawanyiko kati ya watu wenye itikadi tofauti za vyama vya CUF na CCM sasa si wa kificho tena, wamekuwa hawashirikiani katika shughuli za kijamii kama misiba na harusi na hata kususiana katika vyombo vya usafiri na kununua bidhaa dukani.

Mwafaka kati ya CCM na CUF wa kuondoa mpasuko wa kisiasa Zanzibar ulianza kuingia dosari baada ya Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika Butiama hivi karibuni kuzima matumaini ya CUF ambao walitarajia kwamba NEC ingeidhinisha kusainiwa kwa muafaka huo na kuunda Serikali ya mseto visiwani Zanzibar.

Badala yake NEC ilitaka kamati ya muafaka kukaa tena na kupitia mapendekezo yake na kisha kuwahusisha wananchi wa Zanzibar kupiga kura ya maoni kuhusu suala hilo jambo ambalo lilipingwa na viongozi na wanachama wa CUF.

Baada ya CUF kutamka kupitia Katibu Mkuu wake, Seif Sharrif Hamad kwamba wana imani na Rais Jakaya Kikwete tu kuhusu mwendelezo wa mwafaka, jana Rais Kikwete alitoa tamko kuitaka kamati ya CUF kukutana na wenzao wa CCM ili kuzungumza na kwamba CCM ilitoa mapendekezo tu.

Mambo mengine yaliyojitokeza sambamba na kwenda mrama kwa mazungumzo ya mwafaka ni kujitokeza kundi la watu 10,000 walioandika majina na saini zao wakipendekeza kujitenga kwa Pemba na kupeleka waraka katika ofisi za Umoja wa Mataifa.

Hali hiyo imesababisha kuwepo kwa kamatakamata kisiwani Pemba kwa watu wanaotuhumiwa kwa uchochezi, na kufanya baadhi ya watu kuacha majumba yao na kuishi mafichoni.

www.darleo.co.tz

na David, Dar, - 19.05.08 @ 13:17 | #11872

Kibao chawageukia Wapemba
2008-05-18 11:44:54
Na Mwinyi Sadallah,Zanzibar

Wasiwasi umetanda visiwani Zanzibar kufuatia kusambaa kwa vipeperushi vinavyowataka wakazi wa Pemba kuondoka haraka kisiwani Unguja na kurudi kwao.

Kukamatwa kwa wananchi saba wanaohusishwa na kosa la uhaini kumeonekana kusababisha chuki na uhasama wa kisiasa miongoni mwa wananchi wa Zanzibar.

Hali ya kisiasa visiwani hapa inazidi kuwa tete baada ya wananchi wa Unguja nao kusambaza vipeperushi vinavyounga mkono kisiwa cha Pemba kujitenga na vingine vikiwataka wapemba waondoke.

Baadhi ya wananchi waliohojiwa na Nipashe jana walisema sasa ndio itajulikana ipi mbichi na ipi mbivu, wenginewanasema wapemba ndio watakaopata shida zaidi iwapo wataamua kujitenga.

```Kuendelea kukamata watu Pemba ni sawa na kukaribisha machafuko, tunaomba Rais kikwete kusitisha mara moja zoezi hilo,``alisema Bw,Said Kombo mkazi wa Bububu.

Bw.Kombo alisema hivi sasa watu 10,000 waliosaini waraka huo wametishia kujisalimisha katika vituo vya polisi kitendo ambacho kinaweza kusababisha vurugu.

Wakizungumza kwa nyakati tafauti walisema hali ya kisiasa Zanzibar ilianza kutulia mara tu baada ya Rais Jakaya Kikwete kukiri kuwepo mpasuko wa kisiasa na kuahidi kuushughulikia.

``Lakini sasa mambo yamegeuka na hali ni ya kusikitisha,`` alisema mkazi mmoja wa Unguja.
Bw. Salum Ahmed mkazi wa Mchangani mjini Unguja, alisema kukamatwa kwa watu hao kumerejesha hali ya wasiwasi na baadhi ya watu wameanza kukimbia maeneo wanayoshi.

``Kimsingi makosa ya uhaini ni pale watu wanapotaka kupindua serikali au kumuua Rais sidhani kama kutoa maoni ni kosa la uhaini.

Mbona waliokata umoja wa kitaifa na kusema hapana cha mseto hawakuambiwa wanahatarisha umoja wa kitaifa``, alisema Bw. Salum mbaye ni mwalimu.

Mfanyabiashara maarufu Zanzibar , Bw. Mohammed Raza, alisema serikali ya Muungano inapaswa kuwaachia watu hao waliokamatwa ili kuendeleza nia njema ya mazungumzo ya mwafaka baina ya CCM na CUF.

Alisema jambo la msingi kwa sasa ni kwa CCM na CUF kuendelea na mazungumzo ili kumaliza mpasuko wa kisiasa uliopo Visiwani.

Alisema matatizo yanayojitokeza Zanzibar hivi sasa yanachangiwa na mfumo mbaya wa
Katiba ya Muungano na ya Zanzibar.

Bw. Masoud Suleiman alisema tamko la Polisi kuwa kuna watu wengine wanaendelea kutafutwa litasababisha mazingira ya wasi wasi na baadhi ya wananchi kuanza kukimbia maeneo yao.

``Ndugu zangu wako Pemba na nimesikia kuna watu wameanza kukimbia, sasa mazingira kama haya yanaibua siasa za chuki``, alisema.

Alisema wananchi waliopeleka barua ofisi za Umoja wa Matifa jijini Dar es Salaam walikuwa wakitoa maoni yao kama Katiba ya nchi inavyowaruhusu na haikuwa busara kuwakamata na kuwafungulia mashitaka.

``Mbona kuna Wabunge wa CCM katika utawala wa mzee Mwinyi walipeleka hoja Bungeni ya kuwepo serikali tatu, kwa nini hawakukamatwa na kufunguliwa mashitaka ya uhaini,`` alihoji Bw. Suleiman.

Wakati hali hiyo ya wasi wasi ikionekana wazi huku vipeperushi vya kurushiana ****** vikizagaa, Rais wa Zanzibar ,Bw.Amani Abeid Karume amenukuliwa akisema hali ya Zanzibar ni ya amani na shwari tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005.

Rais Karume aliyasema hayo jijini Washington Marekani alipokuwa na mazungumzo na Watanzania wanaoishi nchini humo.

SOURCE: Nipashe
www.ippmedia.com

na David, Dar, - 19.05.08 @ 13:24 | #11874

CUF= Chama cha Ugomvi na Fujo

na Gwagwa, Mwanza, - 19.05.08 @ 13:31 | #11875

JK okoa mwafaka wa CCM na CUF ili amani isitoweke Tanzania.Porojo za akina Makamba na wenzake zitatuletea matatizo kwani hawajiamini kuiwakilisha CCM katika mazungumzo na kuwafanya kutegemea maagizo kutoka nje.

na Busara, Tz, - 19.05.08 @ 13:33 | #11876

HAWA CUF NI ********* SANA SASA WANALETA VURUNGU ZA NINI JK ANGALIA POROJO HIZO

na JUMA HAMISI, DODOMA, - 19.05.08 @ 14:11 | #11884

Tatizo siyo la Viongozi wa CUF wala wa CCM wala serikali. Tatizo ni la hao wote wanaojiita wafuasi. Kama unaakili timamu badala ukapalilie bustani wanao wale unaenda kupigana. Kwani ukipigana kwa nguvu Kikwete atakupa uwaziri kama wewe ni CCM? Au kama ni CUF unadhani Maalim Seif akipewa bure uwaziri kiongozi kwa sababu tu ya muafaka atakupa hata ukuu wa wilaya?

Vyeo wafaidi wengine ngeu muambulie nyie. Wajinga ndiyo waliwao.

Kalagabaho<<<<<<

na mviziaji, Bongo, - 19.05.08 @ 14:25 | #11888

ABORIGINAL naona uko kwenye mistitu ya Australia usijipachike kuwa USA. Kusema uongo kwa baadhi ya maofisa wa FBI haina maana imekufa na wala haina maana imeacha kufuatilia waharibifu.
Huko USA una kazi ya zizi nini?
Rudi Tanzania tunaishi kwa amani. Njoo Pemba ukaongeze pato la karafuu na mwani. Hutabakwa sababu unafanya kazi zizini.

na Sammy - 19.05.08 @ 15:58 | #11898

YOTE HAYA ALAUMIWE KIKWETE ANAYEPENDA KUSAFIRI NA KUJIFANYA KUSURUHISHA MIGOGORO YA WENGINE WAKATI YEYE YA KWAKE INAMSHINDA. CCM NDIO WASSHENZI NA MAHARAMIA WANAOTAKA KUVURUGA AMANI YA NCHI HII

na Said Ali - 19.05.08 @ 16:33 | #11899
 
Sasa tumeanza kujisahau ndugu zangu, hizi siasa za kurushiana maneno pia zina madhara yake, tuwe makini kwa hili
 
Lolote litakalotokea na kusababisha kupotea kwa 'amani' Tanzania basi hakuna wa kulaumiwa ila ni msanii JK na CCM.
 
kuna mambo mengine kichekesho mtu akikosana mwenziwe JK wakiachana JK wakigombeana Kuni JK

kazi si ndogo
 
Cha kushangaza kunapokuwa na 'habari nzuri' kuhusu Tanzania ambazo siku hizi ni adimu sana kuzisikia basi sifa zote arushiwe JK mfano JK boys wanaposhinda lakini wanakuwa Taifa stars wanapopigwa bao, lakini kunapokuwa na habari mbaya basi JK siye wa kulaumiwa! rais wa nchi unasikia wafuasi ndani ya chama chako wanatoa kauli ambazo zinatishia amani ya nchi, nawe unaamua kukaa kimya bila kukemea kauli hizo. Halafu yakitokea maafa kufuatia kauli hizo wewe si wa kulaumiwa! ama kweli Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu.

Marehemu Nyerere, Mwenyezi Mungu amalaze mahali pema peponi, kamwe asingekaa kimya kauli za kipumbavu zinazotishia amani ndani ya nchi zinapotolewa na wafuasi wake.
 
''BABU ATAKA KUSEMA''
USIWE NA MASHAKA SANA KUHUSU AMANI YA NCHI HII SABABU
WANAOTAKA KUHARIBU AMANI YA NCHI HII AMBA HATA SIAFU
NA VIROBOTO NA VIUMBE WASIO NA UTASHI NA WASIO NA UHAI
WANAIFAHAMU AMANI HIYO,MUNGU ALIYE HAI ATAWAHARIBU WAO
KWANZA NA KAMA WANANCHI NA SISI WENYEWE TUTASHINDWA
NA PIA IKISHINDIKANA KWA NJIA ZOTE HIZO BASI NIKUPE UHAKIKA
KUWA MWENYEZI MUNGU HASHINDWI NA JAMBO LOLOTE LILE
NIKIMAANISHA KUWA HATA KWA ''MAUTI'' WATANG'OOKA NA PIA
TUOMBE UZIMA WIKI HII NITAWEKA HEWANI UNABII WA MTUMISHI
MMOJA WA MUNGU ALIYETOKEA HUKO NG'AMBO,VITA NI VYETU
LAZIMA TUPIGANE MPAKA NCHI YETU IWE NA HESHIMA KUBWA
KABISA NA IHESHIMIKE DUNIANI POTE KATIKA JINA LA YESU,
''I LOVE YOU TANZANIA MY MOTHER LAND AND HOME LAND''
 
Tumeyaona yaliyotokea Kenya, Burundi, Rwanda na nchi nyingine mbali mbali duniani. Mdharau mwiba mguu huota tende, ni rahisi mno kuipoteza amani, lakini kuirudisha ni kazi kubwa sana.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom